Hivi Rais wa Tanzania ana uwezo wa kutumia mamlaka yake ya Urais na kutoa agizo tofauti na Katiba ya Tanzania?

Synthesizer

JF-Expert Member
Feb 15, 2010
11,129
18,743
Hadi sasa nashindwa kuelewa kinachoendelea nchini. Mara kadhaa sasa nimeshuhudia katika awamu hii ya tano Raisi Magufuli akitoa maagizo kama Raisi na Amri Jeshi Mkuu, agizo ambalo utakuta linaenda kinyume na Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. Baadhi ya mambo ambayo Raisi Magufuli ameyatolea maagizo kwa mamlaka yake kama raisi ni pamoja na kuzuia mikutano ya siasa na matumizi ya Jeshi la Wananchi Tanzania.

Sasa hapa juzi nimesikia Raisi akitengua maelekezo kuhusiana na wimbo wa taifa na bendera ambayo yalitaka kurekebisha ukiukwaji wa Katiba uliokuwa ukiendelea.

Sasa ninachojiuliza, hivi tuna kipengere sehemu yeyote katika sheria zetu nchini ambacho kinampa Raisi mamlaka ya kutoa agizo, japo kwa muda, linaloweza kuwa linapingana na Katiba, bila kuwapo kwa tangazo la hali ya hatari nchini? Na kama akifanya hivyo, ni kununi gani zinapaswa kutumika ili kumzuia kutumia mamlaka yake ya uraisi kinyume na sheria au Katiba ya nchi?
 
Tunaambiwe "the president may lakin hashulutishwi" kwamaana hiyo suluhu pekee ini katiba mpya itakayoondoa kinga ya madaraka ya raisi.mbaya zaidi tuna rais dicteta.
 
Rais hana uwezo wa kukiuka katiba akifanya hivyo muhimili wa bunge unaweza kumpigia kura ya kutikuwa na imani nae na anaweza kushitakiwa nakufungwa
 
Tunaambiwe "the president may lakin hashulutishwi" kwamaana hiyo suluhu pekee ini katiba mpya itakayoondoa kinga ya madaraka ya raisi.mbaya zaidi tuna rais dicteta.

Mkuu, kama kuna sehemu tunasema "the president may..." kwa namna ya kuvunja katiba, basi kuna tatizo kubwa sana. Labda ndio maana Nyerere alikuwa akisema tatizo la Katiba ya Tanzania ni kwamba mkipata raisi dikteta mtapata shida sana.
 
Raisi hana uwezo wa kukiuka katiba akifanya hivyo muhimili wa bunge unaweza kumpigia kura ya kutikuwa na imani nae na anaweza kushitakiwa nakufungwa
Bunge linaweza kutoa kibali cha raisi kushitakiwa na hata akafungwa? Nakumbuka ilisemwa kwamba raisi hawezi kushitakiwa akiwa madarakani au akiwa amemaliza muda wake. Ila najua anaweza kupigiwa kura ya kutokuwa na imani nae. Ila katika mazingira ya sasa ya kuwa na wabunge wenye kuitikia "ndiyoooooo" bila kutumia akili sidhani kama hilo linawezekana.
 
Raisi hana uwezo wa kukiuka katiba akifanya hivyo muhimili wa bunge unaweza kumpigia kura ya kutikuwa na imani nae na anaweza kushitakiwa nakufungwa
Uwezo wa kukiuka katiba, anapewa na kifungu kipi cha katiba? AU ANAPEWA NA WOGA WA ANAOWAONGOZA?
 
Aliapa akiwa na Biblia mkononi kuwa ataitunza, kuiheshimu na kuilinda katiba.
Hili alishasahau kitambo.
 
Back
Top Bottom