Hivi raia tuendelee kuonewa na Wanajeshi huku Mitaani hadi lini?

ngaiwoye

JF-Expert Member
Aug 26, 2014
1,777
2,489
Jamani wanajeshi tunaokaa nao huku mitaani wanajisahau sana na kujikweza sana kias kwamba unakuta raiya wa kawaida wanaonewa hadi kwenye mambo madogomadogo sana. Na unakuta raia wa kawaida pia hawajui ni wapi pa kwenda kulalamika ikiwa wameonewa na askari wetu hawa wa jeshi.

Mfano mdogo hapa mtaani kwetu wapo wanajeshi wengi ila kuna mmoja ambae anaishi hapa ambae ana watoto wakorofi sana, watoto wake wana kazi ya kupiga wenzao halafu baba yao hachukui hatua kabisa, wala hakanyi wanae, yaani mzazi ukienda kushtaki anakuwa upande wa watoto na anakua mkali kama mbogo (matisho kwa raia sababu ye mwanajeshi).

Jana nilisikitika sana, mtoto wa mwanajeshi huyo alimpiga mwenzie vibaya sana akavimba kweli kichwani, mama wa mtoto aliepigwa akaenda kushtaki ili yule mtoto akanywe lakin yule mwanajeshi bila haya alimtetea mwanae mno.

Kwakua hapa kuna washauri wa maana, je hawa wanajeshi wanapoonea raia hivi, huwa raia wanatakiwa wakalalamike wapi?
 
Raiya = raia

Anzieni serikali ya mtaa

Kama vipi pelekeni polisi

Mkiwa na muda mjiunge kwa pamoja raia pelekeni makalamiko yenu kwa mkuu wa kambi aliyopo

Ikishindikana hao watoto wapeni kichapo cha "mwana ukome" then atajifunza kuonya wanae
 
Mambo mengine ni kuyaendekeza tu!!!

Huyo ni raia wa Tanzania na anatakiwa awe mfano haswa, uanajeshi sio sababu ya kufanya hayo (kama kweli anafanya) kwanza anaaibisha jeshi!!!

Fuata ushauri wa BADILI TABIA
 
Last edited by a moderator:
ngaiwoye

Wakatazeni watoto wenu wasicheze na watoto wa mwanajeshi.hiyo ni hulka haihusiani na yeye kuwa mwanajeshi.hata angekuwa kambini angetetea tu
 
Last edited by a moderator:
Nendeni polisi mkashitaki iwapo watoto wake wametenda jinai. Huyo ni binadamu na raia kama nyie nawashangaa mnavyomuogopa. Uanajeshi wake akiwa kazini/vitani sio huko mtaani/uswahilini. Kama iwapo watoto wake hajatenda jinai ni ugomvi mdogo mdogo na hatoi ushirikiano kama mzazi fuateni ushauri wa ulitolewa hapo juu wa kuitenga hiyo familia (akitokea mnafiki akishirikiano nao naye mnatenga) ili baba na mama wacheze na watoto wao halafu muone filamu ya mapigano wakipigana wenyewe kwa wenyewe.
 
Mambo mengine ni kuyaendekeza tu!!!

Huyo ni raia wa Tanzania na anatakiwa awe mfano haswa, uanajeshi sio sababu ya kufanya hayo (kama kweli anafanya) kwanza anaaibisha jeshi!!!

Fuata ushauri wa BADILI TABIA

Nakuunga mkono........huko ni kuliaibisha jeshi pia sio nidhamu!
 
Last edited by a moderator:
ngaiwoye


wachape tu hao, kama hawana silaha hawawezi kupigana zile za gitaa labda awe komando na makomando hawanaga shari.wengi wenye shari ni makapuku,wanapigika vizuri.
 
Last edited by a moderator:
Huyo Ni Kumfanyuia Umafia Tu
NiPM Nikupe Maujanja, Maana Nina Njaa Nao Sana Hawa Wajeda Na Askari Polisi
Ahsante Jigo
 
Hao watoto ukikutanae mpe kwenzi tatu za kichwa tena za nguvu huku ukimwambia kosa lake halafu ulete mrejesho believe me hatarudia.
 
Hili ni tatizo kwa nchi nyingi za kiafrica tena sn Tanzania watu wachache wanapokuwa na nyadhifa tofauti za serikali au idara yeyote inayo husiana na serikali wanajion wapo (above the law)kwani matukio mangapi watu wameyaona tena mabaya yA udhalilishaji kwa raia ,kisa ww police au solider ,wazir, mkit wA serikali za mtaa hata mgambo wa City .hapo utawala bora upo wapi ?
 
Back
Top Bottom