Hivi Rama Dee aliwakosea nini watanzania

Ngushi

JF-Expert Member
Jul 8, 2016
9,069
18,347
Wakuu, Leo katika pitapita zangu huko you tube nimekutana na video ya msanii Rama dee inaitwa - Kipenda roho
Aisee ni bonge moja ya rnb song
Kinacho nishangaza ni kwanini haikupewa na mpaka sasa haipewi air time ya kutosha kama video nyingine?
Basi hata ile kuzungumziwa kwenye social network sijawahi kusikia!
Tatizo nini kwa msanii huyu?
Nimeshindwa tu kuweka link ya hiyo video hapa ila ni mziki mzuri sana.
Video nzuri unaitazama mpaka nerve sinasisimuka nikakahisi JOE THOMAS amehamia bongo!!

Ndio kitu kilichonisukuma kuuliza huyu mtu aliwakosea nini watanzania? Kama yupo humu awaombe radhi aliowakosea video nzuri kama
ile haikufaa kuishia pale!!

Karibuni tujadili na maoni vilevile yanaruhusiwa huenda yatamfikia
 
Wakuu, Leo katika pitapita zangu huko you tube nimekutana na video ya msanii Rama dee inaitwa - Kipenda roho
Aisee ni bonge moja ya rnb song
Kinacho nishangaza ni kwanini haikupewa na mpaka sasa haipewi air time ya kutosha kama video nyingine?
Basi hata ile kuzungumziwa kwenye social network sijawahi kusikia!
Tatizo nini kwa msanii huyu?
Nimeshindwa tu kuweka link ya hiyo video hapa ila ni mziki mzuri sana

Ndio kitu kilichonisukuma kuuliza huyu mtu aliwakosea nini watanzania? Kama yupo humu awaombe radhi aliowakosea video nzuri kama
ile haikufaa kuishia pale!!

Karibuni tujadili na maoni vilevile yanaruhusiwa
Huyu jamaa anajua huo wimbo ni shida. Changanya nyimbo za ben pol hazioni ndani kwa kipenda roho.
Ila ndiyo hivyo watz wengi kama hawaoni na wengine hawamjui.
Hapo ndipo ujue mziki ni zaidi ya kuwa mwimbaji mzuri.
 
Aisee kweli kabisa mkuu! nimejiuliza maswali mengi sana nimekosa majibu
 
Jamaa aliingia kwenye vita asiyo iweza,

Hapo ni sawa ni Kenya walivyo ingizwa mkenge na Mmarekani kwenye ishu ya Somalia

Wenzake walisha sanda wakaenda kuomba msamaa kwa Boss Ruge

Mwacheni hadi akili imkae sawa ndiyo atajua madhara ya kuingilia ma beef yasiyo mhusu

Mwangalieni Dj Choka alivyo potezwa baada ya kuwa upande wa jay dee kipindi bifu la ruge na jay de
 
wengi wa watu maarufu na wasanii maarufu huwa wanatumia kimbolo uchawi ndo maana unaona kuna wasanii (waimbaji wa mziki) au wachezaji ni wakali lakini hata kujulikana hawajulikani
 
Uteam wenu unawavunja moyo wasanii wengine.
Kwa rnb bongo wakwanza ni rama dee anakuja steve then qchila then bele 9 alafu ndo hao wakwenu hata hawjulikan wanaimba aina gani ya mziki
 
Uteam wenu unawavunja moyo wasanii wengine.
Kwa rnb bongo wakwanza ni rama dee anakuja steve then qchila then bele 9 alafu ndo hao wakwenu hata hawjulikan wanaimba aina gani ya mziki
Siyo u team yani hii ni kawaida duniani kote... kuna waimbaji wakali ambao watu wanawakubari lakini siyo mashuhuri wala hawaingizi pesa nyingi ka wengine.
Mziki ni zaidi ya kujua kuimba.
Rama D anajua kuliko akina ben pol, lakini ben pol tz anafahamika kuliko rama d na ben pol hana team.
 
16 Reactions
Reply
Back
Top Bottom