Hivi Polisi wa Morogoro ingekuwa CHADEMA wanataka kuandamana Itigi ingetumika intelejensia, lori la mafuta dk 45 mmelala tu

Mimi nashauri Watanzania tuwe na desturi ya kusoma maada na kuielewa kisha ndipo tuweze kuchangia.
Mantiki ya Mtoa maada ni kwamba , toka lori lianguke zilipita takribani dakika 45 kabla ya moto kuripuka,, na katika kipindi hiki choote watu walikuwa wanaendelea kuchota mafuta, na kituo cha polisi kiko umbali wa takribani kilomita 1, je polisi walishindwa kuzingira eneo la ajari na kuwatawanya watu walioanza kujitokeza kuchota mafuta dakika za mwanzo kabisa baada ya lori kuanguka tu?

Kumbuka kazi kuu za polisi ni

1) kulinda usalama wa raia na mali zao
2) kutambua viashiria vinavyoweza kuhatarisha usalama wa raia kabla ya madhara hayajatokea
3) Kuokoa raia kwenye ajali endapo watakuwa walishindwa kubaini viashiria vilivyoisababisha ajali hiyo!

Baadhi ya watu tunajiuliza ,

kwa nini taarifa kuhusu viashiria vinavyoweza kusababisha uvunjifu wa amani kwenye mikutano ya wapinzani wa serikali huwa zinapatikana hata siku tatu kabla ya mkutano kufanyika?? ,

Je polisi wetu wamehasiwa akili wakawa makini kushughurika na wapinzani wa serikali tu na kusahau majukumu yao mengine?

Naunga mkono hoja ya mtoa maada,, kamati ya ulinzi na usalama ya mkoa wa morogoro ijitafakari!,
Kama yupo ambae HAJAKUELEWA basi anapaswa kuzikwa akiwa HAI. ASANTE SANA kwa hii Elimu uliyoitoa hapa!
 
Mfano wako hauna ulinganisho mkuu. Maandamano yanaanza na mipango lakini ajali haina mpango. Intelijensia gani inaweza kung'amua ajali itakayotokea dakika tano zijazo? Hata kama hao polisi wangekuwa pale ndani ya dk 10 wangewatawanyaje hao watu? Kwa mabomu ya machozi kwenye mto au bwawa la petrol? Huu si uzembe wa polisi ni wetu wananchi maana hakuna asieifahamu Petrol na makasheshe yake.
Wangewatawanya kwa Maji ya WashaWasha. Tangu Lori kuanguka hadi kulipuka ni zaidi ya Saa Moja, ilihitaji siku ngapi kwa maoni yako kuzuia hili?
 
PM Majaliwa kauliza,tangu ajali itokee,nani alihusika kuwazuia hawa watu wakati mita chache kuna wanausalama!!?
 
Sihitaji madaraka yoyote ya kisiasa, naweza kutoa mchango wangu wa kisiasa bila kuwa kiongozi wala mwanachama wa chama chochote cha siasa, kwani siasa bila madaraka inawezekana. Na ninapenda ufahamu kuwa mimi sio mwanachama wa cdm bali shabiki wa kutupwa wa chama hicho, hivyo usihangaike kunitafutia madaraka huko cdm. Kwaarifa yako cdm ndio chama chenye vijana wengi wanachama na washabiki kuliko chama chochote. Hiyo cdm ni kama mziki wa kizazi kipya, vijana wanavutiwa nao bila kujali ubora, maadili hata faida wazipatazo. Hao ccm ukikuta kijana kafuata nyayo za wazazi wake, fursa ama kwakuwa ni ndio chama pekee kinachoruhusiwa kufanya siasa.

Hao ccm nawafananisha na bendi kama OTTU Jazz, Sikinde nk, wana nyimbo za maadili japo ushirikina uko kwa wingi na Majungu mengi, ila kwa ajili ya raslimali muda vijana hawavutiwi nao tena. Ndio hapo sasa unapoona matumizi makubwa ya nguvu tena kwa uratibu wa vyombo vya dola ili kuwadhibiti wapinzani hasa hao cdm, kwani wazee wana uchu wa madaraka na vijana wanataka kukamata mpini.
hadithi nyingi hazina msingi
 
Maandamano yana taarifa kuwa siku fulani yatatokea ndio maana ni rahisi polisi kujiandaa ila ni lini na wapi uliwahi kuona ajali ina taarifa kuwa itatokea? Acheni kutafuta wa kumtupia lawama huku mkijiua kabisa walioathirika na tukio ndio walikuwa wazembe na wajinga kama sio wapumbavu. Unafanya mchezo na maisha yako mwenyewe kwa kutegemea polisi atakuja kukuokoa. Ni upuuzi wa hali ya juu.
Kama ni uzembe au upumbavu wa wahanga,kwa nini viongozi wanataka kuchukua hatua? Ni kwa manufaa ya nani mtu akitumbuliwa kwa sababu ya upumbavu na ujinga wa wahanga?.
Tukiweka pembeni hisia za kisiasa uchwara tunazoendekeza (hata pasipostahili),lazima tukiri kuna tatizo. Polisi wetu wanakuwa wepesi kwenye matukio ya kisiasa kuliko majanga na matukio yasiyo na harufu ta aina hiyo. Hata Jiwe anastahili lawana kwani alishasema "serikali " haijaleta tetemeko( hapa iwe ajali,moto wala ujinga/upumbavu). Unategemea ninitoka kwa mtu aliyefundishwa kutii kila kitu?
 
