Hivi Rais wenu ana pesa kuliko nyie Watanzania na Tanzania ? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Hivi Rais wenu ana pesa kuliko nyie Watanzania na Tanzania ?

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by Lunyungu, Nov 2, 2007.

 1. Lunyungu

  Lunyungu JF-Expert Member

  #1
  Nov 2, 2007
  Joined: Aug 7, 2006
  Messages: 8,836
  Likes Received: 75
  Trophy Points: 145
  Hili swali leo nimeulizwa na mzungu mmoja tukiwa pale Movenpick tunapata chai . Aliniona nimeshika gazeti moja na akaanza maongezi . Akanieleza jina lake na aksema anatoka US.Akasema aliweza kukutana na ujumbe wa Tanzania wakati JK akiwa US kuhudhuria mkutano wa UN.

  Baada ya swali lake nikamuuliza kwa nini aliuliza maana kama ujuavyo sisi wabongo swali na swali juu si jibu . Akasema amekuja kuangalia mazingira ya kuwekeza lakini anakuta watu ni masikini na anasoma ma scandal kibao wakati US alishuhudia JK anaishi Hotel ya bei mbaya sana ukilinganisha na maisha ya watanzania kwa muda wa wiki 3 akiwa US.

  Nina ncontact za huyu jamaa mkitaka nitawapa na sasa naomba kujua nyie wwatu wa majuu . JK kwa muda wa wiki 3 alijifungua katika Hotel lipi ambalo huyu mzungu anashangaa ? Maana anasema mimi pamoja na pesa zangu siwezi kuishi Hotel ile maana ni ghali .Je rais kwa wiki 3 anawezaje kukaa mle ?

  Mimi nawauliza Mzee alipumzika hotel ipi huko US ?
   
 2. K

  Kalimanzira Senior Member

  #2
  Nov 2, 2007
  Joined: Aug 15, 2007
  Messages: 100
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Ungemweleza tu kwamba maisha kwa afrika na hsa Tanzania, maisha ya viongozi hayahusiani na maisha ya wananchi wa kawaida.Na kuwa umaskini aliouona uansababishwa na hizo anasa alizoziona huko newyork! ..... maana huo ndio ukweli, kinyume chake unataka kutesa nafsi yako tu!
   
 3. Mzee Mwanakijiji

  Mzee Mwanakijiji Platinum Member

  #3
  Nov 2, 2007
  Joined: Mar 10, 2006
  Messages: 31,361
  Likes Received: 6,382
  Trophy Points: 280
  Kalimanzira, that is one of the best quote I have encountered ambayo ndani yake kuna ukweli mzito sana ambao unaweza kupasua kichwa cha mtu akitumia muda kuufikiria. Kuwa, ukiona viongozi wa Afrika wanavyoishi iwe ugenini au nyumbani, haihusiani kabisa na maisha ya watu wao. As a matter of fact we easily postulate that the life of An African leader is not directly linked or reflected by looking at the lives of their people.
   
 4. S

  S. S. Phares JF-Expert Member

  #4
  Nov 2, 2007
  Joined: Nov 27, 2006
  Messages: 2,141
  Likes Received: 9
  Trophy Points: 0
  Mbona FM ES alisema hapa kuwa Muungwana alikaa Hotel ya bei chini kabisa kulinganisha na Mkapa wakati wa utawala wake...yupi anachemsha kati ya huyo Mzungu Muwekezaji na FM ES..??

  Au huyo mzungu anaangalia vigezo ghani kusema rais wetu alitanua sana alipokuwa US?
   
 5. Nyani Ngabu

  Nyani Ngabu Platinum Member

  #5
  Nov 2, 2007
  Joined: May 15, 2006
  Messages: 73,651
  Likes Received: 35,409
  Trophy Points: 280
  But the question that easily comes to mind is ....why? Is it because they wield so much power that no one dares to question them? If so, how can a handful of people have so much power over masses of people like that? How does that happen?
   
