Uchaguzi 2020 Hivi Rais Magufuli kuamua kutoa ahadi ya kutuongezea mishahara wafanyakazi wa nchi hii wakati huu wa kampeni, haoni kuwa ndiyo anaharibu zaidi?

Mystery

JF-Expert Member
Mar 8, 2012
14,360
2,000
Wananchi tumemuona ndani ya hii miaka hii 5 ya utawala wake kuwa ni mtawala ambaye hawasikilizi wananchi wake wanataka nini na analoamua yeye ndiyo huwa.

Tujikumbushe maneno ambayo amewahi kuyatamka katika utawala wake wa kipindi hiki cha miaka 5.

Ati sisi wananchi hatuna uwezo wa kumpangia la kufanya, kwa kuwa ni yeye mwenyewe ndiye aliyeamua kwenda kuchukua fomu ya Urais huko Dodoma, miaka 5 iliyopita, mwaka ule wa 2015.

Kwa kuweza kutujibu jeuri, sidhani kuwa yeye Magufuli alikuwa anadhani kuwa mwaka wa uchaguzi 2020 unaweza kufika kweli.

Nakumvuka wakati wa kampeni mwaka ule wa 2015, wakati huo akiwa mgombea wa Urais, alituahidi wafanyakazi wa nchi hii, kuwa tutakapomchagua, atafikiria maslahi yetu na kuahidi kuwa ndani ya utawala wake, ataboresha sana maslahi ya wafanyakazi.

Tulimchagua mwaka ule wa 2015 ma kuwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, lakini "alitugeuzia kibao" baada ya kumchagua kwa kutakatalia kata kata katika kipindi chote hicho cha miaka 5 na kusema kuwa hawezi kutuongezea mishahara yetu hadi pale atakapokamikisha ujenzi wa miundo mbinu yake.mikubwa aliyoianzisha, ambayo ni ujenzi wa reli ya SGR na Bwawa la umeme la Stieglers Gorge!

Umefika tena mwaka wa uchaguzi 2020, Rais Magufuli "amesahau" kuwa alitukatalia kata kata kutuongezea mishahara, licha ya kwamba alituahidi kuwa angetuongezea mishahara yetu katika kampeni yake mwaka 2015.

Wafanyakazi mwaka huu tunamwambia Rais Magufuli, kuwa hatudanganyiki tena na tuna jambo letu, ifikapo hiyo kesho kutwa ya terehe 28, siku ambayo tunakwenda kufanya maamuzi ya kiongozi gani tutakwenda kumchagua kwenye uchaguzi wa mwaka huu na wafanyakazi wa nchi hatutakubali tena kuoigwa "fix" nyingine na tutaenda mchagua mgombea wa Urais ambaye tunaamini kuwa ndiye msema kweli kwa ahadi yake ya kutuongezea mishahara Mara tu tutakapomchagua na kuwa Rais wa nchi hii.
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom