Hivi Open University of Tanzania Wameshatoa Majina Ya Wale Waliomba Lozi Moja Kwa Shahada ya Kwanza!

Online Pastor

JF-Expert Member
Sep 7, 2017
1,949
2,000
WakuNingependa kujuwa kama Chuo Huria nao wameshatoa majina kwa wale waliomba shahada ya kwanza!?
 
zigi 01

JF-Expert Member
Oct 22, 2017
234
225
hivi utaratibu wa Ada ukoje kwa open university? na usomaji wake ukoje kwa anaesoma IT ?
 
hmtk

Senior Member
May 24, 2013
154
225
FOUNDATION ROGRAMME CHUO KIKUU HURIA CHA TANZANIA

Tunapenda kuutangazia Umma kuwa, bado tunaendelea kupokea Maombi ya kujiunga na Foundation Programme mpaka tarehe 26/09/2018. FOUNDATION PROGRAME imepewa ithibati na TCU kwa lengo la kuwaongezea sifa wahitimu wa Form Six na Diploma waliopungukiwa sifa za kujiunga na Bachelor degrees. Wakihitimu na kufuzu vizuri watapata sifa ya kujiunga na degree kwenye vyuo mbalimbali nchini na hata nje ya nchi. Programme hii husomwa kwa mwaka mmoja wa masomo na inatolewa na Chuo Kikuu Huria tu nchi nzima. Programme hii ipo katika makundi matatu ya Foundation Arts, Science na Business Studies na mwanafunzi atachagua mkondo unaomuhusu mara masomo yatakapoanza.

Sifa za kujiunga ni:

(a) Muhitimu wa Kidato cha Sita mwenye ufaulu wa angalau pointi 3.5 mpaka1.5 katika masomo mawili. Hii ni sawa na kusema kuwa wahitimu wote waliopata kuanzia DIV 3 ya pointi 14 na kuendelea wanaweza kujiunga ikiwa tu wana E na S katika masomo mawili.

(b) Muhitimu wa Diploma mwenye ufaulu wa GPA ya 2.9-2.0

(c) Muhitimu wa NTA level 5

Tunasisitiza kuwa maombi yanapokelewa bure katika matawi yetu yaliyopo katika mikoa yote ya Tanzania Bara na katika Visiwa vya Unguja na Pemba. Pia, unaweza kutuma maombi moja kwa moja kupitia www.out.ac.tz

Kwa wale ambao tayari wameshatuma maombi yao wasitume tena bali wasubiri orodha ya waliochaguliwa ambayo itakuwa inatolewa kwa awamu. Tunawaomba watulie wavute subira majina yatatolewa mapema tu taratibu zote za udahili zitakapokamilika.

Pamoja na kupokea maombi ya Foundation Programme pia tunapokea maombi kwenye ngazi za Certificates, Diploma, Bachelor Degrees, Master Degrees na PhD bure. Leta maombi yako sasa usisubiri kesho.

Kwa moyo mkunjufu kabisa tunakuomba ukiupata ujumbe huu tusaidie kuusambaza kwa wingi kadri utakavyoweza ili wadau mbalimbali waendelee kupata taarifa hii. Asante sana.

Kwa mawasiliano zaidi unaweza kutupigia kupitia nambari 0719017254

Imetolewa na:
Dkt. Mohamed Omary Maguo
Mkurugenzi wa Mawasiliano na Masoko
Chuo Kikuu Huria cha Tanzania
06/09/2018
Dar es Salaam.
 
debbug

JF-Expert Member
Jun 9, 2018
400
1,000
hivi utaratibu wa Ada ukoje kwa open university? na usomaji wake ukoje kwa anaesoma IT ?
karibu San kiongozi Mimi ni miongon mwa wanafunzi wanaosoma bachelor of science in ICT apa open.Kuhusu ada unalipa kwa unit mfano java programming language ina unit tatu kwa mwaka na kila unit ni tsh 90000 so kama tatu apo uatazidisha mala 90000 kwaiyo utapiga masomo kwa mwaka ni mangap na jumla unit kwa masomo yote ni ngap so utazidisha mala 90000
 
KIXI

Member
Mar 3, 2015
44
95

Utaratibu ukoje wa kusoma ni full time au kuna part time?
 
zigi 01

JF-Expert Member
Oct 22, 2017
234
225
Hallo kiongozi
karibu San kiongozi Mimi ni miongon mwa wanafunzi wanaosoma bachelor of science in ICT apa open.Kuhusu ada unalipa kwa unit mfano java programming language ina unit tatu kwa mwaka na kila unit ni tsh 90000 so kama tatu apo uatazidisha mala 90000 kwaiyo utapiga masomo kwa mwaka ni mangap na jumla unit kwa masomo yote ni ngap so utazidisha mala 90000
 
Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom