Hivi Nyerere, Mwinyi na Mkapa walifanya ziara kuaga nchi wahisani?

Salary Slip

JF-Expert Member
Apr 3, 2012
47,013
144,371
Hili ni swali ninalojiuliza hasa ukizingatia nchi yetu hii ni ombaomba.

Utaratibu huu inawezekana unafanywa na viongozi wa mataifa makubwa lakini sisi nchi masikini tunapaswa kuiga kila kitu hata kama uchumi wetu hauruhusu?

Je,haiwezekani raisi akatoa hotuba maalumu ya kuaga na kuzishukuru nchi wahisani na katika hotuba hiyo nchi hizo zote zikaorodheshwa na kisha hotuba hiyo ikasambazwa katika balozi zote za nchi wahisani/marafiki zilizopo hapa nchini?

Jamani twendeni na hali halisi ya uchumi wa nchi yetu na si kuiga kila kitu.

Kama ni kuiga,mbona basi hatuthubutu kuiga kwenda mwezini?

Kwakweli raisi wa nchi hii ana madaraka ya kupitiliza na bahati mbaya hakuna wa kumuhoji na hili ndio tatizo kubwa.Inasikitisha.
 
Nakumbuka Mwl. Nyerere aliaga mikoani, Unguja, Pemba, na nchi zilizokuwa mstari wa mbele - SADC sasa isipokuwa Afrika Kusini.
 
Huu utaratibu haufai kabisa kwa nchi hizi ombaomba na ni bora tukaachana nao.
 
Mkapa alikuja huku mwishoni mwishoni .. akatumia nafasi hiyo kuaga (ila sijui kama ilikuwa ziara mahsusi ya kuaga). Hao wengine sina uhakika
 
JK alianza kujitambulisha. Alizunguka mno. Sasa anamaliza kama alivyoanza kwa kuaga.
Kila mualiko kwake ni sababu tosha. Haikutosha kuwaaga mabalozi mwaka mpya!
Record yake ya kusafiri itadumu miaka 1000 ijayo!
 
Anashukuru nini wakati deni la taifa ni trilioni 40 na alikuta likiwa trilioni tisa! Hao jamaa ni walimhisani au kumkopesha? Au kuna fedha yeye na Salma Kikwete walikuwa wanafadhiliwa bila sisi kujua? Hivi ukienda bank kukopa hela na ukapata, utaita hiyo bank ni mhisani wako? Huyu jamaa amekuwa akikopa miaka yote ya uongozi wake na hakuna alichozalisha. Nashangaa hajafanya ziara kuwashukuru wazabuni na wakandarasi wa ndani aliowakopa hadi wengine wamefilisika
 
mswahili hafai nafasi zaidi ya mjumbe wa kitongoji au balozi wa nyumba ten ten sisi tukampa hadi urais tumekoma
 
Huyo jamaa ni kama vile alijiwekea nadhiri moyoni mwake kuwa akiingia madarakani avunje rekodi ya kusafiri nje ya nchi, kuwapita viongozi wenzake wote waliomtangulia

Hata hivyo rekodi hiyo ameiongeza kwa kuwa kiongozi pekee aliyesafiri nje ya nchi yake mara nyingi kuliko kiongozi yeyote duniani kwa nyakati hizi!
 
Kwani anashindwa kuwaita mabalozi wa hizo nchi na kuwaaga kwa niaba hapo magogoni?
 
Huyo jamaa ni kama vile alijiwekea nadhiri moyoni mwake kuwa akiingia madarakani avunje rekodi ya kusafiri nje ya nchi, kuwapita viongozi wenzake wote waliomtangulia

Hata hivyo rekodi hiyo ameiongeza kwa kuwa kiongozi pekee aliyesafiri nje ya nchi yake mara nyingi kuliko kiongozi yeyote duniani kwa nyakati hizi!

aisee !
 
Hili ni swali ninalojiuliza hasa ukizingatia nchi yetu hii ni ombaomba.

Utaratibu huu inawezekana unafanywa na viongozi wa mataifa makubwa lakini sisi nchi masikini tunapaswa kuiga kila kitu hata kama uchumi wetu hauruhusu?

Je,haiwezekani raisi akatoa hotuba maalumu ya kuaga na kuzishukuru nchi wahisani na katika hotuba hiyo nchi hizo zote zikaorodheshwa na kisha hotuba hiyo ikasambazwa katika balozi zote za nchi wahisani/marafiki zilizopo hapa nchini?

Jamani twendeni na hali halisi ya uchumi wa nchi yetu na si kuiga kila kitu.

Kama ni kuiga,mbona basi hatuthubutu kuiga kwenda mwezini?

Kwakweli raisi wa nchi hii ana madaraka ya kupitiliza na bahati mbaya hakuna wa kumuhoji na hili ndio tatizo kubwa.Inasikitisha.
Unajuaje mkuu?? huenda JWTZ washafanya secret mission za kwenda huko!
 
Anashukuru nini wakati deni la taifa ni trilioni 40 na alikuta likiwa trilioni tisa! Hao jamaa ni walimhisani au kumkopesha? Au kuna fedha yeye na Salma Kikwete walikuwa wanafadhiliwa bila sisi kujua? Hivi ukienda bank kukopa hela na ukapata, utaita hiyo bank ni mhisani wako? Huyu jamaa amekuwa akikopa miaka yote ya uongozi wake na hakuna alichozalisha. Nashangaa hajafanya ziara kuwashukuru wazabuni na wakandarasi wa ndani aliowakopa hadi wengine wamefilisika

Mkuu umeeleza vizuri sana, in fact huyu jamaa sijui huwa anafikiri nini. Thi is as bad as it gets
 
Huyo jamaa ni kama vile alijiwekea nadhiri moyoni mwake kuwa akiingia madarakani avunje rekodi ya kusafiri nje ya nchi, kuwapita viongozi wenzake wote waliomtangulia

Hata hivyo rekodi hiyo ameiongeza kwa kuwa kiongozi pekee aliyesafiri nje ya nchi yake mara nyingi kuliko kiongozi yeyote duniani kwa nyakati hizi!

Hana uchungu na hii nchi ndio maana hajali.
 
Back
Top Bottom