Mwanaoshimba
Member
- Mar 8, 2017
- 61
- 82
Kwa sasa ofisi, idara na taasisi nyingi za serikali zikiwemo ofisi za wakuu wa mikoa na halmashauri za wilaya, majiji na manispaa zina maafisa uhusiano, maafisa mawasiliano au kama wengine wanavyowaita maafisa habari.
Nimetafakari sana juu ya ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Dsm, inakuwaje muda mwingi Mkuu anafanya shughuli za habari mwenyewe kama vile kwenda studio na kupoteza muda mwingi akihariri vipindi vyake kama ambavyo tumemsikia akisema? Mfano alisema kuwa alikuwa akienda mara kwa mara Clouds kwenda kuhariri vipindi vyake. Kwa nini hizo kazi asifanye Afisa Uhusiano au Mawasiliano wa Mkoa?
Au Dsm hawana Afisa huyo?