Hivi Rais Magufuli anavyohamasisha utumiaji wa pombe ya gongo na uvutaji wa bangi anataka vijana wa nchi hii wawe vichaa?

Kwa hili nipo na Rais wangu.

Sio kila kitu cha kupinga, maendeleo hayana chama
acheni tule ndumu bhana maisha yenyewe yako wapi?!

Sent using Jamii Forums mobile app
Kwa hiyo una maana bange ni kwa ajili ya wale waliokata tamaa ya maisha siyo!!! Naamini huyu Rais anafahamu kuwa Watanzania wengi wamekata tamaa kwa jinsi alivyoyafanya maisha yao kuwa magumu. Ndiyo sababu anahamasisha uvutaji wake kupitia kwa Waziri!!!
 
unauhakika kama rais alimwambia waziri avute bangi au umesimuliwa? nilikuwepo uwanjani maneno aliyoyatumia hayakua yakumwambia avute bangi kama agizo, isitoshe Yale yalikua ni maneno ya utani tu, msipende kubeba bango kwa kila jambo afu mnapotosha watu. hivi kwa akili yako rais anaweza kumwambia mteule wake akavute bangi? mcwe watu wa kupinga kila jambo
Kwa hiyo unataka kutuambia kuwa alikuwa anafanya utani kama Magufuli au kama Rais Magufuli!!!?
 
Tumemsikia wenyewe kwa masikio yetu hivi Leo kule Makambako, Rais wetu Magufuli wakati akiwahutubia wakazi wa huko akimwelelekeza Waziri wake wa Maji, kuwa eti avute bangi kisirisiri, ili awe mkali katika kushughulikia miradi ya maji nchini!

Tulimsikia pia Rais Magufuli huko siku za nyuma akisema kuwa pombe ya gongo itengenezwe kitaalamu zaidi ili ihalalishwe watu wainywe!

Ndipo hapo ninapojiuliza hivi Rais Magufuli "kupigia" debe pombe ya gongo na kuvuta bangi haoni kuwa analipotosha Taifa hili, ili vijana wake wawe walevi wa kupindukia kwa kutumia hivyo vilevi ambavyo kisheria ni haramu??

Najiuliza pia hivi Rais wetu kama kweli ni muumini wa Dini ya kikristo, ambayo katika Biblia takatifu inaeleza wazi kuwa ulevi wowote ule ni dhambi kubwa ambayo mshahara wake ni kuchomwa moto wa milele na milele hapo siku ya hukumu huko mbinguni, inakuwaje basi yeye awe ndiye muhamasishaji mkubwa wa vitendo hivyo, ambavyo ni kinyume cha maadili ya dini zetu zote za kiislam na kikristo??

Raisi keshawajua..... anaamini mtalishikia bango na kusahau yale mambo ya CGA sjui TAG.......ahhhh hadi jina linanitoka... yule ambaye spika alisema hawatafanya nae kazi
 
Tunajua hanywi pombe! lakini NDUMU ehhhhhh! ulizia seminari ya katoke kilichomfukuzisha ni nini! Hata lile dirisha alilobomoa alilifidia juzi. Na alipokuwa Lake sec ndiyo mtu na NDUMU.
Ndumu tokea mwaka 1961 ni marufuku lakini wavuta bangi hawajawahi kupungua zaidi ya kuongezeka zaidi hata akiruhusu kuvuta nchi haitakuwa kama Jamaica au uholanzi ambapo bangi ni ruksa saa 24
 
Tumemsikia wenyewe kwa masikio yetu hivi Leo kule Makambako, Rais wetu Magufuli wakati akiwahutubia wakazi wa huko akimwelelekeza Waziri wake wa Maji, kuwa eti avute bangi kisirisiri, ili awe mkali katika kushughulikia miradi ya maji nchini!

Hivi Watanzania kila kitu mnachukulia serious kiasi kwamba hata Rais asiseme neno la utani; na mahali pa utani. Akiwa mkali sana mnasema ananuna sana au mkali sana. Mbona ukimsikiliza alisema kwa utani lakini ndani yake alikuwa anasisitia jambo muhimu. Tusije kuwa watu wa kukwazwakwazwa mara kwa mara.. hata kwa vitu vya utani..

Halafu watu mkumbuke kuwa bangi inaendelea kuondolewa sehemu nyingi duniani kama kosa la kihalifu..
 
Je, ni halali, haki na busara kwa Rais wetu kuhamasisha unywaji wa gongo na uvutaji wa bangi, tena kwenye mkutano wa hadhara huku akimshauri Waziri!!!?
Najaribu ku-imagne impact ya kauli yake Mkuu wa nchi

Atawafanya Pollisi wetu wafanye kazi yao katika mazingira magumu sana......

Kwa kuwa kama yeye Rais "amehalalisha" bangi ivutwe waziwazi kwa kumuelekeza Waziri wake wa maji akaivute bangi

Sasa Polisi wakimkamata kijana yeyote mvuta bangi, atawajibu kuwa hii bangi "imehalalishwa" na Rais mwenyewe, sasa nyinyi Polisi hamna ubavu wa kunikamata!
 
