Hivi ninyi CCM, matatizo ya Wananchi ni Lowassa?

Mahweso

JF-Expert Member
Jan 10, 2014
1,098
1,501
Mbona hatuwasomi vile, inakuwaje muda mwingi mnamshambulia huyu Mtu? kwani Serikali haipo?

Hivi kweli Maji hayapatikani kwa sababu ya Lowassa? Hivi kweli Dawa hakuna kama anavyo sema Magufuli kwa sababu ya Lowassa? Hivi kweli migogoro ya mashamba ni kwasababu ya Lowassa? Hivi kweli Elimu mbovu ni kutokana na Lowassa?

Tuambieni mtatutoaje kwenye hali ya umasikini, Kama mkitaka tuanze kukashifiana mbona kila mwana CCM ana yake? Mbona wenzenu wanahangaika kutushawishi jinsi ya kututoa kwenye Umasikini mbona ninyi mnahangaika na Lowassa?

Hivi kweli umasikini wetu ni Lowassa?

Tunaomba kidogo mtuheshimu maana tunajielewa msifikiri hatujielewi jamani,
 
Lowassa ndiyo sera ya sisiem hakuna nyingine hawana jipya ndiyo maana hii sera tumeisikiliza kwa makini na tumeilewa sana na tutaichagua tarehe 25,waacheni waendelee kutueleza juu ya Lowassa wakijashtuka yye yupo ikulu
 
Ukiishiwa Sera kwa demu.mpondee bwana ake.angalizo.

Iwapo tu una mvuto,kama huna inakuwa kama ccm.utaharibu zaidi.
 
Mbona hatuwasomi vile, inakuwaje muda mwingi mnamshambulia huyu Mtu? kwani Serikali haipo?

Hivi kweli Maji hayapatikani kwa sababu ya Lowassa? Hivi kweli Dawa hakuna kama anavyo sema Magufuli kwa sababu ya Lowassa? Hivi kweli migogoro ya mashamba ni kwasababu ya Lowassa? Hivi kweli Elimu mbovu ni kutokana na Lowassa?

Tuambieni mtatutoaje kwenye hali ya umasikini, Kama mkitaka tuanze kukashifiana mbona kila mwana CCM ana yake? Mbona wenzenu wanahangaika kutushawishi jinsi ya kututoa kwenye Umasikini mbona ninyi mnahangaika na Lowassa?

Hivi kweli umasikini wetu ni Lowassa?

Tunaomba kidogo mtuheshimu maana tunajielewa msifikiri hatujielewi jamani,

lowasa anashambuliwa sana kwasabab ni fisad na amekinunua chama chetu kwa bei nafuu kutoka kwa mbowe
 
lowasa anashambuliwa sana kwasabab ni fisad na amekinunua chama chetu kwa bei nafuu kutoka kwa mbowe

Kwanza umeelewa mada? Ufisadi ni mfumo au Mtu binafsi, elewa tuko kwenye Uchaguzi, tunataka kujua watatufanyia nini, kama wanataka tuwasikilize kuhusu Lowassa wajitoe kwenye uchaguzi wapambane na Ufisadi kwanza,

Tunataka kujua watatutoa vipi kwenye umaskini, ahadi walizo ahidi wametekereza asilimia ngapi, na wanazo ahidi watatekereza vipi. Ufisadi ni kazi ya Serikali sisi wananchi tunataka maisha bora, kupambana na Ufisadi ni kazi ya Serikali kama imeshindwa sisi wananchi tutafanya nini? hata mkitwambia Lowassa Fisadi inatusaidia nini? kuwa mwelewa ili uweze kujadiri mada kama hizi.
 
Back
Top Bottom