Hivi R, L na H, ni Ugonjwa wa Taifa?

nuruyamnyonge, Haya si makosa ya kisarufi, useme kwa mfano, kusema anakujaga ni makosa, Kiswahili sahihi ni kusema anakuja.

Haya ni makosa ya kuchanganya herufi.

Kwa mfano, Magufuli mtu atamke "Magufuri" au "Mzee wa Kiraracha" mtu atamke "Mzee wa Kilalacha".

Hivyo basi, utaona ni vigumu kuweka kanuni katika makosa ambayo kimsingi si ya kisarufi (grammatical), bali ni ya kimatamshi (phonetical).
 
Huu ni ugonjwa wa taifa, ni 'aibu' sana miandiko mibovu kweli mpaka watu maarufu wenye nyadhifa kubwa tu serikalini ama mashirika binafsi hawajui kutofautisha r na l, a na ha, inafikia hatua msomaji unaona hata aibu kwa niaba ya mwandishi
 
Tatizo lingine kubwa ni hili kama lako. Wengi hawajui wapi h au a inatumika. Mfano wewe ulitakiwa kuandika waandishi. Au mwingine hajui tofauti ya HANA na ANA.
Hili ni tatizo la kimataifa, Wajamaica, hasa wa Kingston, katuka Kiingereza wengi hawajui kuweka h sehemu inapotakiwa na wanaiweka sehemu isipotakiwa.
 
Tatizo lingine kubwa ni hili kama lako. Wengi hawajui wapi h au a inatumika. Mfano wewe ulitakiwa kuandika waandishi. Au mwingine hajui tofauti ya HANA na ANA.
Mimi ni typing error, ni kweli nimekosea na nilijaribu nirekebishe ikanigomea.
 
Watu wanajifunza na kunyoosha lugha. Hajataka tu.

Mbona kuna wazee wengi tu wamezaliwa huko na wanaongea vizuri tu.

Sipingi hoja yako, lakini naona ni tatizo la kawaida kwa wengi. Na ni wachache sana wanafanya jitihada kuondokana na hilo kwani ni tatizo linalovumika na kueleweka dunia kote, na katika lugha zote.
 
morenja,

Huku kwenye mitandao ni kosa la mtu kushindwa kuandika au kujua herufi sahihi. Tatizo lake Magufuli ni wakati wa kuongea, hayo ni matatizo ya kibinadamu kutoka lugha moja au nyingine. Sioni shida yoyote kwake kwenye hili.
 
Haya si makosa ya kisarufi, useme kwa mfano, kusema anakujaga ni makisa, Kiswahili sahihi ni kusema anakuja.

Haya ni makosa ya kuchanganya herufi.

Kwa mfano, Magufuli mtu atamke "Magufuri" au "Mzee wa Kiraracha" mtu atamke "Mzee wa Kilalacha".

Hivyo basi, utaona ni vigumu kuweka kanuni katika makosa ambayo kimsingi si ya kisarufi (grammatical), bali ni ya kimatamshi (phonetical).
Asante kwa elimu Kiranga.
 
Huku kwenye mitandao ni kosa la mtu kushindwa kuandika au kujua herufi sahihi. Tatizo lake Magufuli ni wakati wa kuongea, hayo ni matatizo ya kibinadamu kutoka lugha moja au nyingine. Sioni shida yoyote kwake kwenye hili.
Rais mzima hajui kuongea Kiswahili lugha ya taifa na wewe mwananchi huoni shida yoyote?
 
Lazima tufike sehemu sasa tukubaliane na hali, kanda ya ziwa, mbeya kote, kanda ya kati na sehemu mbalimbali hizi herufi zimeshashindikana. Tukubali tu kama vile Mjerumani hawezi kusema roho anasema hoho au mtu wa india kusema wewe hawezi hata umshikie bunduki atasema veve. Au kama kiingereza cha kimarekani kilivyo tofauti kimatamshi na kiingereza cha uingereza. Kuna sehemu mpaka bbadhi ya majina yameathirika KAROLI...KALOLI,nk
 
Rais mzima hajui kuongea Kiswahili lugha ya taifa na wewe mwananchi huoni shida yoyote?

Mkuu tafadhali, mimi sio mshabiki wa Magufuli, lakini haimaanishi nitamponda kwenye tatizo la kibinadamu. Magufuli anakijua kiswahili vizuri hata kama sio kwa kiwango cha kupata A+, lakini anakijua. Isipokuwa anapata tatizo ya kutamka herufi fulani fulani, kutokana na herufi hizo kutokuwepo kwenye lugha aliyozungumza hasa wakati wa utotoni.

