Hivi nini hatma ya mtumishi wa Serikali ambaye amekopa benki Tsh. mil. 15 na akaamua kutoweka kazini?

the kind

JF-Expert Member
Nov 6, 2019
773
571
Amani ya Mwenyezi Mungu iwe nanyi

Kuna mtumishi mwenzetu ambaye amekopa benki kiasi cha Tsh. milioni 15 na baada ya wiki akatoweka hakuonekana tena kazini ni mwezi wa pili sasa tangia atoweke na wala hapatikani kwa mawasiliano yoyote yale

Je, nini hatma ya pesa aliyokopa benki, namaanisha marejesho?

Nini hatma yake kama siku anapatikana?

Ipi inaweza kuwa hukumu yake endapo atapatikana?
 
Kwa benki hakunaga tatizo kwa sababu mikopo yao huwa ina bima.

Na hata ikitokea wamekukamata huwa hakuna kesi ila mnakaa mezani na kupatana njia ya marejesho kutegemea na uwezo ulionao kwa wakati huo.

Ila kwa upande wa serikali sijajua kulingana na kitengo cha huyo mto anayekimbia kazi.

Kama ni kazi inayohusu uaskari ukikimbia wanakutafuta na wakikukamata wanakuweka mahabusu ukitoka unalazimishwa kuendelea na kazi.
 
Enzi za JK ingewezekana! Ila kwa awamu hii, lolote linaweza kutokea. Kama ni wewe mwenyewe mwenye mpango huo, ni vyema ukavumilia tu mpaka hilo deni litakapo kwisha!

Achana na hayo mambo ya kukopa sherehe, kulipa matanga.
 
Watanzania wengi hatusomi ile sehemu ya vigezo na masharti..mambo kama haya huwa yanawekwa wazi kule.
 
Tuelimishane kidogo

✓Kuna hela ya mtumishi wa umma anaktwa kwenye hifadhi za kijmii, mfano LAPF
✓Huyu mtumishi anapoenda kukopa Benki, Cha kwanza benki ataangalia kwenye LAPF yako umefikisha kiasi gani
✓Afu Benki watakukopesha kutokana na kiasi kilichopo kwenye LAPF
✓Endapo utatoroka na kuondolewa kwenye payment wao watapeleka barua huko LAPF kuonyesha deni lako na baada ya kujiridhisha,,pesa yako itahamishiwa kwenye account ya benki inayokudai
 
Back
Top Bottom