Hivi R, L na H, ni Ugonjwa wa Taifa?

kenna

JF-Expert Member
Joined
May 30, 2014
Messages
2,116
Points
2,000

kenna

JF-Expert Member
Joined May 30, 2014
2,116 2,000
Kumbe mtu akikushinda hoja tayari anakua mwanamke?

Its funny some humans assign sex gender to other humans!

Una power kubwa sana ya ku-assign gender to other humans aisee!

Are you some powerful God or Ghost or something like that?
Kuna hoja gani ulioshinda hapo , hoja za matusi , kweeli ujinga mzigo, kuna vijora vinauzwa mtaani nadhani vitakufaa.ujinga ujinga mwingi, kha viongozi wetu wanakazi kuongoza watu wenye vichwa kama hivi du !
 

Wyatt Mathewson

JF-Expert Member
Joined
Dec 22, 2017
Messages
7,662
Points
2,000

Wyatt Mathewson

JF-Expert Member
Joined Dec 22, 2017
7,662 2,000
Kuna hoja gani ulioshinda hapo , hoja za matusi , kweeli ujinga mzigo, kuna vijora vinauzwa mtaani nadhani vitakufaa.ujinga ujinga mwingi, kha viongozi wetu wanakazi kuongoza watu wenye vichwa kama hivi du !
Nimeshinda!

Weww ni nani unipangie kama nimeshinda au sijashinda!?

Wewe jisemee mwenyewe!

Jinga wewe unaeongea na jinga!

Utakua jinga kubwa zaidi!
 

kenna

JF-Expert Member
Joined
May 30, 2014
Messages
2,116
Points
2,000

kenna

JF-Expert Member
Joined May 30, 2014
2,116 2,000
Nimeshinda!

Weww ni nani unipangie kama nimeshinda au sijashinda!?

Wewe jisemee mwenyewe!

Jinga wewe unaeongea na jinga!

Utakua jinga kubwa zaidi!
Wewe si ndio umesema umeshinda kwa kutukana matusi kama hayawani, akupangie nani wewe hay*wani, hayawani anapangiwa na nani ? Si hua anajamba tu hovyo bila utaratibu.
 

MASSHELE

Member
Joined
Jul 13, 2018
Messages
23
Points
75

MASSHELE

Member
Joined Jul 13, 2018
23 75Ugonjwa huu wa kimatamshi umezidi kukua siku hadi siku. Ingawa zamani ilifahamika kuwa husababishwa na athari za lugha mama (lugha za kikabila) kwa wale wanaojifunza kiswahili baada ya kuwa na lugha yao waliyoiamili kutoka kwa wazazi wao.

Lakini kwa sasa kwa uchunguzi tulioufanya umebaini kuwa hata wale waliozaliwa na kukulia katika kiswahili wanafanya makosa hayo ya kimatamshi kwa kiasi kikubwa. Hivyo tunaweza kusema sababu kama mazoea mabaya, kujiendekeza, uigaji, na matatizo ya kimaumbile katika utamkaji ni sababu mojawapo zinazosababisha makosa ya kimatamshi.

Kuhusu L na R , watumiaji wengi wa kiswahili wamekuwa wakifananisha matumizi ya hizi sauti mbili na kuwa sauti moja inaweza kutumika kama mbadala wa nyenzake ndiposa utakuta

-Mtu akitamka - Nisubili badala ya nisubiri

- Tafadhari badala ya Tafadhali

- Mahali badala ya mahari na kinyume chake.

- Mstali badala ya mstari

- Upiri badala ya upili

- Siri badala ya sili na kinyume chake.

Makosa haya sio tu yanaharibu lugha yetu ya kiswahili na kurithisha kiswahili kibovu kwa watumiaji wa baadaye bali pia huweza kupotosha maana hasa pale makosa haya nanapofanywa katika uandishi wa aina yeyote. Kwa mfano mtu aandikapo sili akimaanisha (jambo lililofichika) msomaji huweza kuchukulia kuwa alimaanisha (hatokula)

Utofauti wa L NA R upo wapi?

Ingawa sauti sote hizi huweza Kuwekwa katika kundi la

Vilainisho au vimadende
Sauti [l, r] zinaitwa vilainisho. Ingawa wakati zinapotolewa kunakuwa na mzuio wa mkondo-hewa kama katika utoaji wa konsonanti nyingine, mzuio huu ni mdogo sana na hausababishi ukwamizo. Wakati sauti [l] inapotolewa, ulimi huwa umeinuliwa na kugusana na ufizi, na hivyo hewa hupita kwa kuzunguka kwenye pembe za ulimi. Sauti [r] hutolewa kwa kukunja ncha ya ulimi nyuma ya ufizi.

