Hivi R, L na H, ni Ugonjwa wa Taifa?

Sio r na l tu, ni kwamba Watanzania wengi hawawezi kuandika kiswahili. Huko Facebook ndio balaa kabisa, najiuliza hawa watu walimaliza vipi shule za msingi.

Bora fb!jana kun mtu kasema amesoma Pugu Advanced!jamani anavyoandika km standard 4!ikabiid nimuulize Pugu umesoma ww??akaanza nitajia had walimu🤣! Yaani kinyaa
 
Makabila mengi Mkoani wa Mara hayana L; kila kitu ni R tu. Wengi hudhani ni wakuria tu ila ukweli ni kuwa makabila karibu yote ya mkoa huo hayana R kabisa. Sauti ya R ni nuksi kwao
JIWE hajui kingereza japo sometimes huwa anafosi ila akiongea kiswahili ndio anachapia kabisa hizo "R,L'
 
Hizo ni athari za lugha ya nyumbani na sio rahisi kubadilisha kama unavyofikiri.Lugha yoyote inayokuja kwako kama lugha ya pili lazima itaathiriwa na lugha ya kwanza.Nailo ni swala la ulimi sio akili.Hata wazungu kwenye nchi wanazozungumza kingereza wanatofautiana lafudhi kati ya nchi na nchi wakati lugha ni ile ile.kwaiyo hiyo ni kawaida sana kwenye jamii yetu na kamwe hatuwezi kufanana ulimi.
kwenye lafudhi sawa tunaathiriwa na lugha za kwanza, lakini hata kwenye kuandika!!! reo. rakini, lais nk
 
Kuna janga lingine naliona limeshamiri, mfano;
"fulani katoa NYIMBO mpya"
"Nimesikiliza Nyimbo yako nzuri sana"
Inakera na kuchefua sana kuona watu wazima wana haribu hii lugha adhimu ya Kiswahili.
 
Kuna "dha" na "za" bila kusahau "thu"na "su".
"Dhambi" mtu anaandika "zambi" unakuta "thamani" mtu anaandika "samani".

Kule kwetu kuna "bhwi" watu hugeuza inakuwa "bwi"
Kunawatu wanaitwa "Nyabhwire" mjini wanaiita "Nywabwire" hii sio sawa "Bhoke" nao hujiita "Boke". Hii siyo sawa wenzangu.
 
Opuk Jater,
Hizo lugha za' nyumbani' hazikuwepo miaka ya 50 na sitini??? Mfano mzuri ni mwalimu Nyerere. Yeye alikuwa ni mtu wa bara na alikuja Dar akiwa mtu mzima lakini matamshi yake ya kiswahili yalikuwa mazuri sana.
 
Na umesahau matumizi ya maneno "Ga" "Ge" na "Gi" mfano "alikwendaga" yananikera sana.
 
racso kaunda,
Nenda Zanzibar ukaonje ladha ya Kiswahili hawana usumbufu wa herufi kimaandishi na matamshi sijui ni ule urojo wanaokula
Kwenye mitihani ya kitaifa, wanafunzi wa Tanganyika wanafanya vizuri sana kwenye Kiswahili kuliko wa upande wa visiwani, huko ulikosema wanajua Kiswahili.
 
Kwenye mitihani ya kitaifa, wanafunzi wa Tanganyika wanafanya vizuri sana kwenye Kiswahili kuliko wa upande wa visiwani, huko ulikosema wanajua Kiswahili.
Si juzi tu umesikia watoto wamefaulu lakini hawajui kusoma wala kuandika sijui ndo Multiple choice au tia √ × Ila ni ukweli usio pingika hata mkaazi wa Jumba jeupe zinampa shida hizi herufi
 
Kwenye mitihani ya kitaifa, wanafunzi wa Tanganyika wanafanya vizuri sana kwenye Kiswahili kuliko wa upande wa visiwani, huko ulikosema wanajua Kiswahili.

Lugha inazungumzwa mdomoni, Hata mzungu naweza pasi mtihani wa darasani akisoma.
 
Lugha inazungumzwa mdomoni, Hata mzungu naweza pasi mtihani wa darasani akisoma.
Mkuu Lugha inazungumzwa na kuandikwa pia. Tena ya kuandika ndiyo ya muhimu zaidi kwa sababu inakuwa documented (sijui Kiswahili cha hili neno, kama wajua nijuze) na hivyo kuwafia wengi zaidi wakati huo mwandishi haupo nao, japo kwa upande wa wana-habari kama radio, tv, nk hata hiyo ya kuongea, lugha fasaha ni muhimu pia.
 
Back
Top Bottom