Synthesizer
JF-Expert Member
- Feb 15, 2010
- 11,135
- 18,746
Hadi sasa nashindwa kuelewa kinachoendelea nchini. Mara kadhaa sasa nimeshuhudia katika awamu hii ya tano Raisi Magufuli akitoa maagizo kama Raisi na Amri Jeshi Mkuu, agizo ambalo utakuta linaenda kinyume na Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. Baadhi ya mambo ambayo Raisi Magufuli ameyatolea maagizo kwa mamlaka yake kama raisi ni pamoja na kuzuia mikutano ya siasa na matumizi ya Jeshi la Wananchi Tanzania.
Sasa hapa juzi nimesikia Raisi akitengua maelekezo kuhusiana na wimbo wa taifa na bendera ambayo yalitaka kurekebisha ukiukwaji wa Katiba uliokuwa ukiendelea.
Sasa ninachojiuliza, hivi tuna kipengere sehemu yeyote katika sheria zetu nchini ambacho kinampa Raisi mamlaka ya kutoa agizo, japo kwa muda, linaloweza kuwa linapingana na Katiba, bila kuwapo kwa tangazo la hali ya hatari nchini? Na kama akifanya hivyo, ni kununi gani zinapaswa kutumika ili kumzuia kutumia mamlaka yake ya uraisi kinyume na sheria au Katiba ya nchi?