Hilo ni tatizo ambalo hata awe rais wa dunia hakuna atakayemshangaa kutokuweza kuzitamka. Ingekuwa wakati wa kuandika pia anafanya kosa hilo ungekuwa na hoja lakini sio kwenye kutamka boss.
 
Lazima tufike sehemu sasa tukubaliane na hali, kanda ya ziwa, mbeya kote, kanda ya kati na sehemu mbalimbali hizi herufi zimeshaashindikana. Tukubali tu kama vile mjerumani hawezi kusema roho anasema hoho au mtu wa india kusema wewe hawezi hata umshikie bunduki atasema veve. Au kama kiingereza cha kimarekani kilivyo tofauti kimatamshi na kiingereza cha uingereza. Kuna sehemu mpaka bbadhi ya majina yameathirika KAROLI...KALOLI,nk
Mkuu una hoja. Kama vipi, BAKITA waamue kuwa, kutumia 'nakula' sawa, kutumia 'nakura' pia sawa. Kama ilivyo kwenye harusi, ukitumia harusi sawa, ukitumia arusi pia sawa.
 
Naamini wana JF wote mpo sawa. JF imepata bahati kuwa na waandishi au wadadavuaji wazuri sana. Lkn wapo ambao wanasumbuliwa na Maneno 'R' na 'L'. Baadhi hawajui R watumie wapi na L waweke wapi. Kuna mwana JF kaandika lais JPM badala ya rais JPM. Mwingine kaandika jambo lahisi...badala ya jambo rahisi...mwingine kaandika mahali 'namshukulu Mungu,' badala ya 'namshukuru Mungu'. Wapo pia wanaotatizwa na neno 'hawezi kufika' wakiandika 'awezi kufika'. Nia yangu ya kuandika uzi huu ni kwamba, tusome vizuri uzi za wadadavuaji wa JF ambao tunawajua wako vizuri kwenye kiswahili maana Elimu haina mwisho.

Kwa leo tushughulikie hili la mchanganyiko wa "R" na "L" kama ingewezekana kabla ya kuyaweka hayo mengine ya 'h'alafu n.k., ambayo hayo nadhani ni rahisi zaidi kuliko hili la wapi kutumia "R" na wapi panapostahili "L".
Uelewa wangu ni kwamba "hakuna kanuni maalum, mbali ya kujua au kuwa na uzoefu wa kuzitumia herufi hizi."

Ni mtu asiye makini tu anayeweza kuandika "Laisi", badala ya "Rais" hata kama hakuna kanuni inayofuatwa katika matumizi ya herufi hizi. Wakati naandika haya nimejikuta natatizwa na neno "Sara" au "Sala". Najua siku zote hutumia neno sahihi, lakini sasa hivi sikumbuki sahihi ni lipi. Bahati nzuri kuna 'google' siku hizi, kwa hiyo hakuna shida.

Wataalam wa lugha hii bila shaka wanaweza kutoa ushauri wa jinsi ya kuzitumia ipasavyo 'R' na ' L'
 
Kwa leo tushughulikie hili la mchanganyiko wa "R" na "L" kama ingewezekana kabla ya kuyaweka hayo mengine ya 'h'alafu n.k., ambayo hayo nadhani ni rahisi zaidi kuliko hili la wapi kutumia "R" na wapi panapostahili "L".
Uelewa wangu ni kwamba "hakuna kanuni maalum, mbali ya kujua au kuwa na uzoefu wa kuzitumia herufi hizi."

Ni mtu asiye makini tu anayeweza kuandika "Laisi", badala ya "Rais" hata kama hakuna kanuni inayofuatwa katika marumizi ya herufi hizi.
Wataalam wa lugha hii bila shaka wanaweza kutoa ushauri wa jinsi ya kuzitumia ipasavyo 'R' na ' L'
Mwaka 1999 alipofariki Baba wa Taifa, Mwalimu Nyerere, mwombolezaji mmoja katika kutoa pole kwa familia kupitia gazeti moja aliandika: Pore mama Malia Nyelele kwa msiba mzito. Pokea lambilambi zangu Mungu akupe uvumirivu. NILISHANGAA SANA.
 
Kwa kawaida, ningeweza kusema kwamba kiwango cha elimu aliyopata mtu kama huyu inawezekana kuwa elimu ya msingi.
Lakini kama mtu wa aina hiyo ni mtu aliyemaliza kidato cha nne au sita, hicho kitakuwa ni kielelezo tosha cha ubovu wa elimu yetu.
 
8 Reactions
Reply
Back
Top Bottom