Hivi polisi wameruhusiwa kuua wakihisi fulani ni mhalifu? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Hivi polisi wameruhusiwa kuua wakihisi fulani ni mhalifu?

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by Magobe T, Mar 29, 2009.

 1. M

  Magobe T JF-Expert Member

  #1
  Mar 29, 2009
  Joined: Mar 19, 2008
  Messages: 2,945
  Likes Received: 357
  Trophy Points: 180
  Napenda nielemishwe kwa hili. Sheria zetu zinazuia mtu kujichukulia sheria mkononi. Lakini mara nyingi nimekuwa nikisikia polisi kujichukulia sheria mkononi hasa kuua raia kwa kuwadhania kuwa ni wahalifu. Mfano, huko Arusha kuna taksi dreva ameripotiwa na vyombo vya habari kuwa aliuawa na polisi katika mazingira ya kutatanisha (hakuwa na silaha).

  Huko Mbeya polisi anadaiwa kumwua kichaa kwa kumpiga risasi kichwani. Hapa Dar es Salaam (huko Kimara) dreva teksi anadaiwa kuawa na polisi kwa kupigwa risasi akiwa ndani ya gari baada ya kuamriwa kusimama.

  Hivi karibuni waandishi wa habari walitishiwa kwa bastola na polisi walipokuwa wakifuatilia tukio fulani huko Morogoro.

  Je, hii sheria ya kujichukulia sheria mkononi haiwahusu polisi na je, polisi akishamhisi mtu kuwa ni mhalifu tayari anaruhusiwa kuua? Huu ndo utawala bora?

  Nimeona niyaseme haya kwa sababu naogopa mauaji ya namna hii yatakuwa yakiendelea na raia tutakuwa tunaendelea kukosa ulinzi wa polisi kwani badala ya kulinda maisha yetu na mali zetu wanaanza kutumaliza mmojammoja kwa kuhisi tu kuwa fulani anahusika kwenye uhalifu.

  Pia ni lini polisi anaruhusiwa kuua na lini anaruhusiwa kujeruhi tu ili kufanikisha kumkamata mtu anahehisiwa kuwa mhalifu na anayekimbia au kukataa kukamatwa lakini hana silaha yoyote? Huu ugonjwa wa kuua watu kwa risasi utaendelea hadi lini?

  Pili kuna kitu kingine kina kera. Kuna baadhi eti ni askari wastaafu na wana bastola. Sasa wakiwa baa na wakibishana kidogo (kwa maneno) na wanywaji wengine wanatoa bastola na kutishia kuua. Na wengine hata kabla ya kuulizwa wanajitangaza kuwa ni moto wa kuotea mbali na ukibisha kidogo kinatolewa cha moto. Sasa hii tabia inatoka wapi jamani Watz wenzangu? Hivi tumechokana kiasi hicho hata hatuthamini tena uhai wa wenzetu?
   
 2. Ndamwe

  Ndamwe Senior Member

  #2
  Mar 29, 2009
  Joined: Jun 11, 2008
  Messages: 107
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 35
  Hii ni hatari sana, sijui taifa letu kwa sasa linaelekea wapi. Pia sijui wanafundishwa nini huko chuoni kwao. Nilitegemea wafundishwe mbinu za kukamata waarifu, na wala sio kuwaua. TUNAHITAJI TAMKO HARAKA la serikali na mamlaka husika kuhusu mwenendo huu wa hawa polisi kwani sasa unatutia mashaka makubwa watanzania. hii inatisha sasa!
   
 3. Lambardi

  Lambardi JF-Expert Member

  #3
  Mar 29, 2009
  Joined: Feb 7, 2008
  Messages: 10,314
  Likes Received: 5,606
  Trophy Points: 280
  Polisi wetu ni waoga na hawajafuzu mafunzo...pia uoga. Wao unatokana na udhaiu wao wa kupenda rushwa....kuhofia mapambano...pia uduni wa vifaa wakati wa ambush....huwa hawana hata bullet proof ndio maana wakiambiwa jambazi oooh anawaza nikilemaa atanimaliza ngoja nimuanze...kumbejamaa hana hata wembe....nini silaha...
   
 4. paesulta

  paesulta JF-Expert Member

  #4
  Mar 30, 2009
  Joined: Mar 13, 2009
  Messages: 227
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 35
  ...mi kwangu naona tatizo kubwa ni swala la kutokuwa na uhuru wa sheria ndilo linasababisha yote haya.maana sheria yetu ingekuwa inafanya kazi kama inavyotakiwa basi matatizo yote haya wala yasingetokea......
   
