Hivi Rais Samia angeamua kuanzisha uchunguzi wa tukio la Lissu kupigwa risasi, sukuma gang wangekuwa na hali gani? Shukurani kamsitiri

Hawa jamaa nawashangaa sana kumlaumu Rais Samia kuwa anafanya mambo kinyume na Mwendazake na kwamba anajaribu kuharibu wanachokiita Legacy ya Mwendazake!

Binafsi najiuliza leo hii Mama angemuru uchunguzi huru wa tukio la Lissu kupigwa risasi, hali ya hawa watu itakuwaje? Je, si wangelala na viatu mitandaoni au wangetembea wamevaa boxer vichwani?

Mimi nadhani wamshukuru sana huyu Mama kumsitiri Mwendazake katika hili vinginevyo wangetamani ardhi ipasuke waingie huko na wapotee kabisa katika uso wa hii dunia.

Tuacheni sisi ndio tumlaumu kwa uovu anaoutuendea/anaoubariki kama huu wa kumtesa Kamanda wa Anga lakini sio nyie SUKUMA GANG mnaofichiwa uovu wenu na wa Mwendazake.

Narudiia,hampaswi kumlaumu huyu Mama kwakuwa anawabeba pakubwa mno kwani Mwendazake amebariki uovu mwingi sana alipokuwa ofisini.

Tuacheni sisi tumlaumu lakini kamwe sio nyie.

La vifaranga cha mtoto.
Uchunguzi uanze tu
 
Mimi sikuwahi kumkubali mwendazake hata siku moja na namshukuru sana Mungu kutuondolea ibilisi moja muovu. Kutokana na kifo chake, wengi wetu tulipona.

Hata hivyo nadhani katika swali lako umekosea. Ungeuliza hivi...hivi Rais Samia angeamua kuanzisha uchunguzi wa tukio la Lissu kupigwa risasi, yeye Rais Samia angekuwa na hali gani?

Naomba usisahau wakati huo alikuwa ni makamu wa mwendazake!

maKu
 
..kuna orodha ilitoka ya wananchi wa Mkiru ambao inasemekana walikamatwa na haijulikana walipo mpaka leo.

..pia kuna mama mmoja alihojiwa kwenye Tv ni wa maeneo ya Mkiru mumewe aliuwawa na yeye alijeruhiwa na watu waliofika nyumbani kwake wakitumia gari aina ya NOAH.

..sasa utakumbuka wengi wa watu waliopata misukosuko kipindi kile walikuwa wakitaja kuwa waliowashughulikia walikuwa na gari ya NOAH.

..tukio la Lissu lililenga kumnyamazisha na kutuma ujumbe kwa wanaharakati na wakosoaji wengine wa Magufuli.

..Kwamba walitumia marisasi mengi huenda ni kwasababu alikuwa ndani ya gari. Walenga shabaha walikuwa hawajui kama risasi zinampata au la.

..Hakuna anayejua kama Lissu angeteremka toka ktk gari walenga shabaha wangemtwanga risasi ngapi.

..Lingine ni kwamba Lissu hakukamatwa. Huenda angekamatwa na akafia mikononi mwao naye angetiwa kwenye kiroba, au angetupwa porini aliwe na fisi.

..Mwisho, Magufuli ananaswa na mambo yafuatayo. Mosi, walinzi wa serikali kuondolewa. Pili, serikali kutomsaidia Lissu. Tatu, serikali kutokufanya uchunguzi.

Maswali ya jamaa ni mazito ila unayajibu ki wepesi sana, mimi pia naungana nae kuamini Magufuli hakua mjinga kiasi hiko kuamuru Lissu auliwe tena kipindi ambacho umaarufu wa the former kwa wananchi ulikua juu sana hasa baada ya ku deal na ishu ya makinikia katika namna ambayo wananchi wengi waliona ni sahihi na ya kijasiri sana.

Na sasa tunaelekea miezi 18 bila mzee na wote tunajua huyu mama hawezi kusita kufanya kitu chochote kitakachoshusha heshima ya JPM kwa wananchi, mbona hajaruhusu ufanyike uchunguzi huru kama alivyokurupuka kuchunguza ile miamala ya BOT?

Mimi katika vitu naogopa ni kuhukumu kitu nisichokua na uhakika nacho, kuna siku mambo yatajulikana, tutatafuta hizi comments tuzifute na kuzidelete kabisa!
 
Hoja zako zinafikirisha sana na hazitakiwi kupuuzwa hata kidogo.

.Nimelazimika kumlaumu au kumnyooshea kidole Magufuli kwa sababu zifuatazo.

