Hivi Nyerere aliwezaje kukabiliana na mataifa ya magharibi na Marekani? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Hivi Nyerere aliwezaje kukabiliana na mataifa ya magharibi na Marekani?

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by LINCOLINMTZA, Sep 19, 2011.

 1. LINCOLINMTZA

  LINCOLINMTZA JF-Expert Member

  #1
  Sep 19, 2011
  Joined: Mar 15, 2011
  Messages: 1,640
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 0
  Dungu wanaJF,
  Nimekuwa nikiwaza jinsi haya mataifa makubwa ya ulaya na Marekani yanavyoendesha siasa zake katika dunia hii.
  Mataifa haya yanatumia njia mbalimbali ili kuweza kujipatia rasimali na nguvu za kiutawala kutoka mataifa mengine kwa njia mbalimbali kama za kijasusi au za kawaida. Na ninavyojua mimi, taifa kama Marekani limekuwa na nguvu na ujuzi mzuri sana wa kufanya kazi hiyo tangia karne ya 19 hadi sasa.

  Baba wa Taifa, Mwl. J.K. Nyerere alikabiliana nao katika uongozi wake wote bila kuyumba na hasa ikizigantiwa kwamba kipindi chake hakukuwa na maendeleo ya mawasiliano kama sasa ambapo kwa sasa unaweza pata hata siri za Marekani kupitia WikiLeaks,na kwingineko
  Swali, Je ni njia gani mwalimu alitumia, kwanza kuwaelewa hawa watu na pili kukabiliana nao kwa wakati huo wote?
  Hii itasaidia vijana wetu wanojiandaa kuwa viongozi kuweza kuona mbinu hizo mapema kwani waliowengi hawana expose ya mambo kama hayo.

  Naomba kuwakilisha wanaJF kwa heshima na utiifu.
   
 2. T

  Topical JF-Expert Member

  #2
  Sep 19, 2011
  Joined: Dec 3, 2010
  Messages: 5,176
  Likes Received: 11
  Trophy Points: 0
  Alikuwa mnafiki wa kutupwa..ndio maana ali survive

  Makaburu walikuwa wana chimba madini huku anajidai hawapendi..
   
 3. M

  Mbopo JF-Expert Member

  #3
  Sep 19, 2011
  Joined: Jan 29, 2008
  Messages: 2,532
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 0
  Unawachukiza wale wanaodhani kwamba awamu yake ya uongozi ilikuwa faultless. Kwa kujua kwamba uongozi ni changamoto, basi hata awamu yake ilikuwa na mazuri na mabaya yake na hili hata yeye mwenyewe amewahi kukiri hadharani.
   
 4. Makindi N

  Makindi N JF-Expert Member

  #4
  Sep 19, 2011
  Joined: Mar 14, 2008
  Messages: 1,068
  Likes Received: 12
  Trophy Points: 135
  Nyerere alikua mzalendo wa kweli hawa wa leo hakuna kitu! He practiced what he preached....... Tatizo uongozi wake haukuandaa viongozi wa sasa km yy.....
   
 5. T

  Topical JF-Expert Member

  #5
  Sep 19, 2011
  Joined: Dec 3, 2010
  Messages: 5,176
  Likes Received: 11
  Trophy Points: 0
  Mfano?
   
 6. Jethro

  Jethro JF-Expert Member

  #6
  Sep 19, 2011
  Joined: Mar 23, 2009
  Messages: 2,223
  Likes Received: 98
  Trophy Points: 145
  Kwa hili najua Nyerere alikuwa mzalendo ingawa naye alikuwa na mapungufu yake esp kwenye mitazama ya kiitikadi ingawa alikuwa anataka mazuri kwa wananchi wake,

  Alikuwa na uwezo wa kujenga Hoja kwa hao watu wa magharibi hakuwa mrafi kama hawa viongozi wetu na ndio maana alikuwa anachukia sana wala rushwa alipenda tujitegemee sisi wenyewe taratibu mpaka tufike ila alipo toka tu viongzi hawa walipo pewa nchi nadhani kazi yao ya kwanza walipo sikia anaumwa ndipo wakamalizia kabisa kwanini nasema hayo tukijiuliza tu kwa mara ya kwanza nyerere ameenda tibiwa na kufia huko huko haiiji akilini na baada ya hapo viongozi wetu wakauza kila kitu na kurudisha wazungu kuja kuwekeza kumbuka Nyerere aliyapinga hayo yote ya kurudi hawa kuwekeza kwani alijua fika tutazurumiwa tuu hatukuwa na hatuna viongozi makini wenye kujenga hoja na kutetea rasilimali zetu.

