Nje ya Jimbo lake,lazima apate kibali kwa Askofu mahaliaNi baba mhashamu anaweza kusalisha kanisa lolote la Roma Tanzania.
Asante mkuu.Nje ya Jimbo lake,lazima apate kibali kwa Askofu mahalia
Japo ni kawaida na ni kama utamaduni,Kanisa la St.Petro kule O'bay kutokana na Jiografia yake na historia yake,siku za sikukuu "wakubwa" wa kanisa na "wakubwa" wa Serikali hukutana hapa.
Ila ukiwa Rais burudani Ase
Yaaani kila unachofanywa kinatangazwa
Nikiwa Rais mi nitakuwa nashinda kwenye lile paipu la kupitisha Uchafu kila weekend
Au Nitakuwa natembea kwa miguu hadi koko ili mradi niwasumbue tu
Nione wabongo watachongaje
Kwani Cathedral ni IPI?Nafahamu Kadinali Pengo ni askofu wa Jmbo Kuu la Dar es Salaam ambapo makanisa ya St Peter's na St. Joseph yako ndani ya jimbo hilo lakini napenda kujua je Pengo Kanisa lake la nyumbani ni lipi?
Cathedral ni IPI kati ya St. Peter's na St.Joseph?Ni baba mhashamu anaweza kusalisha kanisa lolote la Roma Tanzania.
nakumbuka wakati sista wangu yupo aekondari darasa moja na akina simon msuva..kuna kijana ana mwanya mkubwaa kama jino limeng'oka bt halioti tena..tangu form one wanamtania wanamwita kardinali pengo...
Sexer sio kweli nini?Umeelewa nilichoandika?Kuna sehemu nimekataa kuwa JPM hakuwa anasali pale kabla?sio kweli wanakutana tu pale kwenye sikukuu bali mtu anasali pale sababu ndo kanisa lake. mfano magufuli anasali pale kabla hata ya urais na ni mwanajumuiya wa pale. nadhani hakuona haja ya kuhamia kanisa jirani kwa sasa la st joseph
Kanisa Kuu au Kanisa la Kiaskofu au Cathedral ni pale St.Joseph. kinacholipa hadhi ya ukuu ni kile kiti maalum i.e cathedral kilichosimikwa pale.Nafahamu Kadinali Pengo ni askofu wa Jmbo Kuu la Dar es Salaam ambapo makanisa ya St Peter's na St. Joseph yako ndani ya jimbo hilo lakini napenda kujua je Pengo Kanisa lake la nyumbani ni lipi?
Mkuu ninachojua ni kuwa wakati wa sikukuu kuu za kanisa hususani sikukuu kubwa katika kanisa kama pasaka ni lazima askofu mkuu asali katika kanisa kuu la jimbo na kukalia kiti cha kiaskofu.Na kwa taratibu za kanisa askofu mkuu anasali ile misa kuu na kwa jimbo la dar es salaam misa kuu ni ile ya saa nne katika la st joseph ambapo askofu mkuu wa jimbo analazimika kusali katika himaya yake.Kila jimbo ni lazima liwe na kanisa kuu yaani "Cathedral" au "Kanisa la Kiaskofu"
Kwa Dsm Kanisa la Kiaskofu ni pale "St Joseph".
Lakini sababu Pengo ndio Askofu Mkuu wa Dsm,basi ana mamlaka ya kusali popote anapoona inafaaa.
Japo ni kawaida na ni kama utamaduni,Kanisa la St.Petro kule O'bay kutokana na Jiografia yake na historia yake,siku za sikukuu "wakubwa" wa kanisa na "wakubwa" wa Serikali hukutana hapa.
Enzi za Mwalimu,alikuwa na kiti chake maalumu kisichokaliwa akiwa hayupo,na alikuwa misa ya asubuhi na Jpli lazima afike akiwepo Dsm.Mkapa alipenda sana Paroki ya Bikira Maria Imakulata-Upanga,Pinda pale Parokia ya Hananasifu-Kinondoni,maarufu kama "Kwa Pinda"
Siyo kweli, in mpaka apate ruhusa ya askofu wa jimbo husika.Ni baba mhashamu anaweza kusalisha kanisa lolote la Roma Tanzania.