Hivi Polisi wa Tanzania wanafanyaje kazi zao?

Kifuna

JF-Expert Member
Aug 7, 2008
434
225
Tumewaona Polisi mala nyingi mno wakikataza na kuzuia maandamano na mikutano kwa sababu za KIINTELIJENSIA sasa! kinacho nishangaza hapo kama mmeambiwa hizo taalifa za kiintelijensia mmezipata kwa nini msiongeze ulinzi? maana maandamano ni haki ya wananchi katika nchi yoyote ile. Wananchi wanapinga jambo au kuunga mkono kwa maandamano.
Maadam kazi ya polisi ni kulinda usalama wa raia na mali zake kwa nini msilinde hivyo badala ya kuwanyima haki yao ya kikatiba?
Vitu vingine wanavyonishangaza hawa mapolisi ni kudhalilisha watu bila kufanya utafiti. Eti tumemkamata na siraha hii na ile yenye risasi kadhaa wakati vyote hivyo mtu huyo anavimiriki kiharali. Sasa! hawa jamaa wako sawa kweli kiutendaji? kumbuka watu wakichoka wataandamana tu hata wakatazwe vipi Misri ilikuwa hivihivi!
Naomba kutoa hoja
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom