Hivi Rais Samia anavalishwa kweli Majoho ya Kimila au anafanyiwa tu Ushirikina uliochangamka kutoka Mwanza na Dodoma?

MINOCYCLINE

JF-Expert Member
Apr 2, 2015
8,011
16,748
Endeleeni tu kutufanya Watanzania wote ni hamnazo ( tuna Akili za Kipa Katoka ) hivyo mtatuzuga kwa kila namna wakati tuliobobea kwa Mambo hayo ( japo Juzi tulizidiwa na wa Yanga SC ) tumeshajua nini Kinaendelea.

Naona kabla hajaiacha Ardhi ya Tanzania kwenda kwa Joe Biden Wasukuma kupitia Zuga ya Joho la Kitemi walimfanyia Mambo na amerudi Wagogo nao wamemaliza Kazi kwa Kukamilisha Utamaduni wa Sayansi ya Mwafrika kwa Zuga ile ile ya Joho la Kitemi.

Mwisho nawaombeni Msaada wenu wa Kuelimishwa Kimantiki Uhusiano wa Rais kupewa Heshima ya Kimila za Makabila na Kuitwa Mtemi dhidi ya Maendeleo ayatakayo Mtanzania hasa katika zama hizi za Sayansi na Teknolojia huku nchi yetu ya Tanzania ikiwa imechelewa mno Kimaendeleo na Wananchi wanalia Ukata ( hali ngumu ya Kimaisha ) kila Uchao tu.

Na Sisi akina Mightier ambao ni Wapemba Kikabila tunataka tumvalishe Joho na tumpe Jina la Kitemi kama ambavyo ameshapewa na Wasukuma na Wagogo na tafadhali tunaomba ratiba yake isimbane sana Mheshimiwa Rais ( Bi. Hingaya ) ili Watu wa Unguja na Pemba nao Wamfanyie Mila Ushirikina waliouzoea na hata Kuubobea pia.
 
Jipendekeze ili upendekezwe, subiri wanataaluma nao wakianza kujitowa akili waanze kummininia Honoraly PhD.

Hii ni nchi ya mipango inachotakiwa fungia akili zako kabatini cheza midundo kama wanayocheza wao.
 
Back
Top Bottom