davetz28
JF-Expert Member
- Dec 17, 2017
- 543
- 617
Habarini
Nilikuja kutoa matongotongo kidogo Dar na leo ninapoandika ujumbe huu natoka Kariakoo narudi zangu huko ambako hasa ndio tunazalisha chakula.
Nimefika Kariakoo nikasema ngoja nitafute chochote cha kuwabebea watoto,lahaulaaa la kwata!!, Nimeshindwa kuendelea kuzunguka njia zimejaa watu hata kutembea na mafua yatatuacha kweli?
Lakini mbaya zaidi joto ni kali sana, suruali inaloa, shati nililovaa limelowana na jasho.
Je hali hii ni ya kawaida kwenu mnaokaa hapa mjini? Kwetu mwaka huu kuna joto ila si kama huku.
Poleni sana watu wa Dar, je mnahimili vipi hali hii, na wanaokula matunda kwa masihara wanafanyeje kwenye hali hii kama mfuko umelegea kwenda kwenye nyumba zenye viyoyozi?
Ila nimegundua pia wasichana wa Dar machi juu sana ndio maana hata ule uzi wa Riki boy unapata umaarufu
Povu ruksa maana nimesweti sana