1. Kuondolewa kwa WALINZI wa serikali eneo aliloshambuliwa Tundu Lissu.

2. Serikali kukataa kutoa msaada na kumhudumia Lissu baada ya kushambuliwa.

3. Serikali kutokufanya uchunguzi wa tukio hilo, na kutoa visingizio visivyo na mantiki.

4. Serikali kukataa kuita wachunguzi toka nje ambao wanaaminika na pande zote.

5. Serikali kumfukuza Lissu bungeni kwa madai kuwa haujulikani alipo.

6. Viongozi wa serikali na Ccm kutoa kauli za kumkashifu Lissu hata alipokuwa ktk mazingira ya ugonjwa hospitali.

Ikiwa ITATHIBITIKA pasipo na shaka kwamba waliojaribu kumuua Lissu sio watu wa serikali nitakuwa tayari kuomba RADHI ktk jukwaa hili.
 
Hawa jamaa nawashangaa sana kumlaumu Rais Samia kuwa anafanya mambo kinyume na Mwendazake na kwamba anajaribu kuharibu wanachokiita Legacy ya Mwendazake!

Binafsi najiuliza leo hii Mama angemuru uchunguzi huru wa tukio la Lissu kupigwa risasi, hali ya hawa watu itakuwaje? Je, si wangelala na viatu vitandani au wangetembea wamevaa boxer vichwani?

Mimi nadhani wamshukuru sana huyu Mama kumsitiri Mwendazake katika hili vinginevyo wangetamani ardhi ipasuke waingie huko na wapotee kabisa katika uso wa hii dunia.

Tuacheni sisi ndio tumlaumu kwa uovu anaoutenda /anaoubariki kama huu wa kumtesa Kamanda wa Anga lakini sio nyie SUKUMA GANG mnaofichiwa uovu wenu na wa Mwendazake.

Narudiia, hampaswi kumlaumu huyu Mama kwakuwa anawabeba pakubwa mno kwani Mwendazake amebariki uovu mwingi sana alipokuwa ofisini.

Tuacheni sisi tumlaumu lakini kamwe sio nyie.

La vifaranga cha mtoto.
Hakuna haja ya uchunguzi. Kila kitu kinajulikana
 
..Nilichokuwa najaribu kuonyesha ni kwamba watu wasiojulikana hawakuwa na namna moja ya kuua watu.

..kwamba ukiwa mwanaharakati basi utauwawa kama Lissu, na ukiwa mtu wa Mkiru utawekwa kwenye kiroba.

..Labda nikuulize na wewe hao jamaa waliokuwa kwenye NOAH kwanini wamuue jamaa mbele ya mke na kitoto kichanga? Kwanini hawakumuua " kistaarabu " kwa kumhifadhi kwenye kiroba cha thamani?
Mimi sijui hao waliyokuwa wanauliwa ni akina nani na walikuwa wanauliwa kwa sababu zipi na ndio maana nikakuuliza wewe mwenye kuwajua kwamba hata yule mume wa yule mama alionekana kwenye tv naye alikuwa mkosoaji wa Magufuli ndio maana aliuliwa?
Binafsi siwajui hao waliyokuwa wanauliwa wala sababu za kuuliwa kwao hivyo siwezi kuwa na jibu la swali uliloniuliza, matukio ya uhalifu yapo na watu wanauwana kwa sababu mbalimbali kwa aina tofautofauti.
 
Hoja zako zinafikirisha sana na hazitakiwi kupuuzwa hata kidogo.

.Nimelazimika kumlaumu au kumnyooshea kidole Magufuli kwa sababu zifuatazo.

1. Kuondolewa kwa WALINZI wa serikali eneo aliloshambuliwa Tundu Lissu.

2. Serikali kukataa kutoa msaada na kumhudumia Lissu baada ya kushambuliwa.

3. Serikali kutokufanya uchunguzi wa tukio hilo, na kutoa visingizio visivyo na mantiki.

4. Serikali kukataa kuita wachunguzi toka nje ambao wanaaminika na pande zote.

5. Serikali kumfukuza Lissu bungeni kwa madai kuwa haujulikani alipo.

6. Viongozi wa serikali na Ccm kutoa kauli za kumkashifu Lissu hata alipokuwa ktk mazingira ya ugonjwa hospitali.

Ikiwa ITATHIBITIKA pasipo na shaka kwamba waliojaribu kumuua Lissu sio watu wa serikali nitakuwa tayari kuomba RADHI ktk jukwaa hili.
Kwamba serikali kukataa kumuhudumia Lissu baada ya kushambuliwa ni moja ya sababu ya kwamba serikali ndio iliyohusika na shambulizi la Lissu?
 
..inaonyesha nia mbaya ya serikali / Magufuli dhidi ya Tundu Lissu.