  Mfano mzuri tu huko Musoma kuna watu wananchimba madini kimya kimya Mkono anauliza serikali hao wachimbaji wamekujakuja vipi je ni buhemba nyingine ???madhara yake ndio hayo ya viongozi legelege kutokujua kujenga hoja kuna wasumbua ni uroho wa kuhongwa maana wazungu kwa rushwa ni namba mmoja
   
 7. Makindi N

  Makindi N JF-Expert Member

  #7
  Sep 19, 2011
  Joined: Mar 14, 2008
  Messages: 1,068
  Likes Received: 12
  Trophy Points: 135
  Mfano wa nn? Uzalendo wake? Viongozi wa leo ambao hakuna kitu? Wat practised as he preached? Viongozi tulionao ambao hawakuandaliwa vizuri au ni mfano gano unaotaka?
   
 8. Mr.Toyo

  Mr.Toyo JF-Expert Member

  #8
  Sep 19, 2011
  Joined: Feb 9, 2007
  Messages: 433
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  BONYEZA HAPA Mwalimu Julius K. Nyerere | Father of the Nation AU http://www.nyererecenter.org

  Naamini utapata viunganishi vya jawabu..
   
 9. T

  Topical JF-Expert Member

  #9
  Sep 19, 2011
  Joined: Dec 3, 2010
  Messages: 5,176
  Likes Received: 11
  Trophy Points: 0
  Sema huna mfano acha kulalamika!

  Mengine unaimba ngojera ulizoimbishwa kwenye jumuiya..ok

  kama hakuna mfano..unakubali kuwa alikuwa mnafiki...double standards at most ndio maana ali- survive
   
 10. Makindi N

  Makindi N JF-Expert Member

  #10
  Sep 19, 2011
  Joined: Mar 14, 2008
  Messages: 1,068
  Likes Received: 12
  Trophy Points: 135
  If u r political blind jukwaa la siasa ain't ur right place............ Hata mtoto wa darasa la tatu hayo maswali anayo majibu yake............
   
 11. LINCOLINMTZA

  LINCOLINMTZA JF-Expert Member

  #11
  Sep 19, 2011
  Joined: Mar 15, 2011
  Messages: 1,640
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 0
  Kwa hiyo unafiki ilikuwa ni mbinu ya kukabiliana na mataifa makubwa? Unaweza kuelezea zaidi? Vipi kuhusu uchoyo alipowanyima wazungu kuchimba madini yetu, haujauona?
   
 12. zimmerman

  zimmerman JF-Expert Member

  #12
  Sep 19, 2011
  Joined: Feb 17, 2011
  Messages: 579
  Likes Received: 280
  Trophy Points: 80
  Wazungu ni wajanja sana. Kabla ya yote wanaanza wanasoma pyschologies za viongozi wenu. Wakishangundua viongozi wenu wakuu, hasa rais, ni mtu mwenye weledi wa kutosha, yuko exposed, ana akili, ana uwezo wa kujenga hoja thabiti za kulinda maslahi ya wananchi wake hata ikibidi kujitoa muhanga kisiasa lakini hayuko tayari kuibiwa basi wanafanya mambo yafuatayo kutegemea na mazingira: Kwanza, wanamuheshimu. Wanafahamu kwamba hawataeleweka kwa dunia nyingine iwapo watafanya ghasia tu ili kuwavuruga na kuwaibia. Pia hata wao wana dhamira ya hatia (moral consciousness) kufanya mambo ya kiwizi kinyume na utashi wa kisiasa na viongozi wenu wakuu, Wanahukumiwa nafsi zao wanapowapora maslahi yenu pasipo utashi wa viongozi wenu hasa mkiwa nchi maskini sana iliyotwaliwa kikoloni. Hivyo walimuheshimu Nyerere na hawakupenda kumchokoza kwenye uongozi wake mpaka pale walipopata mwanya.

