Uchaguzi 2020 Hivi Rais Magufuli kuwaahidi nafasi za uteuzi akina Andrew Chenge, siyo kutonesha kidonda kwa mamilioni ya vijana wasiokuwa na Ajira?

Mystery

JF-Expert Member
Mar 8, 2012
15,478
30,141
Tulimsikia alipokuwa kwenye mkutano wa kampeni, huko Bariadi akimuahidi Mzee Andrew Chenge, ambaye alishinda kura za maoni jimboni kwake, kuwa atampa nafasi "nzuri" ya uteuzi, miongoni ya nafasi zake nyingi za uteuzi, kwa sharti tu la kumuunga mkono mgombea "wao" wa vikao vya juu vya Central Committee!

Aliamua kumuahidi nafasi hiyo ya uteuzi, kama afanyavyo Mwalimu anapoamua kumzawadia pipi, mtoto wa shule ya chekechea!

Alifanya vivyo hivyo alipofika Shinyanga Mjini, ambapo alimuahidi Stephen Masele, nafasi ya uteuzi, kwa kuwa amegundua kuwa Jimbo hilo, kuna hatari kubwa sana, ya kulipoteza na kwenda upinzani, baada ya vikao vya juu vya chama cha CCM "kupindua" maamuzi ya wajumbe, kwa kumteua Petrobas Katambi, ambaye aliachwa mbali sana, katika kura hizo za maoni.

Wananchi wamekuwa wakijiuliza, ikiwa Rais Magufuli anaamini kuwa ana nafasi nyingi za uteuzi, ni kwanini asitumie nafasi hizo, kumteua "kipenzi" chake Katambi?

Vivyo vivyo alipofika Biharamulo, akamuahidi Anna Tibaijuka, ambaye alitangaza mwenyewe kuwa kutokana na umri wake kuwa mkubwa, anastaafu siasa, na kuamua kuanza kula pensheni yake.

Lakini cha ajabu Rais Magufuli akaamua "kumlazimisha" huyo mama wa "vijisenti vya mboga" kuwa eti bado a anamuhitaji, kwa hiyo ataendelea kumtumia kwenye nafasi nyingine.

Kwanza nimweleze Rais Magufuli kuwa hivi sasa yeye ni mgombea, kama walivyo wagombea wengine, kwa hiyo siyo vyema kuamua kuahidi kutoa vyeo wakati akijua yupo kwenye kinyang'anyiro cha Uchaguzi, ambapo anaweza kushinda, lakini vile vile wananchi wanaweza wasimpe kura za kutosha na hivyo anaweza kung'olewa kwenye nafasi hiyo ya Urais, na asiwe Rais wa awamu ya sita na atakuwa Rais Mstaafu.

Hivi nimuulize Rais Magufuli, hivi akishindwa kwenye Uchaguzi huu wa mwaka huu, hivyo vyeo anavyowaahidi hao "wakereketwa" wa chama chake, atawazawadia akiwa Chato kwake, akiwa Rais Mstaafu?

Kwa vile huu ni Uchaguzi, kuna kushinda na kushindwa, iweje yeye akiwa mgombea kama walivyo wagombea wengine, akina Tundu Lissu, ajihakikishie uhakika wa asilimia 100, wa kushinda Uchaguzi huu?

Au yeye Rais Magufuli anaamini kuwa ni lazima atashinda, hata kama kura hazitatosha, kwa kuwa Tume ya Uchaguzi itakayotangaza matokeo hayo ni "yake" aliyoiteua?

Vile vile kuna hoja nyingine kubwa, kama yeye Rais Magufuli anafahamu kuwa idadi ya vijana wanaomaliza vyuo vikuu na kupata degree zao ni kwa maelfu, ambao hawana kazi, iweje sasa, awaahidi nafasi za kuteuliwa hao "wazee" waliostaafu na kuanza kula pensheni zao, wakati akiwaacha "solemba" vijana hao, ambao kutwa kucha wanazunguka na CV zao bila mafanikio yoyote?

Hivi unawezaje kumhakikishia nafasi ya uteuzi Mzee Andrew Chenge, ambaye amekuwa akifanya kazi, tokea enzi za utawala wa awamu ya kwanza ya Mwalimu Nyerere, wakati kuna vijana wengi kwa maelfu."wakisota" wakiwa hawana ajira zozote?

Hivi hii hali ya Rais Magufuli, kuahidi kutoa nafasi ya kuwateua hao makada wa CCM, kama siyo mazingira ya utoaji rushwa wakati wa uchaguzi, tuiite nini?
 