Ccm iko madarakani Kwa nguvu ya polisi, ccm uitumia polisi kuwalazimisha ikubaliwe na wananchi
 
Ukiwaza sana unaweza ukawapiga polisi mawe..washenzi sana.

Siamini kama polisi walizidiwa nguvu labda na wananchi, nachoamini ni uzembe mkubwa sana ulifanywa na polisi waliokuwepo eneo hilo,maana hapo msanvu tu geti la kutokea huwa wapo.

Anyway, hebu ngoja tusitiri kwanza hawa wapendwa wetu kisha tuanze kuulizana vizuri.
mkuu polisi ccm kazi yao ni kupokea maagizo kutoka juu bila agizo hawawezi chochote,laiti agizo lingetoka juu kwenda kuwatawanya watu kwenye lori ndugu zetu wangenusurika
 
Kama ni uzembe au upumbavu wa wahanga,kwa nini viongozi wanataka kuchukua hatua? Ni kwa manufaa ya nani mtu akitumbuliwa kwa sababu ya upumbavu na ujinga wa wahanga?.
Tukiweka pembeni hisia za kisiasa uchwara tunazoendekeza (hata pasipostahili),lazima tukiri kuna tatizo. Polisi wetu wanakuwa wepesi kwenye matukio ya kisiasa kuliko majanga na matukio yasiyo na harufu ta aina hiyo. Hata Jiwe anastahili lawana kwani alishasema "serikali " haijaleta tetemeko( hapa iwe ajali,moto wala ujinga/upumbavu). Unategemea ninitoka kwa mtu aliyefundishwa kutii kila kitu?

Yeye ndo chanzo cha kuleta njaa na dhiki nchini Kwa Sera zake mbovu za ujamaa za Kusomesha watu no.MTU mwenye kipato na uelewa asingesogea kwenye hatari ya kutaka kupata japo Lita Mbili za mafuta auze akapate shibe. Polisi nao wangetumia mda mwingi kuielimisha jamii madhara ya matenki ya mafuta kuliko kukimbizana na upinzani Kwa kutumiwa na wanasiasa, madhara kama hayatewezajirudia rudia tena
 
Makampuni yatengenezayo matenki ya mafuta tunaomba wakachukue technology ya mifuniko nchi za wenzetu, IPO mifuniko ambayo hata tenk libiringite vipi mifuniko haifunguki,hii uepusha hatari za kujirudia rudia kama hizi,ndani ya dk kadhaa hata Lori likianguka tayari askari washafika kuzuia watu mita 100 wasisogelee tank iliyoanguka.
 
mkuu polisi ccm kazi yao ni kupokea maagizo kutoka juu bila agizo hawawezi chochote,laiti agizo lingetoka juu kwenda kuwatawanya watu kwenye lori ndugu zetu wangenusurika

Hapo mmoja angepiga tu Simu kwamba tumeona bodaboda kama 10 zinabendera ya ACT au njooni huku chadema wamekusanyika hata dk 5 isingefika wangeshafika.Wakisikia majambazi uvuta time hatuna mafuta,wakisikia upinzani wamekusanyika kikao cha siri sekunde haipiti.
 
ungekuwa wewe polisi ingekuchukua muda gani kujua kuwa kuna roli limekula mweleka, tusitengeneze lawana zisizo na maana tukawavunja moyo askari wetu, na wangefika mapema wakaanza kukamata watu nyie haohao mgesema polisi inawabambika kesi,
Nashukuru PM kaliona... wacha iundwe tume. Maisha yana thamani sana, yasipotee bure.
1565519509995.png
 
Ujinga; Umaskini na Maradhi = Vyanzo vikuu ya majanga mengi nchini.
 
Fikra za aina yako ndio tatizo kubwa Afrika, lazima tuwe critical; tuache mambo ya "Mungu kapanga". Uchunguzi ufanyike, polisi ilijua nini na wakati gani, walichukua hatua gani?

Mbona mambo ya Chadema wanayajua sana, hata wakifanya mkutano katikati ya mapori wanaweza kufika haraka, hiyo nguvu inayotumika kudhibiti wapinzani kwanini hatuioni kwenye majanga? Juzi huko huko Morogoro wamekamata wana Chadema kwa kuingia "jimbo" ambalo sio lao, walishindwaje kujua kama kuna "bomu" limeanguka Msamvu, muda wowote linaweza kulipuka.
Vifo VS chadema
wamepata agenda
 
Back
Top Bottom