Hivi Obama ana msimamo thabiti na dhamira yake? Hebu jadili hili: | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Hivi Obama ana msimamo thabiti na dhamira yake? Hebu jadili hili:

Discussion in 'International Forum' started by trachomatis, Jan 25, 2012.

 1. trachomatis

  trachomatis JF-Expert Member

  #1
  Jan 25, 2012
  Joined: Jun 7, 2011
  Messages: 3,653
  Likes Received: 93
  Trophy Points: 145
  Kwenye State of Union address yake ametilia mkazo kwamba hatakubali Tehran wafanikishe mipango yao ya Nyuklia.. Na atafanya kila jitihada itakayowezekana kuhakikisha Iran wanashindwa kutekeleza mpango huo...

  Akasema kuwa atakuwa upande wa Taifa la Israel wakati wote na watalisaidia Taifa hilo inapobidi ili kudumisha ushirikiano wa muda mrefu wa nchi hizo mbili...

  Sasa kumbukeni aliahidi kulifunga gereza la Guantanamo,na ameshindwa kufanya hilo hadi leo,na si kushindwa tu,hatalifunga,na halitafungwa kamwe..!
  Hii ni kutokana na shinikizo la sheria mpya aliyoisaini,tena kwa shingo upande,hili ni kwa mujibu wa hotuba yake mwenyewe,kwamba amesaini kwa sababu amelazimika na si kutokana na utashi wake.

  Na sheria hiyo ni mbaya sana hata kwa Wamarekani wenyewe kwa maana inaruhusu mtu/watu kukamatwa na kuwekwa kizuizini huko Guantanamo,bila ya ushahidi wa kutosha,na bila hata ya kutegemea kufunguliwa mashitaka!
   
 2. Yegomasika

  Yegomasika JF-Expert Member

  #2
  Jan 25, 2012
  Joined: Mar 21, 2009
  Messages: 7,125
  Likes Received: 23,734
  Trophy Points: 280
  Tofautisha kati ya suala la Iran na kufungwa kwa gereza la Guantanamo, ukiweza kuona tofauti ya hivyo vitu viwili utaijua dhamira yake.
   
 3. trachomatis

  trachomatis JF-Expert Member

  #3
  Jan 25, 2012
  Joined: Jun 7, 2011
  Messages: 3,653
  Likes Received: 93
  Trophy Points: 145
  Sawa ni mtazamo tu..
  Na nje wale tunaowaita OWS walikuwa na hotuba yao ya kupinga address ya Obama.. They are the 99%.... Hotuba yao waliisoma kama imla... Na kwamba wao wanapigania mapinduzi..
   
 4. trachomatis

  trachomatis JF-Expert Member

  #4
  Jan 25, 2012
  Joined: Jun 7, 2011
  Messages: 3,653
  Likes Received: 93
  Trophy Points: 145
  Yaani pengine baadhi yetu tulikuwa na mtazamo tofauti na Barack... Je mmeona fulana za maveterani wa vita ya Iraq? Nao wamejiunga kwenye maandamano ya OWS! Na wanasema,they were fighting for their country some years back,but now they have come to know their real enemy..
   
 5. trachomatis

  trachomatis JF-Expert Member

  #5
  Jan 25, 2012
  Joined: Jun 7, 2011
  Messages: 3,653
  Likes Received: 93
  Trophy Points: 145
  And yet they add kwamba,hotuba walizopatiwa wakati wanaenda vitani nchi tofauti duniani ni kwamba wanaenda kukomboa wananchi wanaoonewa na kunyimwa uhuru ndani ya nchi yao..
  Sasa wanashangaa yale yaliyoifanya nchi yao ikapigane kwenye mataifa mengine yanafanyika kwenye nchi yao,, wanashangaa hiyo ni demokrasia gani na ni uhuru gani!...
  Hata hivyo Barack amewaignore...
   
 6. Michelle

  Michelle JF-Expert Member

  #6
  Jan 25, 2012
  Joined: Nov 16, 2010
  Messages: 7,364
  Likes Received: 194
  Trophy Points: 160
  American Interests has a four-fold purpose, to increase knowledge of, highlight threats to, explore opportunites for and above all, serve as platform of advocacy for the continuance and preservation of global American dominance because, as was stated well before me, "America must remain strong".

