Hivi nini kinazuia kuonyeshwa picha za watu waliokamatwa na makosa mbali mbali kwenye TV, Magazeti | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Hivi nini kinazuia kuonyeshwa picha za watu waliokamatwa na makosa mbali mbali kwenye TV, Magazeti

Discussion in 'Jukwaa la Sheria (The Law Forum)' started by Kiraka, Jan 29, 2012.

 1. Kiraka

  Kiraka JF-Expert Member

  #1
  Jan 29, 2012
  Joined: Feb 1, 2010
  Messages: 2,551
  Likes Received: 613
  Trophy Points: 280
  Nimekuwa nikiangalia taarifa za habari na magazeti na ni mara chache sana utaona watu waliokamatwa kwa makosa mbali mbali kuonyeshwa picha zao kwenye runinga, au picha kwenye magazeti.
  Je kuna sheria yoyote inazuia hili, hatusemi kuwa wamehukumiwa na makosa lakini kwani si ni kweli wamekamatwa kuna tatizo gani kuonyesha picha zao?
  Nikilinganisha na nchi za Ulaya au hata Kenya wao huwa wanaonyesha habari kama ilivyo, lakini sisi utakuta mara nyingi Wakuu wa polisi wakiwa na marundo ya risasi au vitu vya wizi wakionyesha kuthibitisha kutokea kwa tukio, lakini kamwe hawata onyesha picha za waliokamatwa. Je kwa kufanya hivi hawaoni kuwa hata wanaongeza bure muda wa kufanya upelelezi , kwani pengine wangeonyesha hao waharifu labda wangepata watu kuwasaidia katika upelelezi au kupata taarifa zaidi za matukio mengine.

  Naoma ufafanuzi wa kisheria kama kuna sheria inazuia hili maana mimi sioni sababu ya kuficha sura za watu waliokamatwa na makosa mbali mbali kwani wangesaidia sana sisi raia kuweza kujilinda, inawezekana kabisa tunaishi na majambazi yanakamatwa katika matukio lakini kwakuwa hawaonyeshwi basi hatujui na tunaendelea kuishi nao bila kuchukua tahadhari yoyote.
   
 2. zeus

  zeus JF-Expert Member

  #2
  Feb 5, 2012
  Joined: Aug 13, 2009
  Messages: 213
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  mimi si mtaalamu wa sheria lakini nadhani si vizuri kumuonyesha mtuhumiwa kwenye tv au gazeti la kila siku kwa sababu ya tuhuma tu. Unapom-parade mtu kwenye runinga au gazeti unaonyesha umma kuwa mtuhumiwa ni mtu fulani na umma unhukumu kwa namna fulani, watu wanakuchukulia kuwa wewe ndio unahusika hata kabla mahakama hazijathibitisha hivyo kulingana na ushahidi. ni sawa na kumhukumu mtu bila ushahidi. hali hiyo inaathiri heshima na mahusiano ya mtu na rafiki zake, familia yake na jamii kwa ujumla. Inaathiri kazi au biashara yako, watu watakukwepa, hutapata ajira, hakuna mtu anakuamini, unapomtangaza mtu kuwa ni muuaji, mbakaji, au jambazi utawezaje kuja kumsafisha pale itakapothibitika kuwa hahusiki na kosa liliofanyika? utamlipa fidia au? Utakuta magazeti yetu yanaandika '' aburuzwa mahakamani kwa kubaka** , unategemea wasomaji wako waelewe au waamini nini? wakati huyo mtu ametuhumiwa tu au pengine amefananishwa! au pengine mlalamikaji ni muongo wala hakubakwa(ni visa tu). kwa sababu hii tunaweza kusema sio sahihi kuweka picha za watuhumiwa live kwenye runinga au front page ya gazeti. lakini haya yote yanategemea ni kwa kiasi gani tunathamini utu wa mtu. Tanzania tuna jamii inayopenda udaku kuliko uchambuzi, inayopenda matukio kuliko mijadala ya maendeleo. na vyombo vetu vya habari vina akisi jinsi tulivyo.....
   
 3. King Kong III

  King Kong III JF-Expert Member

  #3
  Feb 5, 2012
  Joined: Oct 15, 2010
  Messages: 25,153
  Likes Received: 2,402
  Trophy Points: 280
  Yeah kwasababu ni tuhuma na tuhuma zinahitaji upelelezi ukiwaonyesha kwenye magazeti na tv unaweza ukaharibu upelelezi wa kesi
   
 4. Monstgala

  Monstgala JF-Expert Member

  #4
  Feb 5, 2012
  Joined: Aug 25, 2009
  Messages: 1,080
  Likes Received: 77
  Trophy Points: 135
  Zeus, umechambua vizuri sana hasa pale issue inapokuwa bado ni tuhuma, sasa basi jitihada zingefanywa kuonesha picha za wahalifu baada ya kukutwa na makosa na kuhukumiwa. Hii ingesaidia kwa kiasi fulani maana hata wahalifu sugu mara nyingi wanakuwa hawatambuliki kwa jamii hivyo wanapomaliza vifungo vyao hurudia uhalifu ule ule au zaidi kwa kuwa jamii haiwatambui.
   
 5. Kiraka

  Kiraka JF-Expert Member

  #5
  Feb 6, 2012
  Joined: Feb 1, 2010
  Messages: 2,551
  Likes Received: 613
  Trophy Points: 280
  Kabisa hata mimi ninachosema .. kama mtu amekamatwa na tukio ni kweli limetokea amekamatwa na madawa ya kulevya , kuna ubaya gani kumwonyesha akiwa na hayo madawa au risasi au mali ya wizi.. si kweli kakamatwa, halafu mnasema kuwa bado ni mtuhumiwa... Mimi ninachokataa ni huku kuficha ficha , mbona wakikamatwa watu vijijini huwa wanaonyeshwa kabisa na hata saa nyingine kuhojiwa? Ni kwanini basi iwe double standard.. sidhani kama kwa kumwonyesha mtu na ukasema wazi kuwa ni mtuhumiwa kutakuwa na tatizo lolote pale akishinda kesi.. Mbona Rage leo Mbunge na alifungwa kabisa.

  Mimi nadhani ni njama tu za kutaka kuficha au kudanganya au namna ya kutaka rushwa kwa hao wahusika.
  Nasema tena mbona wenzetu hata hapo Kenya vyombo vya habari viko huru tu.. kwanini hapa....
   
Loading...