Hivi Rais Magufuli anadhani kwa kujifichia kwenye madawa watanzania atamsamehe hata?

H.T.P

JF-Expert Member
Jul 11, 2015
1,169
1,298
Nauangalia mwenendo mzima Wa nchi napata picha nyingi sana kichwani kwangu.

Kwanza Magufuli ameshtuka kwamba kauli zake za kibabe kwa wananchi wanyonge zimempotezea mvuto hivyo ametafuta ishu ya kuwapoteza wasahau machungu, akagundua njia ya madawa na kuwachafua wapinzani,

Magufuli anajua kabisa kwamba uchumi umekua hovyo tangu aingie ikulu na yote aliyoahidi wala hatayatekeleza,

Magufuli amejua kabisa kwamba, nguvu ya upinzani inakua kwa kasi hasa jinsi ambavyo viongozi Wa upinzani wamekua na hekima na busara katika matamshi na maamuzi,

Kama Kweli Magufuli anania njema na hii nchi, kama anataka kupambana na ufisadi kwanza angeruhusu kwanza Makonda achunguzwe ili ukweli juu ya Mali alizochuma kwa muda mfupi ujulikane,

Nimefwatilia kinachoendelea Ukumbi Wa Nyerere nimegundua ni siasa kabisa na kampeni za wazi kabisa..

Hebu jiulize, kile kiitikio wanachoitikia kina mama mle ndani kimeandaliwa SAA ngapi??? Hivi nchi hii jamani haishi vituko? kila anayekuja anakuja na sura yake ilimradi mtanzania aendelee kupumbazwa tu.

Sasa naona baada ya kumtaja Mbowe hawataji tena..
 
Nimeleta mada kama hii nikihoji msururu wa matukio mengi yaliyosahaulika ila bahati mbaya hawa mods(sijui hawaguswi na hali hii) wameunganisha uzi wangu.

All in all hii ni siasa tu.
 
Kuna ongezeko la viwanda 2,000. Uchumi @7% rate of growth, ajira zinakuja sema kwa ssa tumesitisha, wanafunzi wa sekondari wanachujwa kwanza..... Tutafika tu japo kwa taabu.
 
KUMBE MPK WALE MAJIMAMA YASIYOKUWA NA KAZI MJINI YAPO EEEEEEEE KAZI KWELI KWWELI


UJINGA NI KUSEMA HAPA KAZI TUU HUKU HUNA KAZI ZAIDI YA KUZUNGUKA NA KIVULI ILI KUKWEPA JUA
 
Wahuni hawa hawana jipya baada ya usanii wao wa wafanyakazi hewa, uhakiki wa vyeti sasa wamehamia kwenye madawa ya kulevya! Huku uchumi wa nchi ukizidi kudhoofika.

Wapuuzi hawa..

Vita hewa kabisa hii..

Makonda msanii haswaa..

Sasa hawa watoto sijui wa kutoa vibwagizo kule nyuma sijui walifanya rehersal lini??

Usanii mtupu.
 
Ukitaka kujua msingi wa mtu yeyote inabidi kuchunguza alikotokea - uangalie aliko na ujue anakokwenda. Binadamu ambaye utotoni mwake aliishi maisha na kukataliwa na mmoja wa wazazi wake .. kuna hali fulani ya kuwa na mapungufu kwenye fikra zake.
Hali hiyo lazima imuathiri hata kwenye utendaji wake wa kazi ....

Tuwe na utaratibu wa kuwafanyia uchunguzi viongozi wetu kabla ya kuwaweka kwenye uongozi. Nakumbuka enzi za mwalimu ... mgombea alikuwa anapendekezwa na sio kujipendekeza yeye mwenyewe. Uongozi ni kazi .. utawala sio kazi ...
 
Wahuni hawa hawana jipya baada ya usanii wao wa wafanyakazi hewa, uhakiki wa vyeti sasa wamehamia kwenye madawa ya kulevya! Huku uchumi wa nchi ukizidi kudhoofika.
Sijapata uhakika bado..
Ila nasikia makusanyo ya January ni AIBU kabisa Mkuu.
 
  • Thanks
Reactions: BAK
Safi sana timu Ufipa,endeleeni kupiga kelele ili makondakta nae azidishe moto ili vijana wetu wapone na hili janga maana kasema kelele zenu ni kichocheo kwake!
 
Sijapata uhakika bado..
Ila nasikia makusanyo ya January ni AIBU kabisa Mkuu.
Achilia mbali hali ilivyo MBAYA huko kwenye ELIMU BURE. Huyu bwana ana tatizo la kichwa ambalo halijawahi kupata daktari wa kulisema. Alichoweza mpaka sasa ni kubuni MIROPOKO na vitisho tu kila siku vinavyomuongezea wanaomchukia kila kukicha. Waliopindisha taratibu za chama chao kumuweka nadhani watakuwa na tiba ya kukitibu chama chao ambacho ni obvious kitakuwa taabani by 2020.
 
aibu ya mwaka muda na resources zote wamekamata kete mia ngapi sijui na kipisi cha bangi
 
Nauangalia mwenendo mzima Wa nchi napata picha nyingi sana kichwani kwangu.

Kwanza Magufuli ameshtuka kwamba kauli zake za kibabe kwa wananchi wanyonge zimempotezea mvuto hivyo ametafuta ishu ya kuwapoteza wasahau machungu, akagundua njia ya madawa na kuwachafua wapinzani,

Magufuli anajua kabisa kwamba uchumi umekua hovyo tangu aingie ikulu na yote aliyoahidi wala hatayatekeleza kuyatelekeza,

Magufuli amejua kabisa kwamba, nguvu ya upinzani inakua kwa kazi hasa jinsi ambavyo viongozi Wa upinzani wamekua na hekima na busara katika matamshi na maamuzi,

Kama Kweli Magufuli anania njema na hii nchi, kama anataka kupambana na ufisadi kwanza angeruhusu kwanza Makonda achunguzwe ili ukweli juu ya Mali alizochuma kwa muda mfupi ujulikane,

Nimefwatilia kinachoendelea Ukumbi Wa Nyerere nimegundua ni siasa kabisa na kampeni za wapi kabisa..

Hebu jiulize kile kiitikio wanachoitikia kina mama mle ndani kimeandaliwa SAA ngapi??? Hivi nchi jamani haishi vituko kila anayekuja anakuja na sura yake ilimradi mtanzania aendelee kupumbazwa tu.

Sasa naona baada ya kumtaja Mbowe hawataji tena..
Baada ya kumtaja Mbowe,lengo limetimia.Hakuna atakayetajwa tena
 
14 Reactions
Reply
Back
Top Bottom