 5. paesulta

  paesulta JF-Expert Member

  #5
  Mar 30, 2009
  Joined: Mar 13, 2009
  Messages: 227
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 35
  nilimaanisha....utawala wa sheria...na sio uhuru wa sheria
   
 6. paesulta

  paesulta JF-Expert Member

  #6
  Mar 30, 2009
  Joined: Mar 13, 2009
  Messages: 227
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 35
  Askari aliyemuua dereva tax awekwa lupango


  Monday, March 30, 2009 9:43 AM
  ASKARI polisi aliyemuua dereva taksi wa Kimara Suka ametiwa ndani huku uchunguzi ukiendelea kufanyika.
  Askari huyo ambaye jina lake bado halijawekwa wazi mwenye cheo cha Luteni amewekwa ndani kwa kuwa uchunguzi wa awali umegundulika risasi iliyomfikia marehemu na kupoteza maisha aliifyatua yeye na askari wengine kukiri.

  Dereva huyo aitwae Lazaro Mapi aliuawa Machi 26, Mwaka huu jijini Dar es Salaam.

  Dereva huyo aliweza kupoteza maisha yake bila ya hatia yoyote kwa kuhofiwani kuwa alikuwa jambazi jambo ambalo halikuwa kweli.

  Aliweza kuuawa na askari wakati anatoka kwenye shughuli zake za kawaida za kubeba abiria kwenye eneo hilo, ambapo awali katika eneo hilo alilokwenda kulitokea tukio la ujambazi.

  Ndipo wakati anarudi aliposimamishwa na askari hao ambao hakuwatambua kuwa ni askari kwa kuwa walivalia kiraia na kuondoka bila kutekeleza agizo hilo la polisi kwa kuhofia kuwa labda walikuwa majambazi.

  Kitendo cha kuuawa kwa dereva huyo kilitokea baada ya askari hao kumsimamisha na yeye kuondoa gari jambo ambalo liliwafanya askari hao kuhisi kuwa labda alikuwa mmoja kati ya majambazi waliofanya uporaji katika eneo hilo.

  Ndipo walipopiga risasi kuelekea katika Tax hiyo na kumpata marehemu na kufariki papohapo.

  Wakati huohuo Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Abbas Kandoro ameunda tume ya siku 14 kwa ajili ya kuchunguza undani wa kifo hicho.

  Tume hiyo iliyoundwa na mkuu huyo ni ya kuchunguza kwa umakini chanzo cha kifo cha dereva huyo ambayo itaongozwa nje na maaskari ili kubaini kama kuna kiini kingine zaidi ya hicho.

  Na Chondoma Shabani, Dar es Salaam
   
 7. Pascal Mayalla

  Pascal Mayalla JF-Expert Member

  #7
  Mar 30, 2009
  Joined: Sep 22, 2008
  Messages: 24,589
  Likes Received: 18,573
  Trophy Points: 280
  Asante Teles kwa kuibua issue hii. Kwa mujibu wa sheria yetu, hakuna mtu yoyote anaruhusiwa kuua bila shera kufuata mkondo wake. Hata wanao hukumiwa kifo, ni mpaka rais asaini.
  Kinachofanywa na polisi wetu, ni ukiukwaji mkubwa wa haki za binaadamu ambao hawa polisi wetu hawazijui.

  Kwa mujibu wa sheria penal code na criminal procedure, polisi anatakiwa kutumia reasonable force wakati wa kufanya arrest. Akitumia nguvu zaidi ili liable for prosecution.

  Ziko sheria makini sana zinazoelekeza ni wakati gani polisi atatumia silaha kwenye arrest atempt, only mtuhumiwa ni armed na ikiwa imeelekezewa kwa polisi or on the chase na hideout.

  Polisi pia anaweza kutumia silaha kuzuia jaribio la kutoroka kwa mtuhumiwa asiye na silaha. Hapa polisi anatakiwa kumpiga risasi miguuni ili isiweze kukimbia.

