Mystery
JF-Expert Member
- Mar 8, 2012
- 15,479
- 30,144
Tumemsikia wenyewe kwa masikio yetu wenyewe, Rais Magufuli katika shughuli ya kufunga mafinzo ya Polisi Kurasini, akiwaambia Polisi kuwa yeye anawaruhusu kuua majambazi na Polisi hao hawapaswi kukamatwa na kupelekwa mahakamani kujibu tuhuma hizo!
Nimeshangazwa sana na kauli hiyo ya Rais ya "kuruhusu" askari wetu kuua na wasipelekwe mahakamani, kwa kuwa nijuavyo kwa mujibu wa Katiba ya nchi, ni mhimili wa mahakama pekee ndiyo unaoweza kuthibitisha tuhuma za mwananchi yeyote na kutoa adhabu, ambayo itakuwa kwa mujibu wa "penal code" kwa mtuhumiwa huyo iwapo itathibitika kuwa yeye ni jambazi
Hivi Rais Magufuli anapowapa kiburi cha aina hii Polisi, anategemea hali itakuwaje nchini??
Natabiri kuwa raia wema wengi watauliwa, kwa "kisingizio" kuwa wao ni majambazi!
Hivi Rais Magufuli anaweza kutwambia Jeshi letu la Polisi lina "credibility" gani hadi kuaminiwa kuua na wasiulizwe chochote??
Hivi kwa Jeshi hili la Polisi, ambalo kuna watanzania wenzetu wengi wamepotea katika mazingira ya kutatanisha na hadi Leo hatujui waliko na Jeshi letu la Polisi lipo na linadai linaendelea na uchunguzi
Jeshi letu la Polisi limeshindwa kutuambia yuko wapi Ben.Saanane, ambaye tokea kupotea kwake ni zaidi ya miaka 2 sasa
Jeshi letu la Polisi limeshindwa kutuambia yuko wapi, Azory Gwanda, ambaye tokea kupotea kwake ni zaidi ya mwaka mmoja sasa
Jeshi letu la Polisi limeshindwa kumkamata hata mtuhiwa mmoja, kati ya wale waliojaribu kumwua kwa kumpiga risasi Mbunge wa Singida Madhariki, Mheshimiwa Tundu Lissu, zaidi ya mwaka mmoja tokea tukio hilo litokee
Vile vile nimkumbishe tu kidogo Rais Magufuli, kuhusu principle kubwa sana ya sheria inayosema kuwa A MAN CAN NOT BE A JUDGE IN HIS OWN CASE
Kwa kuwaruhusu Polisi waue kwa "kisingizio" cha kuwamaliza majambazi, maana yake ni kuwa keshawaruhisu mapolisi wawe ni mahakimu katika kesi imayowakabili wao wenyewe!
Hivi atajuaje kama Polisi ameua jambazi au amemwua raia mwema asiye na hatia kwa sababu zake binafsi??
Mungu ibariki Tanzania

- Ni muhimu kila mhimili wa dola ufanye kazi zake kwa mujibu wa Katiba ya nchi unavyoelekeza
Mungu ibariki Tanzania