 6. Gaijin

  Gaijin JF-Expert Member

  #6
  Nov 2, 2007
  Joined: Aug 21, 2007
  Messages: 11,850
  Likes Received: 57
  Trophy Points: 0
  it might be a cheaper hotel than the one Mkapa used, lakini bado ni ghali sana kwa hali anayoiona kwa watanzania wa kawaida.

  ukiwa kiongozi afrika, it means ni wakati wako wa kuishi kama mfalme, wa kutumia bila kujali sana bili atalipa nani na kwa hali gani, ni wa kati wako wa kujilimbikizia mali.......

  wenyewe wanasema kama hujala wakati ni kiongozi utakula lini?
   
 7. M

  Masatu JF-Expert Member

  #7
  Nov 2, 2007
  Joined: Jan 29, 2007
  Messages: 3,285
  Likes Received: 18
  Trophy Points: 135
  Tuliambiwa na na FMES Kikwete alifikia ktk hotel za kawaida tofauti na alizokuwa anakaa Mkapa wakati wa Rais wake.

  Sasa kwa mantiki hiyo naungana na Yebo*2 kupata ufafanuzi ukweli ni upi?
   
 8. M

  Mwafrika wa Kike JF-Expert Member

  #8
  Nov 2, 2007
  Joined: Jul 5, 2007
  Messages: 5,194
  Likes Received: 12
  Trophy Points: 0
  Yebo yebo,

  hoteli aliyofikia Kikwete na ujumbe wake wa watu 50 na vimada wao bado ni very expensive hata kama haitalinganishwa na zile alizokaa Mkapa.

  Hotel hiyo ni very expensive na kama alitaka cheap hotels zipo tu na wala hakwenda huko. Safari yake mwaka jana ambapo alitembelea states zingine, alifikia one of the most expensive hotels katika hizo states.
   
 9. KadaMpinzani

  KadaMpinzani JF-Expert Member

  #9
  Nov 2, 2007
  Joined: Jan 31, 2007
  Messages: 3,749
  Likes Received: 21
  Trophy Points: 0
  [​IMG]

  LABDA PICHA ZENYEWE NDIO HIZI WALIZOKUWA WANADAI !!
   
 10. M

  Mwafrika wa Kike JF-Expert Member

  #10
  Nov 2, 2007
  Joined: Jul 5, 2007
  Messages: 5,194
  Likes Received: 12
  Trophy Points: 0
  ki-complex kitakumaliza.

  kwi kwi kwi kwi
   
 11. M

  MzalendoHalisi JF-Expert Member

  #11
  Nov 2, 2007
  Joined: Jun 24, 2007
  Messages: 3,868
  Likes Received: 115
  Trophy Points: 160
  What is a cheap Hotel kwa Raisi- NY au Washington?
   
 12. KadaMpinzani

  KadaMpinzani JF-Expert Member

  #12
  Nov 2, 2007
  Joined: Jan 31, 2007
  Messages: 3,749
  Likes Received: 21
  Trophy Points: 0
  [​IMG]
   
 13. M

  Mtanzania JF-Expert Member

  #13
  Nov 2, 2007
  Joined: May 4, 2006
  Messages: 4,818
  Likes Received: 49
  Trophy Points: 145
  Lunyungu,

  Si unajua rais sio sawa na wewe na hawezi kukaa sehemu yeyote maana hata hao wenyeji zake hawawezi kukubali.

  Hata mimi Mtanzania na umaskini wangu, nikiwa safari za kikazi
  siwezi kujibana zaidi maana nikipata madhara mwajiri wangu anaweza kukataa kunilipa. Kuna level inayokubalika lakini sio chini ya hapo.

  Labda tatizo la JK ni ukubwa wa msafara wake lakini sio kukaa hoteli aghali. Huyo Mzungu alitaka rais wetu akakae B&B kwasababu tu TZ ni maskini?
   
 14. Bi. Senti 50

  Bi. Senti 50 JF-Expert Member

  #14
  Nov 2, 2007
  Joined: Apr 17, 2007
  Messages: 291
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 35
  Rais ni Rais wa nchi, na akienda kuishi huko anaishi kama Rais wa Nchi. Kama wanakijiji hawana maji ina maana Rais wao asiwe na maji?

  asante.
   
