Hivi Rais Samia yuko serious kweli katika kuunda Kamati Maalumu ya Corona? Mbona haoneshi mfano wa kutilia maanani ugonjwa huu?

Hiyo Kamati ishauri yote, lkn siyo masuala ya quarantine, yameshapitwa na wakati kwasasa.
Kikubwa tutakachodaiwa ni kutoa figures za waathirika as of now.
Lengo liwe tu kuwa at per na Jumuia ya Kimataifa tu.
Ile pesa ya CDC na WHO tutalamba tutaidirect kwenye kuadvance facilities zetu za Health.
Kwisha.
 
Kamati ni muhimu sana Mkuu... Tanzania is not an island. Lazima turudi tushirikiane na mataifa mengine. Kama kuna tahadhari za WHO tuzifuate kikamilifu...
Wengine ishaanza kuwa ngumu kusafiri kwenda nchi za nje kikazi... Unaambiwa huna Covid vaccine usijiangaishe...
Hivi ushawahi kukutana na madhila ya chanjo ya Yellow fever? Basi hii ya Covid ishaanza kuwa official.
Kamati ni muhimu sana... Nategemee itatoa muongozo wa Kisayansi zaidi na tutarejea duniani kuishi na kujamiiana na wengine...
We are part of a bigger world! Citizens of the world

Hili swali la kutaka traveler awe na proof of COVID vaccination litasababisha unnecessary inconvenience. Tafiti zenyewe zinaonesha COVID vaccine inakupa protection ya miezi sita tu. Sasa kama nimechanjwa leo kisha nikawa na safari mwaka ujao, proof of vaccination nitakayoitoa mwaka kesho ina relevance gani, kama protection COVID vaccine imeshaisha kitambo?
 
Rais wetu huyu mpya majuzi katangaza kuwa ataunda sijui kamati ya Corona!

Bado sijaelewa hasa lengo na madhumuni ya hiyo kamati yatakuwa ni yepi.

Sasa ni zaidi ya mwaka na ushee tokea dunia ikumbwe na hili janga.

Kwa jinsi mwelekeo wa hali unavyoonekana, janga hili ni kama vile linaelekea elekea ukingoni sasa hususan baada ya upatikanaji wa ‘chanjo’.

Licha ya hivyo, nadhani kwa sasa nitakuwa sawa nikisema kuwa ‘tunajua’ kiasi cha kutosha kuhusu ugonjwa huo.

Sasa, kama kweli Rais Samia ana nia ya dhati ya kuunda kamati ya corona, kwa nini mpaka sasa walau haonyeshi mfano kuwa kweli anautilia maanani ugonjwa huo kwa kuzingatia hata zile tahadhari zilizo za msingi kama kuvaa barakoa na kukaa ama kusimama mbalimbali na watu?

Leo kampokea waziri Amina Mohammed kutoka Kenya aliyekuwa katumwa na Rais Kenyatta.

Bi. Amina kaingia ikulu ya Dar akiwa amevaa barakoa. Samia yeye hakuwa kavaa.

Waziri Mulamula naye mwanzoni alionekana kavaa.

Baadaye wote walipokuwa wanaongea na waandishi wa habari, wote wakaonekana hawajazivaa.

Hivi ni kweli Rais Samia yupo serious au alikuwa anaongea tu siku ile ili kuridhisha baadhi ya watu kwa maneno tu lakini hakuwa na nia ya dhati kuonyesha kimatendo kuwa anamaanisha anachokisema?

Yeye kama raia namba moja si ndo anapaswa kuonyesha mfano wa kimatendo, au nakosea?

Au Watanzania walio wengi hawana muda na matendo bali wanapenda tu kusikia maneno yawapendezayo masikioni mwao?

Wee unataka atoe mipovu kama yule Jamaa yenu ndio ujue yuko serious?

Sent from my Nokia 8.1 using JamiiForums mobile app
 
Kwendeni zenu na korona yenu.mwenda zake Ali tackle vizuri issue ya korona.korona ni propaganda tu.Siku huko kwenu ika kwetu ninapoishi sioni watu wakifa hovyooo maisha yanaendelea kama kawa.korona korona kila Siku wimbo huu tu.nyie na wazungu wenu kwendeni huko.korona kwenu na wazungu wenu huko....waonee mfyuuuushxxxy
 
Ile kauli ilikuwa kuwafurahisha tu wanaharakati wa kovidi, ila sitegemei chenjezi yoyote.......kazi kwenu mnaoshangilia mapema
 
"Urithi"

JPM alisema hatuna corona. "Si vema" kubadilisha uelekeo bila kupata ushauri wa kitaalamu kama ugonjwa upo/umerudi (kinyume na alivyosema JPM).
 
11 Reactions
Reply
Back
Top Bottom