  Siku zote viongozi wakuu wa Marekani wanachagua lile lililo la maslahi kwa taifa lao na linalohakikisha wanaendelea kutawala dunia....Obama kama Obama aweza kuwa na dhamira tofauti na matendo yake,lakini kama Rais wa Marekani lazima alinde interest za wamarekani....Tukikumbuka Obama kipindi cha kampeni,alivyopokelewa Berlin na hadi kupewa Tuzo ya Nobel Peace kwa kuhubiri amani,wengi wetu tunashindwa kuamini ndo huyu wa sasa.....kwa gharama yeyote lazima ahakikishe Marekani inabaki kuwa taifa lenye nguvu zaidi duniani hata kama dhamira yake inamsuta....!
   
 7. trachomatis

  trachomatis JF-Expert Member

  #7
  Jan 26, 2012
  Joined: Jun 7, 2011
  Messages: 3,653
  Likes Received: 93
  Trophy Points: 145
  Nakuelewa vizuri Michelle.. Maana si kila mtu anapata jibu la kuridhisha kulingana na maswali yake.,aliyouliza.
   
 8. Michelle

  Michelle JF-Expert Member

  #8
  Jan 26, 2012
  Joined: Nov 16, 2010
  Messages: 7,364
  Likes Received: 194
  Trophy Points: 160
  Pole kama sijakujibu, hao wanaodai mapinduzi,sina hakika kwamba kweli walikwenda nchi kama Iraq wakijua kwamba Sadam Hussein alikuwa na silaha za maangamizi si kuwa serikali yao ilikuwa na maslahi ya kiuchumi zaidi....siwezi kuelewa kwanini hadi sasa huko Syria watu wanakufa hivyo wanajeshi wa Marekani hawajatumwa kusaidia wanaoonewa.....Kama viongozi wa Marekani wanawadanganya wanajeshi wake basi hiyo itakuwa mpya....binafsi naamini wanajuaga kinachowapeleka na hili hata Donald Trump analiweka wazi.....!
   
 9. Chamoto

  Chamoto JF-Expert Member

  #9
  Jan 26, 2012
  Joined: Dec 7, 2007
  Messages: 2,078
  Likes Received: 1,115
  Trophy Points: 280
  Na huo ndiyo ukweli mengine yote ni siasa.
   
 10. K

  KIM KARDASH JF-Expert Member

  #10
  Jan 26, 2012
  Joined: Sep 21, 2011
  Messages: 5,083
  Likes Received: 60
  Trophy Points: 145
  Obama is a food stamp president,hana jipya..amalize miaka yake mitano arudi kwao hawaii.
   
 11. trachomatis

  trachomatis JF-Expert Member

  #11
  Jan 26, 2012
  Joined: Jun 7, 2011
  Messages: 3,653
  Likes Received: 93
  Trophy Points: 145
  Michelle nimekuelewa vizuri sana...
  Na you have answered all the asked and unasked questions kwa kweli.. Thanks a lot.. Ila Occupy Wall Street nadhani will haunt him for a while..
   
 12. trachomatis

  trachomatis JF-Expert Member

  #12
  Jan 26, 2012
  Joined: Jun 7, 2011
  Messages: 3,653
  Likes Received: 93
  Trophy Points: 145
  Nimekuelewa vizuri sana Michelle..
  Na umenitajia Syria,ndiyo kabisa..Hebu tazama nchi kama Yemen kwa mfano,na linganisha na Syria..
  Kifupi nimekupata.. Ila mifumo yake hiyo inawafanya wawe ama wajiundie maadui ndani na nje.. No wonder hizo 4 folds..
   
 13. trachomatis

  trachomatis JF-Expert Member

  #13
  Jan 26, 2012
  Joined: Jun 7, 2011
  Messages: 3,653
  Likes Received: 93
  Trophy Points: 145
  Wajua ni kama vile hakukidhi matazamio ya wengi...
  Yaani amepiga about turn ya ajabu...
   
Loading...