 15. M

  Mtanzania JF-Expert Member

  #15
  Nov 2, 2007
  Joined: May 4, 2006
  Messages: 4,818
  Likes Received: 49
  Trophy Points: 145
  Lunyungu,

  Hivi wananchi wa jimboni kwako tajiri sana mpaka upate chai Movenpick? Huyo mzungu angepita jimboni kwako au kwenye familia yako, si ajabu angekuuliza swali hilo.

  Mkuu, ungeenda kunywa chai kwa mama Ntilie ili ufanane na Watanzania walio wengi.
   
 16. M

  Mwafrika wa Kike JF-Expert Member

  #16
  Nov 2, 2007
  Joined: Jul 5, 2007
  Messages: 5,194
  Likes Received: 12
  Trophy Points: 0
  Mtanzania,

  yaani Kikwete kutumia pesa za serikali inaweza kulinganishwa na Lunyungu kutumia pesa zake binafsi? au ndio ya the principle of being different!
   
 17. M

  Mwafrika wa Kike JF-Expert Member

  #17
  Nov 2, 2007
  Joined: Jul 5, 2007
  Messages: 5,194
  Likes Received: 12
  Trophy Points: 0
  Kikwete kula nchi Mwaya, na this time ukija NY inabidi ununue suti expensive zaidi maana wachongaji wamezidi mno kukusema!
   
 18. M

  Mfwatiliaji JF-Expert Member

  #18
  Nov 2, 2007
  Joined: Oct 5, 2007
  Messages: 1,325
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 0
  Ulivyozungumzia movenpick nimekumbuka siku moja nilimsindiza rafiki yangu pale royal palm (siku hizo ilikuwa sheraton) kuclear ticket yake, nikamwambia tupate walau soda moja pale ground floor bar, cha ajabu wale wahudumu wakatuchunia..nadhani sababu tulikuwa waswahili. Lakini siku hiyo nilifurahi maana nilimjua na manager wa hotel baada ya kutema cheche kali.
   
 19. Kitila Mkumbo

  Kitila Mkumbo Verified User

  #19
  Nov 2, 2007
  Joined: Feb 25, 2006
  Messages: 3,347
  Likes Received: 78
  Trophy Points: 145
  We are missing the point! The problem is not which hotel the president stays. Hata akikaa hotel cheap namna gani huko US bado itakuwa ghali tu kwa standard zetu. Sasa labda msema Rais akalale nyumbani kwa balozi wetu! The issue hapa is why did he have to spend all the days in a foreign land? Why should he have to travel all that frequently with such a huge delagation like Gaddafi?! More importantly, why should our president be moving around begging from the people who despise us so much instead of sitting down to strategise about solving our never ending problems?

  Yaani kulala Rais lazima alale panapoeleweka, vinginevyo ni utani. Hawezi kabisa kulala maisha yale ya kalimanzila. Hata sisi sasa hivi hata ubalozi wa nyumba 10 hatuna tunajaribu kuhakikisha tunakwenda hotel zenye hadhi fulani. Walio Dar niambieni wangapi kati yenu wenye uwezo wa kushika key board mnakunywa pale ile bar maarufu ya Manzese kwa Mfuga Mbwa? Wote manajaa Rose Garden, why?

  There are certainly bigger questions to ask kuliko hili la Rais alilala wapi, tuache tu uvivu wa kufikiri!
   
 20. M

  Mtanzania JF-Expert Member

  #20
  Nov 2, 2007
  Joined: May 4, 2006
  Messages: 4,818
  Likes Received: 49
  Trophy Points: 145
  Una uhakika gani Lunyungu hapo alikuwa hatumii pesa za serikali? Pesa za walalahoi? Unaweza kuta Lunyungu ni mbunge kwahiyo anatumia pesa tunazomlipa walalahoi.

  Hata kama za kwake kwanini akalipe pesa nyingi Sheraton wakati kuna sehemu nyingi tu ambazo ziko very cheap?

  Point yangu ni kwamba mtu mmoja anachoona aghali kinaweza kuwa bei nafuu kwenye level ya mtu mwingine.

  Hata mlimani watu tulikuwa tunachomewa makuku enzi hizo na kulilia mayai, huku Watanzania wenzetu wanashindwa hata kula, mbona hatukulalamika?
   
Loading...