  Kwenye kesi ya Uhaini ya 1982, wakili Murtaza Lakha, aliichachafya sana serikali mahakamani kufuatia kuuwawa kwa
  Mtuhumiwa Martin Tamimu, ambaye alikuwa ni comandoo, alipozingirwa ili akamatwe, aliruka ukuta, akadandia pick-up up iliyokuwa kwenye mwendo kasi lakini hakuwa na silaha yoyote.
  Mwenye pick-up alipogundua, akasimamisha pembeni, polisi wakaizingira hiyo pick-up, wakamiminia risasi 7 toka umbali wa meta 3!. Lakha akauliza hii ni arrest atempt gani polisi kupiga risasi 7 umbali wa mita 3 wakati risasi moja tuu ilitosha!.
  Huu ni unyama wa polisi na kuna matukio mengi sana ya kutisha na kusikitisha yanayofanywa na polisi kuua raia wasio na hatia. Haya yanaripotiwa ni machache kati ya mengi yasiyoripotiwa.
  Hii kesi ya Zombe, japo atashinda, inafungua milango ya polisi kuwa makini zaidi na kazi yao, vinginevyo mkono wa sheria ambao ni mrefu, utawakuta.
   
 8. M

  Magobe T JF-Expert Member

  #8
  Mar 31, 2009
  Joined: Mar 19, 2008
  Messages: 2,945
  Likes Received: 357
  Trophy Points: 180
  Kweli Pasco, inasikitisha sana. Leo nilipita karibu na Kituo cha Polisi pale Msimbazi - Kariakoo. Nikakuta gari la mgambo limesimama hapo na baadhi ya watu (wanaume na wanawake) walikuwa wanasukumizwa ndani hata bila kukaidi chochote.

  Sijui kama walikuwa mgambo au polisi (maana walikuwa wamevaa kiraia). Nilisimama nikaangalia kwa muda 'behaviour' ya hao askari nikajisikia vibaya sana.

  Hata watu wengine walikuwa wakiangalia kilichokuwa kinaendelea. Nikawa nifikiri hivi bila kutumia nguvu sana (kumdhalilisha mtu) askari haonikani amefanya kazi? Askari mwenye akili timamu anamsukumiza mtu ambaye anaingia kwenye gari mwenyewe bila kukataa kama mzigo.

  Halafu akishaingia badala ya kumwambia asogee kule mbele anasukumwa tena kwa nguvu zote na unaona mtu anaenda kuanguka kule mbele ndani ya gari. Kuna matukio mengi kama unavyosema na hasa wananchi wa kawaida wanateseka sana wanapokuwa wanahisiwa kutenda kosa fulani hata kama ni dogo tu lakini askari ata'behave' utafikiri analipwa kwa kuwadhalilisha watu. Kwa kweli inasikitisha sana.
   
 9. Pascal Mayalla

  Pascal Mayalla JF-Expert Member

  #9
  Sep 10, 2017
  Joined: Sep 22, 2008
  Messages: 24,589
  Likes Received: 18,573
  Trophy Points: 280
  Kuna kitu nimekumbuka kuhusu bandiko hili.

  Paskali
   
 10. Pascal Mayalla

  Pascal Mayalla JF-Expert Member

  #10
  Sep 10, 2017
  Joined: Sep 22, 2008
  Messages: 24,589
  Likes Received: 18,573
  Trophy Points: 280
  Kuna kitu nimekumbuka kuhusu bandiko hili.

  Paskali
   
 11. a

  aliisaac1000 JF-Expert Member

  #11
  Sep 10, 2017
  Joined: Jul 11, 2015
  Messages: 382
  Likes Received: 199
  Trophy Points: 60
  Ni shida kubwa kwa jeshi letu la polisi bado linafanya kazi kama enzi za ujima lakini chakushangaza hicho ndio wanachokifurahia viongozi wetu. Mara nyingi jeshi letu la polisi huuwa kwa makusudi majambazi na wahalifu halafu utasikia wanatuambia eti walikua wana kimbia, ukweli ni kuwa wanawaua tena hata pale ambapo wahalifu hawana silaha. Huu ni muendelezo wa utendaji mbovu wa polisi ukishabikiwa na viongozi wa ngazi za juu. Hata magereza zetu ni nyumba za mateso huwezi kulinganisha na wenzetu wa Kenya, magereza zao ni bora sana hazina tofauti kubwa na zile za nchi zilizondelea, kwakweli jeshi letu la polisi na magereza vinahitaji mageuzi makubwa sana na silioni hilo kwakuwa viongozi tulionao wanashabikia mateso.

  Sent using Jamii Forums mobile app
   
Loading...