barafu
JF-Expert Member
- Apr 28, 2013
- 6,739
- 32,866
Sikubaliani sanaaa na JPM kwa mambo mengi, lakini sajajua watu wanataka aanze na lipi na aachane na lipi.
Sikubaliani nae kwa baadhi ya mambo,lakini mbona kila analoanza nalo, ambalo hata hao wapinzani walituahidi kuanza nalo wanakuwa hawaungi mkono? Hivi yote ya huyu Mzee ni "mabovu".
Zitto dhamiri inamsuta, anajua "madudu" ya Manji akiwa mwenyekiti wa kamati ya PAC akiwa mbunge wa Kigoma Kaskazini, kila walipofungua miradi "tata" ya NSSF, PSPF, Kagoda, Tanesco, huko kote huwezi kumkosa Yusufu.
Alituambia Godbless Lema, kuwa hizi transfoma za TANESCO zinanunuliwa mara tatu zaidi ya bei ya kawaida. Yusufu yupo katikati anapiga pesa, Lema akasema kama hii serikali inafukunyua "wezi" kwanini isifukunyue huyu mtu na kuvunja hiyo biashara yake na TANESCO?
Baadae tukaambiwa mradi wa Coco Beach mpaka huko Tigo ni muendelezo uleule. Gazeti la MwanaHalisi likatueleza jinsi Yusufu alivyoandaa mapesa ya kuwapa madiwani na watendaji ili apate Umeya wa Jiji, kama si yeye basi chama chake. Akahisani harakati zote kuhakikisha UKAWA hawana Meya wa jiji, mambo yakagonga mwamba.
Tukaambiwa, lengo la Umeya huu wa diwani wa Mbagala Kuu, ilikuwa ni kuhakikisha mambo yake yanakwenda vizuri kama "Lord Mayor of Dsm City". Maanake sasa lile shamba la Geza Ulole lingepata hati halali, na timu ya wananchi ingepata eneo la kujenga uwanja ili unapotaka kuuchukua uwanja, basi upambane na mashabiki wa team ya Wananchi na si Mayor wa Dsm.
Kwa midomo yao, na kauli zao, Zitto alitamani nchi ikamatwe na watu wenye maono na nia ya Meles Zenawi, Waziri Mkuu wa Ethiopia. Zitto ni muumini wa sera na mtindo wa uongozi wa Meles Zenawi, alimuandikia Tanzia siku ya kifo chake, aliomboleza na akatamani Tanzania ipate watu aina ya Meles Zenawi.
Meles Zenawi "hakupenda" Wapinzani, hakuwa mwanademokrasia, alichapa kazi bila kutazama nyuma. Zenawi aliwapendelea kidogo watu wa kabila lake ili asipate kupingwa sana.
Shirika na ndege lilikua na miundombinu ikastawi. Zenawi wa Addis Ababa ni kipenzi cha Zitto, kwanini ZZK asimpende "Meles Zenawi" wetu ambaye ni kama anaendana na yule wa Ethiopia?
Wakati wa kifo cha Meles Zenawi, Zitto Kabwe aliandika tanzia yenye kicha cha habari.. Soma hapo > Nitaishi kuwa Meles Zenawi.
Tulitaka mtu anayetafuta chanzo, ili apate mwanya wa kufikia "ufisadi" wa mtu kwa kufumba macho. JPM analiweza hili...kwa chanzo kingine ili kufikia jambo jingine!
Haya ndio waliyataka watu kama kina Zitto, lakini leo ni kama wanayapinga.
Dr Slaa ilikuwa ndio matamanio yake. Walituahidi kurudisha nyumba zote za serikali zilizouzwa na Magufuli na Mkapa. Walisema watawatafuta kwa mbinu zote "mamilionea" walio na mashaka na "umilionea" wao.
Zitto alituambia jinsi kada mmoja na mbunge wa CCM wakati huo, alivyotumia mwanya wa ubunge wake kununua mashamba ya mkonge na kuyaweka kama dhamana ya mkopo ktk benki za nje ya nchi. Akajipatia mabilioni ya pesa kwa mgongo wa mashamba ya Mkonge ambayo serikali haikuwa inafaidika kwa lolote. Na kwa sasa ni mmoja wa mabilionea wanaorodheshwa ktk majarida makubwa ya dunia. Inawezekana siku na huyu "akipokwa" mashamba, ZZK atalalamika.
Alipotutangazia "Mapinduzi ya Mkonge" akiwa Tanga, Zitto alionyesha nia ya kuyarudisha mashamba haya kwa wakulima wa mkonge kama atapata dhamana ya kuongoza. Alituaminisha kuwa, linapokuja suala la kuurudisha uchumi na njia zote kwa za uchumi bora kwa wananchi wa chini, "udikteta smart" ndio suluhisho.
Akasema ukiona mtu ni "dikteta" wa uchumi, huyo anatufaa, kuliko yule dikteta ya "siasa na demokrasia", maana wananchi wa chini hawali "siasa" ila wanakula "uchumi".
Pengine leo likianza zoezi la kurudisha nyumba za serikali toka mikononi mwa wale waliouziwa, basi kuna hatari ya watu kuanzisha "maandamano" kuwa "udikteta" unachukua nafasi.
Wapinzani walituambia sana juu ya "Ghost-workers",wakati Dr Slaa (akiwa mwenyeki wa LAAC) alisema sana juu ya watumishi hewa, akasema sana juu ya mishahara hewa, akatuambia sana juu ya "mchwa" wa halmashauri wanaotafuna pesa za maendeleo. Sijajua yeye angepata nchi, angeanzaje kulishughulikia jambo hili.
Ni kweli Mzee huyu ana mapungufu, sio malaika, labda ni kwa sababu amebana sana "uhuru na demokrasia" ndio maana wengi wanampigia kelele bila kumpa pongezi za huu upande anaojitahidi.
Sasa wamekuwa watetezi wa yoyote aliyefikiwa na "bwana pepsi".
Haya yanayohusu CCM na "mafisadi" wao, upinzani wangekaa kimya, wao wajikite ktk kukumbushia uhuru wa habari, demokrasia na siasa huru. Haya ya Manji wa NSSF na Manji wa "Mkemia Mkuu", yanaweza kuwakosesha uhalali wa kukemea mengine mbele ya safari.
Ni mtazamo tu, tujadili kwa usawa bila taharuki.