Hivi Rais wetu yuko Serious? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Hivi Rais wetu yuko Serious?

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Bobby, Mar 3, 2009.

 1. B

  Bobby JF-Expert Member

  #1
  Mar 3, 2009
  Joined: Jan 10, 2008
  Messages: 1,682
  Likes Received: 197
  Trophy Points: 160
  Jana kwenye taarifa ya habari ya saa 2 usiku kwa bahati niliona issue ya ziara ya ghafla ya rais katika bandari ya Dar-es-salaam.

  Wakati ninampongeza rais kwa ziara hiyo ya ghafla ninapata tabu kidogo na seriousness ya mkuu wetu wa nchi kwenye mambo muhimu kama hili la msongamo usio wa lazima katika bandari yetu ya Dar. Kwa macho yangu nilimwona na kumsikia rais akisema anawajua wazembe (alihofu hata kuwaita wazembe) na kwamba anawapa muda (kama alivyowapa walarushwa) wa kujirekebisha wasipofanya hivyo atawaumbua kwa maboss (yeye ndio mkuu wa nchi sijuwi na maboss gani tena hao) wao. Hili ni tatizo la muda mrefu infact kuna nchi zinafikiria kuacha kutumia bandari ya Dar rais anatoa muda hasemi ni muda gani lasivyo anaumbua mtu. Sikujuwa kama bado tunao muda wa kuumbuana kwenye hili zaidi ya kuchukua hatua mara moja.

  Boss wa TRA amesema industry ya transit na transport inaingizia mapato taifa kuliko kilimo (ambacho tumekiua) na Tourism lakini bado tunacheka na hatuchui hatua thabiti. Binafsi ninasafirisha mizigo kwenda DRC, nina staff 200 hivi so jamaa wakijitoa familia zaidi ya 200 zitakuwa affected kupitia kwangu peke yangu na mimi ni tansporter mdogo tu. Achilia mbali effect kwenye wauzaji wa mafuta, vipuri na wengine.

  Bado ninajiuliza ni lini tutakuwa serious na issues serious jamani watz?
   
 2. N

  Nyauba JF-Expert Member

  #2
  Mar 3, 2009
  Joined: Jul 10, 2008
  Messages: 1,098
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 135
  mkuu heshima kwa mada.
  binafsi nilimshuhudia na kwa kweli (raisi) asipobadilika ataendelea kudharaulika kwa wasaidizi wake na kuongeza kasi ya umaskini kwa jamii anayoiongozaaa.

  huyu mkulu nahisi ana VERY SERIOU PERSONAL PROBLEM. Stateman hauwi vile na kauli za ajabu ajabuuuuu.... eti kitilya nitakupatia majina ya hao watu wa maktabaa..hivi hilo anahaja ya kutaja majina au kubadili kabisa mfumo wa kiutendaji wa hicho kitengo cha TISCAN!!! Huyu tumempatia heshima ya kuanzaisha vita (amiri jeshi mkuu) leo anajibizana na watumishi wa kaidara fulani ambao kwanza hawastahili hata kujibizana nae kiutendajiii(defenseless)....

  jamani hili taifa we need NEW FORMULA FOR NEW DIRECTION...

  JK ACHA MASIHARA UNAUMIZA UCHUMI NA WANANCHI KWA UJUMLA...
   
 3. MduduWashawasha

  MduduWashawasha JF-Expert Member

  #3
  Mar 3, 2009
  Joined: Mar 5, 2008
  Messages: 1,568
  Likes Received: 407
  Trophy Points: 180
  watu walionywa lakini ndo mkamchagua wenyewe.huu mzigo tunao mpaka 2015.hopefully jamaa watakuwa hawajajitoa na nchi itakuwa haijaparamganyika.
   
 4. Zak Malang

  Zak Malang JF-Expert Member

  #4
  Mar 3, 2009
  Joined: Dec 30, 2008
  Messages: 5,410
  Likes Received: 18
  Trophy Points: 0
  Tatizo langu hasa na rais katika ziara yake ya huko bandarini ni ile kauli yake ya kusema orodha ya majina ya wakwepa ushuru anayo, na ataikabidhi kwa mkuu wa TRA kuwashughulikia. Hii si njia sahihi katika masuala ya kupiga vita ufisadi na nathubutu kusema kuwa ni siasa tu, na pengine hata ni usanii -- kwa sababu haikuwa lazima kabisa kwa Rais kutangaza hivyo hadharani. Kimya kimya angeweza kumwita mkuu huyo wa TRA na kumkabidhi list -- na kumwambia yeye (Rais) anatarajia kuona results dhidi ya watajwa.
  Kutangaza hadharani ni kuonyesha tu kwamba anajali na angependa wekwepa ushuru washughulikiwe. Kwa upande mwingine, mkuu huyo wa TRA atakuwa amepata 'nguvu' ya kuwashughulikia hata maswahiba wake kwani atasema "sorry, siyo mimi bwana, ni agizo la Rais."
  Wananchi tungependa tu kuona results -- kuonyesha kuwa hakika wakwepa kodi wanashughulikiwa mara moja -- bila ya kelele nyingi za utangulizi -- zinazotangaza dhamira ya kuwashughulikia mafisadi!
  Mfano mwingine: Miaka michache iliyopita, wakati Magufuli akiwa waziri wa masuala ya barabara, alihututubia mkutano wa wafanyakazi wa Tanroads na kusema kuwa amegundua ufisadi katika ununuzi wa magari ya idara hiyo uliofanywa na baadhi ya maofisa wakuu -- magari yalinunuliwa kwa bei maradufu ya bei yake halisi -- kwa hivyo ufisadi ulikuwa umetendeka.
  Waziri alifanya usanii tu -- nia ni kuonyesha eti ufisadi unamkera, kwani issue iliishia hapo tu, hatukuelezwa tena kilichotokea. Wananchi tulitegemea Magufuli asubiri kwanza hadi uchunguzi ukamilike naye baadaye atangaze tu kuwa "fulani na fulani wamefikishwa mahakamani kwa ufisadi kuhusu ununuzi wa magari ya Tanroads." TUNATAKA RESULTS jamani, siyo maneno ya dhamira tu!
   
 5. Masanilo

  Masanilo JF-Expert Member

  #5
  Mar 3, 2009
  Joined: Oct 2, 2007
  Messages: 22,303
  Likes Received: 168
  Trophy Points: 160
  Mkwere hawezi kuwa serious hata siku moja! Angalia Chalinze amekuwa mbunge miaka mingi maendeleo habure miangu! sitegemei kipya kwa huyu muungwana...kule kule list ya wala rushwa, majambazi, wafanya biashara ya kulevya ninayo, wenye vyeti vya Kugushi Kamala et al anayo sasa kipi kipya Muungwana?
   
 6. M

  MzalendoHalisi JF-Expert Member

  #6
  Mar 3, 2009
  Joined: Jun 24, 2007
  Messages: 3,869
  Likes Received: 116
  Trophy Points: 160
  Sasa kama anawajua sii awachukulie hatua haraka??

  Nini anangojea??
   
 7. Elusive

  Elusive JF-Expert Member

  #7
  Mar 3, 2009
  Joined: Nov 26, 2008
  Messages: 223
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 35
  Inaonekana wazi hawajui wazembe, ndio maana anazungumza kijumla jumla kutisha kwa kutegemea watajirekebisha, hiyo ni sawa na kumtisha mtu ambaye huwezi kupigana nae, akitunisha msuli wewe unakimbia.
   
 8. M

  Mama Lao JF-Expert Member

  #8
  Mar 3, 2009
  Joined: Jan 16, 2007
  Messages: 238
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  ....talk of leadership styles...
  ....2010 mkipiga kura tumia akili yako na sio moyo wako...hapo tumeshashikwaa!
  next time "VOTE WISELY"
   
 9. Kiroroma

  Kiroroma JF-Expert Member

  #9
  Mar 3, 2009
  Joined: Feb 6, 2009
  Messages: 368
  Likes Received: 30
  Trophy Points: 45
  Rais Rahisi............(mtu wa watu).Hapo hatujambo kazi ipo.
   
