Hivi Rais Magufuli anavyohamasisha utumiaji wa pombe ya gongo na uvutaji wa bangi anataka vijana wa nchi hii wawe vichaa?

Mystery

JF-Expert Member
Mar 8, 2012
15,483
30,155
Tumemsikia wenyewe kwa masikio yetu, kule Makambako, Rais wetu Magufuli wakati akiwahutubia wakazi wa huko akimwelelekeza Waziri wake wa Maji, kuwa eti avute bangi kisirisiri, ili awe mkali katika kushughulikia miradi ya maji nchini!

Tulimsikia pia Rais Magufuli huko siku za nyuma akisema kuwa pombe ya gongo itengenezwe kitaalamu zaidi ili ihalalishwe watu wainywe!

Ndipo hapo ninapojiuliza hivi Rais Magufuli "kupigia" debe pombe ya gongo na kuvuta bangi haoni kuwa analipotosha Taifa hili, ili vijana wake wawe walevi wa kupindukia kwa kutumia hivyo vilevi ambavyo kisheria ni haramu??

Najiuliza pia hivi Rais wetu kama kweli ni muumini wa Dini ya kikristo, ambayo katika Biblia takatifu inaeleza wazi kuwa ulevi wowote ule ni dhambi kubwa ambayo mshahara wake ni kuchomwa moto wa milele na milele hapo siku ya hukumu huko mbinguni, inakuwaje basi yeye awe ndiye muhamasishaji mkubwa wa vitendo hivyo, ambavyo ni kinyume cha maadili ya dini zetu zote za kiislam na kikristo??
 
Bangi inafaida nyingi kuliko madhara yake,na bangi hutumika kila siku mahospitalini na hotelini....

Sema inatakiwa iwe inachakachuliwa kupunguza toxins zilizomo ambazo kwa watu wa kawaida hasa nchi masikini huwa zinaenda kuumiza ubongo na kuwaweka wa machizi kwasababu ya ubongo kutokuwa na afya yan vile watu tunashindia mchicha daily,urojo,vichipsi n.k

Bangi pia hufaa kupikwa kama mboga aidha uichemshe uile kama supu kama supu ya spinachi kule hiroshima au taiwan au uiunge na nyanya+ mavinegar inakuwa ya ukweli sana

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Chini ya awamu hii mambo yote kwa siri siri tu.

kuvuta bangi
kujenga chattle international airport
upigaji wa 1.5tr
nk nk
 
kwan kahamasisha? kasema ikipimwa basi iuzwe... sasa unafikiri kuna kilichipimwa kikawa kibaya? sawa ni kirasimishwe... angalia konyagi ina alcohol parcent kubwa lakin inauzwa! swala ni kuwa hapo nyuma gongo ilikuwa haipimwi inauzwa kiholela hvyo watu wanakunywa bila kujua inakias gan cha kilevi ndan yake... na ndo maana ikawa hatari kwa sababu ya alcohol iliyopo ndan ya gongo.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Hivi mpaka leo hii unajiuliza maswali juu ya kauli za huyo jamaa?

Unamuona ni mzima kweli?
Hakika kwa sasa ndiyo naona umuhimu wa wale jamaa zetu wa kitengo, kuwafanyia "vetting" hawa jamaa tunaotaka kuwapa dhamana kubwa za kitaifa, ili wajihakikishie kuwa mtu anayeshika wadhifa huo anakuwa sawa huko upstairs.......

Ili tuliepushe Taifa letu na aibu, kama hii tuipatayo hivi sasa
 
Tunajua hanywi pombe! lakini NDUMU ehhhhhh! ulizia seminari ya katoke kilichomfukuzisha ni nini! Hata lile dirisha alilobomoa alilifidia juzi. Na alipokuwa Lake sec ndiyo mtu na NDUMU.
 
Back
Top Bottom