Hivi Watanzania kila kitu mnachukulia serious kiasi kwamba hata Rais asiseme neno la utani; na mahali pa utani. Akiwa mkali sana mnasema ananuna sana au mkali sana. Mbona ukimsikiliza alisema kwa utani lakini ndani yake alikuwa anasisitia jambo muhimu. Tusije kuwa watu wa kukwazwakwazwa mara kwa mara.. hata kwa vitu vya utani..

Halafu watu mkumbuke kuwa bangi inaendelea kuondolewa sehemu nyingi duniani kama kosa la kihalifu..
Mzee Mwanakijiji ngoja nikuulize swali dogo tu, hivi Rais anatakiwa kuwa mtu wa utani katika mambo serious?

Hivi unadhani kauli yake Rais aliyoitoa hadharani, huku akipata coverage kubwa ya vyombo vya habari, ikiwemo kurushwa Live na TBC itakuwa imeleta impact gani kwa jamii kwa ujumla wake??

Ndiyo maana ya kusisitiza kuwa ni vyema Rais wetu akawa anasoma hotuba anazoandaliwa na wataalamu wa hotuba, ili kuepuka aibu kama hii iliyotokea kule Makambako
 
Najaribu ku-imagne impact ya kauli yake Mkuu wa nchi

Atawafanya Pollisi wetu wafanye kazi yao katika mazingira magumu sana......

Kwa kuwa ni kama yeye Rais "amehalalisha" bangi ivutwe waziwazi kwa kumuelekeza Waziri wake wa maji akaivute bangi

Sasa Polisi wakimkamata kijana yeyote mvuta bangi, atawajibu kuwa hii bangi "imehalalishwa" na Rais mwenyewe, sasa nyinyi Polisi hamna ubavu wa kunikamata!
Mwendo wa bangi nibangue kama koroshow kesho mapema barabara nawasha misokoto mitatu kwa mpigo na dumu langu la gongo mgongoni kama nfuko pc tuone nani atanigusa ruksa
 
Mwendo wa bangi nibangue kama koroshow kesho mapema barabara nawasha misokoto mitatu kwa mpigo na dumu langu la gongo mgongoni kama nfuko pc tuone nani atanigusa ruksa
Ni kweli kabisa, wamewaweka katika mazingira magumu sana Polisi wetu watakaokuwa wanataka kutekeleza sheria
 
Tumemsikia wenyewe kwa masikio yetu hivi Leo kule Makambako, Rais wetu Magufuli wakati akiwahutubia wakazi wa huko akimwelelekeza Waziri wake wa Maji, kuwa eti avute bangi kisirisiri, ili awe mkali katika kushughulikia miradi ya maji nchini!

Tulimsikia pia Rais Magufuli huko siku za nyuma akisema kuwa pombe ya gongo itengenezwe kitaalamu zaidi ili ihalalishwe watu wainywe!

Ndipo hapo ninapojiuliza hivi Rais Magufuli "kupigia" debe pombe ya gongo na kuvuta bangi haoni kuwa analipotosha Taifa hili, ili vijana wake wawe walevi wa kupindukia kwa kutumia hivyo vilevi ambavyo kisheria ni haramu??

Najiuliza pia hivi Rais wetu kama kweli ni muumini wa Dini ya kikristo, ambayo katika Biblia takatifu inaeleza wazi kuwa ulevi wowote ule ni dhambi kubwa ambayo mshahara wake ni kuchomwa moto wa milele na milele hapo siku ya hukumu huko mbinguni, inakuwaje basi yeye awe ndiye muhamasishaji mkubwa wa vitendo hivyo, ambavyo ni kinyume cha maadili ya dini zetu zote za kiislam na kikristo??

Tatizo lipo kwenye katiba yetu, kwamba Rais hashitakiwi akivunja sheria.---- si yeye aliyesema wafungwa wakizembea kazi wapigwe teke.🤔🤔🤔
 
Bangi inafaida nyingi kuliko madhara yake,na bangi hutumika kila siku mahospitalini na hotelini....

Sema inatakiwa iwe inachakachuliwa kupunguza toxins zilizomo ambazo kwa watu wa kawaida hasa nchi masikini huwa zinaenda kuumiza ubongo na kuwaweka wa machizi kwasababu ya ubongo kutokuwa na afya yan vile watu tunashindia mchicha daily,urojo,vichipsi n.k

Bangi pia hufaa kupikwa kama mboga aidha uichemshe uile kama supu kama supu ya spinachi kule hiroshima au taiwan au uiunge na nyanya+ mavinegar inakuwa ya ukweli sana

Sent using Jamii Forums mobile app
Sijuhi ulikuwa na maana gani uliposema "toxin" labda kama umeilima kwa mbolea za viwandani, ila bangi haina "toxin" yoyote.
 
Back
Top Bottom