 10. Zak Malang

  Zak Malang JF-Expert Member

  #10
  Mar 3, 2009
  Joined: Dec 30, 2008
  Messages: 5,410
  Likes Received: 18
  Trophy Points: 0
  Tatizo langu kuhusu ziara ya Rais kule bandarini ni yale aliyoyasema kuhusu wakwepa kodi – kwamba anayo orodha ya wakwepa kodi na kwamba atampatia mkuu wa TRA kuwashughulikia.

  Kwa maoni yangu, hii ni siasa tu, na pengine nathubutu kusema kuwa ni usanii tu, hali inayotawala vita nzima dhidi ya ufisadi. Kuna kelele nyingi za dhamira kuhusu kuwashighulikia mafisadi, lakini results zinakuwa hakuna, au kama zipo ni za ubababishaji tu.

  Rais alitakiwa amwite mkuu wa TRA kimya kimya na kumkabidhi list yake ya hao wakwepa kodi na kumwambia mkuu huyo kwamba anachotarajia ni results toka kwake. Wananchi tungetangaziwa tu hizo results – kwamba “fulani na fulani wako mbaroni na watafikishwa kortini.”

  Mfano mwingine: Miaka michache iliyopita, wakati Magufuli akiwa waziri wa miundombinu, alihutubia mkutano wa wafanuakazi wa Tanroads. Alisema kuwa amegundua ufisadi katika idara hiyo kuhusu ununuzi wa magari – yaani kulikuwapo magari yamenunuliwa kwa bei maradufu ya ile halisi.

  Huo pia ulikuwa usanii – alitaka tu atangazwe katika vyombo vya habari kwamba yuko makini katika vitendo vya ufisadi. Hata hivyo issue iliishia hapo hapo, wananchi hatukuelezwa tena kilichotokea, bila shaka hakuna kilichotokea.

  Kimya kimya Magufuli angeamrisha uchunguzi mkali ufanyike na wahusika kukamatwa na kufikishwa katika vuyombo vya sheria – na hapo ndiyo angetangaza kuwa “fulani na fulani, wamekamatwa katika ufisadi ndani nya Tanroads na tayari wamefikishwa mahakamani.”

  Wananchi tumechoka na kelele za dhamira tu, tunahitaji vitendo na hasa hasa results.
   
 11. Bill

  Bill JF-Expert Member

  #11
  Mar 3, 2009
  Joined: Oct 5, 2007
  Messages: 4,165
  Likes Received: 1,251
  Trophy Points: 280
  Unashangaa Maboss wake ni nani ... Marekani aka bush and Obama
   
 12. Fidel80

  Fidel80 JF-Expert Member

  #12
  Mar 3, 2009
  Joined: May 3, 2008
  Messages: 21,976
  Likes Received: 104
  Trophy Points: 145
  Mi najiuliza hawajamaa wakiamua kupretent wamebadilika kitabia tuseme atawasamehe na hakuna haja ya kuwafanyia marekebisho na kuwahamisha?
  Kweli Mitanzania bado tupo nyuma.
   
 13. Abdulhalim

  Abdulhalim JF-Expert Member

  #13
  Mar 3, 2009
  Joined: Jul 20, 2007
  Messages: 16,472
  Likes Received: 126
  Trophy Points: 160
  Wandugu mtanisamehe kwa kuanzia mbali kidogo,

  Ktk vuguvugu au mchakato wa Kisutu ulipoanza, ktk zile thread za shouting-match, mdau wa kwanza alidai kuwa, siku itakayofuata zamu ya kukalia benchi la Kisutu ni Karamagi, lakini alitokea mdau mwingine na kulonga kuwa that will only happen in your wildest-day-dreams.

