Hivi nyie kina Dada/ Mama mnajua mna matumizi mabaya sana ya Pesa zetu?

CONTROLA

JF-Expert Member
Sep 15, 2019
6,939
22,981
Nipo katika mahusiano huu ni mwaka wa 9 niko na mpenzi m1 ninayemhudumia kila kitu, lakini katika huduma ninazompa kuna huduma 1 ambayo nimemtamkia live bila kupepesa macho kuwa ifikapo tar 1 Jan 2021 kama tutajaliwa uhai itakua mwisho wangu wa kutoa; pesa ya yeye kwenda kusuka. Nitatoa pesa ya mahitaji mengine ila si inayohusisha nywele.

Ni mwisho mimi kutoa pesa za kwenda saloon. KUITA msusi aje amsuke, na huduma zngne.nk. Kuna kipindi niliambiwa ninunue mafuta fulani ni bei sana yanauzwa kama 80k hivi, nilishangaa sana nikamuuliza kwanini hela yote hyo? Akaniambia kuwa haya mafuta yanasaidia nywele zisikatike, nikajisemea moyoni (sawa ni vzuri na mimi mpenzi wangu awe na nywele refu) nikanunua.

Lakini tangu kipindi hicho hadi leo zile nywele zipo shingoni tu, miaka na miaka nywele imeganda pale pale shingoni haiji huku mgongoni ifike kiunoni. Nimejitahidi sana kuhudumia hizi nywele ila naona huu upotezaji hela "imetosha sasa" 2021 naenda kuanza maisha mapya na mimi asee.

Nina uhakika ningekua siendi saloon kunyoa nywele zangu zingekua huku miguuni na sizifanyii kitu chochote zaidi ya mafuta na spray tu, ila haiwezekani huyu mwenzangu yeye nywele anazipaka kila kitu ila bado zipo pale pale na katika historia yake anadai nywele kaanza zifuga tangu Chuo.

Sasa hizi nywele za wanawake wa Tz ni kwamba zinadumazwa na hili jua au nyie kina dada hizo nywele zimekuaje, mbona hazikui/haziongezeki? Ktk kauchunguzi kangu ka chini chini nimegundua.

Si huyu mpenzi wangu tu, ila ni wanawake almost 85% na kama yupo wa kuni-prove wrong leo atokee mdada/mmama humu JF mwenye nywele imefika kiunoni natoa 100k (100,000) kwake.

Huu ujanja wenu mimi nimeushtukia. Mkinyimwa hela za saloon mnanuna sana nyie, tena mnavimba ila nawaambia kwamba hamna mtu yupo tayari kumwagilia mti usiotoa matunda, mbolea kila siku.

Msimu wa matunda yanatoka maua tu ila hamna cha embe wala papai, asee maua hayaliwi na kwakua siwezi kuukata huu mti basi hata kumwagilia na kuweka mbolea siweki tena nimechoka eti.

Mbona Rasta zinakua? Marasta man anasokota dread leo ukimtafuta mwakani Dread ipo mogongoni zote ni nywele kama hizo zenu ila kwann zenu zikifika shingoni zinagoma kuendelea? Eti jana akawa ananipanga ananiambia "baby kwani huoni zimejaa?" Nikamwambia mimi sitaki zijae nataka kitu kirefuke, eboooo!

images.jpg
 
We mhudumie tu kusuka, lakini usitegemee mafuta ya elfu 80 ndo yatakuza nywele hizo ni biashara tu wanatangaza.

Nywele ni asili ya mtu. Mwingine haeki chochote na zinakua.

Hyo laki yako iandae kuna watu wana nywele hadi huko kiunoni unapopasemea, tembea uone
 
Mkuu miaka 9 mnatafuta pHd?

Turudi kwenye point nywele za Kiafrika zinahitaji chakula Bora matunda na maji ya kunywa kwa wingi ili zijae sio zirefuke zifike mgongoni. Hao wenzetu sio wote pia wanazo, hiyo elf 80 bora angenunua nywele za kufanana na zake akitaka zionekane ndefu anashonea kwa nyuma, alaf nywele za Kibongo ukisuka na kupeleka saloon Mara kwa mara hazikui.

Kwani hana kazi mpenzi wako huyo? Mpe matumizi ya jumla ya mwezi mambo ya nataka kwenda salauni, ndo unatoa hela itakula kwako.
 
We mhudumie tu kusuka,lakini usitegemee mafuta ya elfu 80 ndo yatakuza nywele hizo ni biashara tu wanatangaza

Nywele ni asili ya mtu. mwingine haeki chochote na zinakua.

Hyo laki yako iandae kuna watu wana nywele hadi huko kiunoni unapopasemea, tembea uone
Najua wapo tena wengi tu
 
Wapo ambao Anatumia Mafuta ya Nazi lakini nyewe hioo.

Kuna wengine tuu wana nyota ya kipara kama sio kipilipili.
Halafu wengi Ma complicator ndio Haziwapendi.
Basi Bongo wengi wana asili ya vipilipili.
 
Mkuu miaka 9 mnatafuta pHd?

Turudi kwenye point nywele za kiafrika zinahitaji chakula Bora matunda na maji ya kunywa kwa wingi ili zijae sio zirefuke zifike mgongoni,hao wenzetu sio wote pia wanazo,hiyo elf 80 bora angenunua nywele za kufanana na zake akitaka zionekane ndefu anashonea kwa nyuma,alaf nywele za kibongo ukisuka na kupeleka saloon Mara kwa mara hazikui.

Kwani hana kazi mpenz wako huyo?Mpe matumizi ya jumla ya mwezi mambo ya nataka kwenda salauni,ndo unatoa hela itakula kwako.
Miaka 9 yawezekana vizuri tu mkuu.

Kumpa matumizi ya jumla ya mwezi ni sawa na kumpa

mtoto wako pocket money ya terms zote ajiwekee mwenyewe.
 
Shida yako Ni nywele zikue! Au gharama?
Eleweka braza
Hawa wanawake ukiwaendekeza makampuni ylutakua unayasikia tuu kwa wengine.
 
Back
Top Bottom