..baada ya Lissu kunusurika pale Dodoma wakaona bora afe kwa kukosa matibabu sahihi ya kitaalam.

..Walitegemea Lissu atashindwa kugharamia matibabu. Matokeo yake wasamaria wema wakaingilia kati.
 
Dhana ni nyingi sana.
 
well said
Lissu asiangalie mbali. Uchunguzi wa tukio unaanzia na motive. Magu alikuwa hana motive ya kumpiga risasi Tundu Lissu. MAGU alikuwa ni Mkuu wa majestic na ni Rais, asingepoteza risasi 16 kama munavyodai Kwa Lissu. `Lissu asiangalie mbali wakati chama chake kina Gaidi anayeitwa Mbowe. Huyu ndiye mwenye sababu ya kuweza kumpiga risasi wakigombania uongozi wa chama chawo. Magu alikuwa busy kuisafisha Tanzania iliyokuwa ikinuka rushwa na wizi na kuokowa mali za Watanzani. Mmoja wa wezi akiwa GAIDI MBOWE. Mwacheni Magu alale salama na Tundu Lissu apambane na maisha yake ya ukimbizi.
 
Dhana ni nyingi sana.
Musisahau ni madakitari wa kitanzania ndiyo walio okowa maisha ya Lissu. Hakuna mtu angefaidika Lissu kufa zaidi ya Mbowe ambaye walipingana kwenye chama chawo Kwa matumizi mabaya ya fedha. Kila kukicha Magufuli mtu ambaye hawezi kuwajibu. Pambaneni na maisha yenu mpaka na nyinyi siku yenu ya kufa ikifika. Kila binadamu ni mpita njia hapa duniani. Ndiyo Hayati Magufuli hatunaye tena, but he was the best president for Tanzania and we miss him a lot.
 
Mimi sijui hao waliyokuwa wanauliwa ni akina nani na walikuwa wanauliwa kwa sababu zipi na ndio maana nikakuuliza wewe mwenye kuwajua kwamba hata yule mume wa yule mama alionekana kwenye tv naye alikuwa mkosoaji wa Magufuli ndio maana aliuliwa?
Binafsi siwajui hao waliyokuwa wanauliwa wala sababu za kuuliwa kwao hivyo siwezi kuwa na jibu la swali uliloniuliza, matukio ya uhalifu yapo na watu wanauwana kwa sababu mbalimbali kwa aina tofautofauti.
Yote Tisa kumi nenda urudi.
Kila kitu ilipangwa!!
Hebu muulizeni Cyprian Musiba huenda Naye mojawapo wanaolijua! Alikuwa anajiamini sana sana! Je Leo hii yuko wapi Musiba wa Musiba domokayah!! Hovyo!!
 
Hoja zako zinafikirisha sana na hazitakiwi kupuuzwa hata kidogo.

.Nimelazimika kumlaumu au kumnyooshea kidole Magufuli kwa sababu zifuatazo.

1. Kuondolewa kwa WALINZI wa serikali eneo aliloshambuliwa Tundu Lissu.

2. Serikali kukataa kutoa msaada na kumhudumia Lissu baada ya kushambuliwa.

3. Serikali kutokufanya uchunguzi wa tukio hilo, na kutoa visingizio visivyo na mantiki.

4. Serikali kukataa kuita wachunguzi toka nje ambao wanaaminika na pande zote.

5. Serikali kumfukuza Lissu bungeni kwa madai kuwa haujulikani alipo.

6. Viongozi wa serikali na Ccm kutoa kauli za kumkashifu Lissu hata alipokuwa ktk mazingira ya ugonjwa hospitali.

Ikiwa ITATHIBITIKA pasipo na shaka kwamba waliojaribu kumuua Lissu sio watu wa serikali nitakuwa tayari kuomba RADHI ktk jukwaa hili.

Leo mkuu inaenda miezi 19 tokea huyu mzee ameondoka, aliekua spika wakati huo kwa sasa hayupo tena, Kipili.mba hayupo, Si. rro hayupo, aliekua RPC Dom hayupo, Ma.konda hayupo!! Huo uchunguzi kwanini haufanyiki? Nani analindwa kwa sasa?

Mimi bado naamini mzee asingeweza kamwe ku order kifanyike kitu cha kipumbavu namna hiyo tena kwa njia ile.

Ila pia sikulaumu, walau wewe mtu akifuatilia nyuzi zako unaonekana hukupenda wala hukukubali chochote alichokua anafanya huyu mzee way before hata hajawa rais, lakini naendelea kukuomba usimtupie mawe walau kwa hili kama hauna uhakika.
 
..yeye mwenyewe ndio alitengeneza mazingira ya kutupiwa lawama.
 
Back
Top Bottom