  Niliposoma kwenye blogu ya Br. Michuzi, ni kuwa Mh. Rais, tuliyemkabidhi ujemedari mkuu, akiwa na dhima ya kuhakikisha anatumia kila nyenzo aliyonayo kuilinda mali ya sisi waTZ wanyonge, anasema bila haya kuwa anawafahamu watu TISCAN (ya Karamagi et al) wanaofaulisha kodi pale bandarini, ila eti anawapa salamu mabosi wao, kuwa eti wawaachishe kazi!


  Nikijumuisha maneno haya ya kinyonge kabisa wa jemedari wetu mkuu, na nukulu ya hapo juu, NAKUBALIANA NA MANENO YA MKUU FMES KUWA MAFISADI WAMESHINDA RAUNDI HII, TUSUBIRI IJAYO LABDA TUTATOKA.
   
  Last edited by a moderator: Mar 3, 2009
 14. C

  Caroline Danzi JF-Expert Member

  #14
  Mar 3, 2009
  Joined: Dec 19, 2008
  Messages: 3,629
  Likes Received: 56
  Trophy Points: 145
  Baba wa Taifa alikwua anaona mbali sana. Tusimlaumu JK, tujilaumu wenyewe kwa kufanya mizaha sehemu ambazo hazitakiwi.

  Waliocheza fyongo ni sisi wapiga kura kutoa uongozi kwa kuangalia handsomity na siyo unadhifu wala uzoefu. For sure tutazidi kumkumbuka sasa Mzee wetu JKN.
   
 15. Mwana wa Mungu

  Mwana wa Mungu JF-Expert Member

  #15
  Mar 3, 2009
  Joined: Aug 14, 2008
  Messages: 1,007
  Likes Received: 21
  Trophy Points: 135
  kusema ukweli, kikwete yuko serious nusunusu, sio complete. anahitaji mtu mwingine wa kumsaidia ile nafasi, yaani ampokee. kama kuna mtu mwenye uwezo zaidi ccm angegombea mwaka kesho ili nchi hii isonge mbele kwa kasi. kama ccm hampo basi vyama vya upinzani wapo tena wengi sana. tukutane mwakani ehee.
   
 16. bm21

  bm21 JF-Expert Member

  #16
  Mar 3, 2009
  Joined: May 12, 2008
  Messages: 774
  Likes Received: 9
  Trophy Points: 0
  Mkuu tena hapa JK haumizi uchumi wa taifa tu bali hata fikra za wanaJF. Maana tunalazimika kufikiria uvivu wake wa kufikiri baadala ya kuwa na muda wakutosha kushauri serikari. Swala la kubadilika nadhani limeshindikana, maana kadili siku zinavyokenda mambo ndio yanazidi kuharibika. kuna msemo unasema ''Personality stabilise with time'' hivyo tusitegemee jama atabadilika kama hatutambadilisha kwa kupata kichwa kingine chenye fikra mpya
   
 17. Teamo

  Teamo JF-Expert Member

  #17
  Mar 3, 2009
  Joined: Jan 9, 2009
  Messages: 12,286
  Likes Received: 51
  Trophy Points: 145
  HALAFU J.K mjanja!ofcourse ni kitu ambacho wanasiasa wengi watakifanya kama HAWATAJIPANGA!

  Sasa ivi j.k ana tension ya 2010.ndo maana HAELEWEKI ELEWEKI!mambo haya kwamba hakuwah kuyajua SIO KWELI!naona hapa '..tunapakana mafuta kwqa mgongo wa chupa..'
   
 18. M

  Mwikimbi JF-Expert Member

  #18
  Mar 3, 2009
  Joined: Mar 8, 2008
  Messages: 1,745
  Likes Received: 109
  Trophy Points: 160
  Mnanikumbusha 1986s, wakati mwinyi anachukua nchi akasema atatumia mara fagio lachuma, oh!!!,

  baadaye akawa anaongozana na wasaidizi wake kuziba mashimo ya barabara za dsm zile za lami kwa matope, huyuu kila kukicha hili na lile
   
Loading...