Hata hivyo sauti[ r] ni kimadende (hutamkwa huku ncha ya ulimi ikipigapiga ufizi wa juu na sauti[ l] ni kitambaza na kwa ujumla sauti hizi hufanya majukumu tofauti kati mjengo wa neno na hakuna mpishano wa namna yeyote ile katika sauti hizi mbili.

Mwisho wewe na mimi tunalojukumu la kukilinda na kukijenga kiswahili na sio kukiharibu tumia[ l] na [R] kiusahihi.

#Masshele Kiswahili
 

Daviie

JF-Expert Member
Joined
May 20, 2016
Messages
976
Points
1,000

Daviie

JF-Expert Member
Joined May 20, 2016
976 1,000
Siku hizi ukikuta mtu ameandika "ana... " kuwa makini pengine anamaanisha "hana... " hizo R na L zinahitaji tu umakini wa mtu maana wengi wasiomakini wanachapiaga hizo herufi
 

marxlups

JF-Expert Member
Joined
Dec 12, 2011
Messages
12,905
Points
2,000

marxlups

JF-Expert Member
Joined Dec 12, 2011
12,905 2,000
Siku hizi ukikuta mtu ameandika "ana... " kuwa makini pengine anamaanisha "hana... " hizo R na L zinahitaji tu umakini wa mtu maana wengi wasiomakini wanachapiaga hizo herufi
Ana ...hana
Kalamu ...karamu
Dhana ...zana
Think ...sink😂
Thelathini ...selasini

Mtu anaweza kuuza ugomvi, mathalani mtu akisema "Tumetoka hospitali wamesema Mayasa ana UKIMWI.😦😢
 

Kichuguu

Platinum Member
Joined
Oct 11, 2006
Messages
8,522
Points
2,000

Kichuguu

Platinum Member
Joined Oct 11, 2006
8,522 2,000
racso kaunda, ]
Tatizo hili sio hapa jf tu. Yaani Waandishi na watangazaji karibu wote kwenye TV za mitandaoni wana tatizo hili R na L
Makabila mengi Mkoani wa Mara hayana L; kila kitu ni R tu. Wengi hudhani ni wakuria tu ila ukweli ni kuwa makabila karibu yote ya mkoa huo hayana R kabisa. Sauti ya R ni nuksi kwao
 

Zabron Hamis

Verified Member
Joined
Dec 19, 2016
Messages
1,203
Points
2,000

Zabron Hamis

Verified Member
Joined Dec 19, 2016
1,203 2,000
Habari Wanandugu,

Katika kitu ambacho huwa kinanishangaza katika nyakati hizi ni maandishi na matamshi ya baadhi ya herufi na silabi. Huwa najiuliza kuwa Watanzania tunakwama wapi kwenye herufi "R" na "L" kuanzia kuyaandika mpaka kutamka?

Miaka ya nyuma kulikuwa na kichaka cha kujificha kuwa kuna Makabila ambayo hayana herufi "R" kwenye lugha zao za nyumbani, hasa mikoa ya kusini (Lindi & Mtwara).

Lakini siku hizi siyo kushindwa kutamka bali yanabadilishwa kabisa. Utakuta mtu na elimu yake anakuandikia "RAKINI" badala ya "LAKINI", Eti " KALILI" badala "KARIRI", kuna muda unamsikiliza mtu mpaka unashindwa kumwelewa kama anaongea kiswahili au anatumia lugha nyingine.

Tena kuna hawa Wachungaji na Manabii ukiwaskia wakiongea ndiyo wanazikazia " L" badala ya "R". Halafu hapo bado haujahamia kwenye vyombo vya habari.

Sasa cha ajabu siwani wakiwa wanabadili matumizi ya R na L wakiwa wanazungumza Kiingereza. Kwa hiyo huu ugonjwa ni ulimbukeni uliotujaa au ni wa makusudi?


MAONI KUTOKA KWA WADAU
Bora hata kiswahili mkuu, kuliko wakichapia kiingereza.

I sink this is ... (Hapa neno sink anamaanisha THINK)
Zis is
Ze table
N.k
 

Forum statistics

Threads 1,367,641
Members 521,789
Posts 33,405,724
Top