  Ila wakigundua viongozi wenu wana ka upungufu fulani au ni hohehahe wa akili kabisa basi hapo watatumia kila hila mpaka wawapate. Kwa Mkapa walitumia mapungufu ya kutokuwa na uzoefu na kukurupuka kwake kufunga mikataba ya kiuwekezaji; kwa Kikwete ndo kabisa rahisi sana yule kumpata; ni kumwalika lunch pale Washington au Ten Downing Street; mpige suti zake tano na chenji mpatie and voila "all country is in your hands; do whatever you wishes!".

  Solution yao hawa wazungu ni rahisi. Huwezi kuwafukuza kwenye mikataba waliyokwisha funga, hilo haliwezekani kwa rais wa sasa au ajaye (nahisi hatatoka CCM). Lakini pamoja na jitihada zote za kisheria kujaribu kuimprove status za mikataba ya sasa, ni lazima pia kuwaonyesha kwa hisia na kwa vitendo kwamba kwamba walichofanya si kizuri na hilo linaanzia kwa kuwawajibisha wale wa upande wa serikali yetu waliofacilitate ile mikataba. Hili angalau litajaribu kurejesha heshima kwa nchi yetu katika jamii ya kimataifa na kwamba ah kumbe Tanzania wamejirekebisha na sasawana viongozi wenye akili wanaoweza kurekebisha mambo.
   
 13. T

  Topical JF-Expert Member

  #13
  Sep 19, 2011
  Joined: Dec 3, 2010
  Messages: 5,176
  Likes Received: 11
  Trophy Points: 0
  Yes unafiki anawadanganya wananchi under the table anafanya nao biashara

  Uchoyo hiyo ni topic nyingine...alikuwa mchoyo mpaka akanyima mwenyewe, akaona kila tajiri ni adui, akaabudu umaskini hatimaye akafa maskini
   
 14. b

  bitimkongwe JF-Expert Member

  #14
  Sep 19, 2011
  Joined: Oct 21, 2009
  Messages: 3,034
  Likes Received: 211
  Trophy Points: 160
  What did he preach and what did he practice?
   
 15. b

  bitimkongwe JF-Expert Member

  #15
  Sep 19, 2011
  Joined: Oct 21, 2009
  Messages: 3,034
  Likes Received: 211
  Trophy Points: 160
  Bila kuyumba? you are joking! Hamukuwahi zile foleni zote za mchele, unga, sukari, kanga, sabuni na mengi mengine....
  ALIYUMBA HASAA MPAKA JASHO LIKAMTOKA.
   
 16. X-PASTER

  X-PASTER Moderator

  #16
  Sep 19, 2011
  Joined: Feb 12, 2007
  Messages: 11,651
  Likes Received: 105
  Trophy Points: 160
 17. ndyoko

  ndyoko JF-Expert Member

  #17
  Sep 20, 2011
  Joined: Nov 2, 2010
  Messages: 4,974
  Likes Received: 279
  Trophy Points: 180
  Maji yalipomfika shingoni ndio akaamua kung'atuka, unadhani aliachia nchi kwa kupenda mdugu!
   
 18. SHERRIF ARPAIO

  SHERRIF ARPAIO JF-Expert Member

  #18
  Sep 20, 2011
  Joined: Aug 25, 2010
  Messages: 7,081
  Likes Received: 1,818
  Trophy Points: 280
  Times have changed, mkuu. Hata huyo Nyerere angekuwa yupo madarakani zama hizi angeishia kupiga kelele tu kama wafanyavyo Chavez na Ahamedinajad leo hii ili dunia imtambue lakini kivitendo asingaliweza kuwazuia wababe wenye dunia yao kufanya wayatakayo.
  Mbona CIA ndio wali-engineer muungano wa Tanganyika na zanzibar na akatekeleza?
   
Loading...