Kuna shida kubwa kwenye kampeni zake...hili la kuahidi vyeo kwa watu waliovimbiwa ukwasi na ambao umri umesonga ni kasoro kubwa sana
Yaani huwa najaribu kuwaza, hivi huyu Magufuli anaelewa kweli kuwa yupo katika kampeni?

Utawezaje kuwaahidi vyeo watu, wakati huelewi kama utashinda uchaguzi huo au laa?

Kwanza huo mchakamchaka, anaoendeshwa na Lissu, siyo wa kawaida!

Mathalani tuchukulie, ameshindwa kwenye uchaguzi huu, hivi hivyo vyeo anavyowaahidi kina Chenge, atawapa akina Chenge, atakapokuwa Chato, akiwa Rais mstaafu?

Hii ni sawasawa na ule msemo wa wahenga, unaosema USIMTUKANE MAMBA KABLA HUJAVUKA MTO
 
Yaani huwa najaribu kuweza, hivi huyu Magufuli anaelewa kweli kuwa yupo katika kampeni?

Utawezaje kuwaahidi vyeo watu, wakati huelewi kama utashinda uchaguzi huo au laa?

Kwanza huo mchakamchaka, anaoendeshwa na Lissu, siyo wa kawaida!

Hii ni sawasawa na ule msemo wa wahenga, unaosema USIMTUKANE MAMBA KABLA HUJAVUKA MTO
Magufuli ametudharau sisi Raia na wapiga kura. Anaelewa fika kuwa sisi ndiyo tumempa ajira na sasa anatunisha msuli wakati maombi yake ya kuongeza mkataba yako mezani na sisi ndiyo waamuzi.
 
Katambi amemuaminisha Jiwe kuwa Tundu Lissu ni level yake na anauwezo wa kumpa makavu hadharani. Kwa muda huu Jiwe Akim pata mtu mwenye uwezo huo anaweza kulabidhiwa hata kukabidhiwa Bombardier iwe mali yake yeye mkewe na watoto wake.
Watu kama hao akina Katambi, ndiyo wanaompotosha huyo Magufuli.

Hivi huyo Katambi anawezaje kujilinganisha na huyu shujaa wa kimataifa, Tundu Lissu?
 
Tutamwongezea kipindi kingine Cha urais "atake asitake": Ndugai.
Hivi huyo Ndugai naye alikuwa anaota ndoto za mchana?

Hivi anajua kuwa muswada kupita Bungeni, ni lazima uungwe mkono na wabunge wasiopungua theluthi 2?

Hivi mchamkamchaka anowaburuza nao huyo Tundu Lissu, hivi hiyo theluthi 2 ya wabunge wataipata wapi?
 
Hivi huyo Ndugai naye alikuwa anaota ndoto za mchana?

Hivi anajua kuwa muswada kupita Bungeni, ni lazima uungwe mkono na wabunge wasiopungua theluthi 2?

Hivi mchamkamchaka anowaburuza nao huyo Tundu Lissu, hivi hiyo theluthi 2 ya wabunge wataipata wapi?
Si wameshapata wabunge wa kupita bila kupingwa. Hata Majaliwa pia ni wa kupita bila kupingwa. Hakika CCM ni ukoo wa panya.
 
Si ndio ahadi za wagombea za watatufanyia nini tukiwapa uongozi? Na baada ya miaka mitano tutawauliza kama wametimiza ahadi zao? Ndio ujue ahadi zozote zinazotolewa ni HONGO takatifu ili tupate mchecheto tuwachague. Hongo mbaya haiahidiwi, inatolewa papo kwa papo unapoitoa kama mgombea😂😂
 
Tulimsikia alipokuwa kwenye mkutano wa kampeni, huko Bariadi akimuahidi Mzee Andrew Chenge, ambaye alishinda kura za maoni jimboni kwake, kuwa atampa nafasi "nzuri" ya uteuzi, miongoni ya nafasi zake nyingi za uteuzi!
Kwa akili yako unaweza kutoka chuo tu ukateuliwa kuwa balozi au katibu mkuu nishati na madini?
vijana someni lakini msitegemee kuajiriwa na serikali
 
Watu kama hao akina Katambi, ndiyo wanaompotosha huyo Magufuli...........

Hivi huyo Katambi anawezaje kujilinganisha na huyu shujaa wa kimataifa, Tundu Lissu?
Katambi kasema Tundu Lissu ni saizi Yake Kama anabisha waweke mdahalo aone atakavyo muaibisha. Pia katambi kasema mtu Kama Salum Mwalimu hafai hata kuwa balozi wa nyumba Kumi.
 
Back
Top Bottom