Hivi nini maana ya kusajili namba za simu tanzania??????? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Hivi nini maana ya kusajili namba za simu tanzania???????

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by drphone, Apr 27, 2010.

 1. drphone

  drphone JF-Expert Member

  #1
  Apr 27, 2010
  Joined: Sep 29, 2009
  Messages: 3,563
  Likes Received: 29
  Trophy Points: 145
  wakuu naombeni mchango wa mawazo nilipoteza line yangu ya voda na aliyeokota akawa anatumia kwa vile ninaline mbili watu wakawa wananipigia line ya tgo kwamba mbona upokei cm ndipo nilipogundua na nilipowasiliana na voda kwa namba ingine nikataja password yangu ya m-pesa wakaifunga ile cm kivumbi nipale nilipokwenda kurudisha line yangu mlolongo niloukuta nikapewa fomu nikajaza mwisho natakiwa nitaje namba 5 nilizokuwanawsiliana nazo na nikatoe copy ya kitambulisho copy hawana na ipo mbali kidogo na ofisi yao swali langu la msingi nilowauliza na ninalotaka msaada wa mawazo kwa greatthinker ni kunamaana gani ya kusajili namba za simu kwani siku ya kusajili nilijaza fomu na copy ya kitambulisho je awaweki rekodi kwenye komputer na kwann iwe hivyo au ndio ubabaishaji
   
 2. PakaJimmy

  PakaJimmy JF-Expert Member

  #2
  Apr 27, 2010
  Joined: Apr 29, 2009
  Messages: 16,236
  Likes Received: 309
  Trophy Points: 180
  Dr Phone, wewe ndo ulitakiwa utueleze haya...
  BTW, Data zinakuwepo kwenye computer, na ndio maana ukituma M-PESA, unapata ujumbe kwenye simu yako kwamba zimemfikia (fulani), ambapo jina lake sahihi linakuwa retrieved!
  Lakini wanaweka kumbukumbu ya hard-copy pia kwaajili ya kuzifanyia kazi baadaye, maana hawawezi kuanza kujaza details zako zote kwenye database kwa muda unaoenda kujiandikisha!

  Mi naona ni kitu chema tu!
   
 3. drphone

  drphone JF-Expert Member

  #3
  Apr 27, 2010
  Joined: Sep 29, 2009
  Messages: 3,563
  Likes Received: 29
  Trophy Points: 145
  mkuu nimelumbana nao sana kwani mm niliwaeleza ninachofahamu wakakubaliana na mm lakini akasema awajaingiza kwenye database yani ni manual ndipo nilipo ona ni ubabaishaji wa kukurupuka bila kujipanga haya ndo madhara yake mkuu inakuwa usumbufu kwetu jambo la dk 1 linachukua masaa kama umesajili namba yako utakiwi tena maswali kama unavykwenda benki wakiingiza jina lako watapata picha na signature yako hayo ndo tunayotaka mkuu
   
 4. drphone

  drphone JF-Expert Member

  #4
  Apr 27, 2010
  Joined: Sep 29, 2009
  Messages: 3,563
  Likes Received: 29
  Trophy Points: 145
  za m-pesa zinakuwa tofauti zile inaonyesha wamezifili kwenye data base zao ndio mana nilipotaka kuifunga line nikaulizwa kama nimesajili m-pesa niliposema ndio nikaulizwa jina na namba ya siri nilipotaja akasema sawa tunaifunga na dk ile ile ikafungwa bila kwenda ofisini kwao ila hizi za kusajili namba kwa zoezi lao hili ndo zipo tu kwenye hardcopy
   
Loading...