Hivi nyie watu wa Dar mnaishije na hali hii ya joto?

Habarini
Nilikuja kutoa matongotongo kidogo Dar na leo ninapoandika ujumbe huu natoka Kariakoo narudi zangu huko ambako hasa ndio tunazalisha chakula.
Nimefika Kariakoo nikasema ngoja nitafute chochote cha kuwabebea watoto,lahaulaaa la kwata!!, Nimeshindwa kuendelea kuzunguka njia zimejaa watu hata kutembea na mafua yatatuacha kweli?
Lakini mbaya zaidi joto ni kali sana,suruali inaloa,shati nililovaa limelowana na jasho.
Je hali hii ni ya kawaida kwenu mnaokaa hapa mjini? Kwetu mwaka huu kuna joto ila si kama huku.
Poleni sana watu wa Dar,je mnahimili vipi hali hii,na wanaokula matunda kwa masihara wanafanyeje kwenye hali hii kama mfuko umelegea kwenda kwenye nyumba zenye viyoyozi?
Ila nimegundua pia wasichana wa Dar machi juu sana ndio maana hata ule uzi wa Riki boy unapata umaarufu
Povu ruksa maana nimesweti sana
We Rudi kwenu subiri tuwaletee maiti mzike maana hata hela ya kuja msibani tukiamua kuzika huku mjini huwa hamna kitu.

Kalime mahindi ule sisi tuache na mji wetu ukiona joto unawasha AC maisha yanaendelea.

Cha muhimu umepata Cha kuwasimulia wa mkoani wenzio kasubiri tukija tiwanunulie bia maana huwa mnasubiri tuje tuwaachie viatu, mashati begi nk.
 
Hahaaaa
 
Habarini

Nilikuja kutoa matongotongo kidogo Dar na leo ninapoandika ujumbe huu natoka Kariakoo narudi zangu huko ambako hasa ndio tunazalisha chakula.

Nimefika Kariakoo nikasema ngoja nitafute chochote cha kuwabebea watoto,lahaulaaa la kwata!!, Nimeshindwa kuendelea kuzunguka njia zimejaa watu hata kutembea na mafua yatatuacha kweli?

Lakini mbaya zaidi joto ni kali sana, suruali inaloa, shati nililovaa limelowana na jasho.

Je hali hii ni ya kawaida kwenu mnaokaa hapa mjini? Kwetu mwaka huu kuna joto ila si kama huku.

Poleni sana watu wa Dar, je mnahimili vipi hali hii, na wanaokula matunda kwa masihara wanafanyeje kwenye hali hii kama mfuko umelegea kwenda kwenye nyumba zenye viyoyozi?

Ila nimegundua pia wasichana wa Dar machi juu sana ndio maana hata ule uzi wa Riki boy unapata umaarufu

Povu ruksa maana nimesweti sana
Wewe ni muumini wa uzi afadhali umetufahamisha tabia yako
 
Sisi "tunaopiga mihuri" ndio tunapata shida, kupanda daladala na mwendokasi na hili joto sio poa. Wenzetu wanatembea huku wamekaa kwenye AC hawana shida na mtu.
 
Back
Top Bottom