Nnangale
JF-Expert Member
- Jul 20, 2013
- 2,664
- 1,374
Maisha bora hayatakuja kwa kukaa na kulaumu kila siku. Jakaya Kikwete hawezi kuleta maisha bora sebuleni kwenu bila ya nyie kujituma na kufanya kazi kwa bidii. Yeye kama kiongozi mkuu wa nchi ameweza kutuhamasisha ili tufanye kazi. Maisha bora hayatakuja kwa kufanya maandamano kila siku. Vijana wengi wanalalamika kwamba hawana kazi ama wanataka kazi za ofisini. Kuna kazi nyingi sana mashambani, tuna ardhi ya kutosha kabisa kufanya kilimo na serikali imetangaza suala la kilimo kwanza kwa maana kwamba serikali iko tayari kuwawezesha vijana katika suala hilo.
Tuache kumlaumu Jakaya Kikwete kwa kila jambo, ni hekima tukubali kuacha tabia ya uvivu na majungu.
kuna dokta mmoja alikuwa mkuu wa mkoa morogoro alikuwa anatoa ushauri kama huu ukuu ukuu wa mkoa ulipoisha hakwenda kulima bali aliuliza jamii alicho mkosea rais badala yakwenda kulima kama alivyokuwa anawashauri wengine