Hivi nina tatizo?

platozoom

JF-Expert Member
Jan 24, 2012
9,366
11,154
Kwenye mahusiano nimepita pengi kiasi. Na hapa nazungumzia uzoefu wangu binafsi ambao hata mimi unanitisha: Ni rahisi kumulika mwizi au kuujua uongo.

Iko hivi, Ni kwamba naweza kuwa kwenye mahusiano mazuri tu na yakaendelea kwa muda fulani, lakini kwangu inakuwa rahisi sana kuhisi (kama ndivyo ilivyo) g/f wangu anachepuka/kuflirt pembeni na nikishahisi sitalala mpaka nipate ushahidi usiotiliwa mashaka.

Hapo napata amani sana................sijui kwa nini lakini kitendo cha mimi kuhakikisha kwamba nachezewa mchezo huwa ndiyo hitimisho la amani, na kama sitapata nachokitaka sitakuwa "comfortable" (na lazima nitaujua ukweli).

Si hilo tu kuna kusema uongo........Ipo hali kudanganya kwenye mahusiano: Inawezekana tukawa katika hali ya kawaida ya mahusiano lakini kama itatokea akanidanganya kwa lolote lile hata kama ni dogo haitachukua muda nitaujua ukweli au papo hapo kushuku alichoniambia. Na bahati mbaya huwa sikawizia au kuvumilia.... napojua tu namlipua (hata kama si kumuacha).

Hii imepelekea hata huyu g/f wangu wa sasa kuniogopa kiasi fulani japo haniambii na pia sijaonyesha kumchimba ingawa kuna wakati aliniambia X wangu huwa anawaambia watu ananiogopa (anamfahamu).

Ndipo najiuliza mimi ndio nina tatizo ama nipo kwenye mkondo sahihi au ni pepo lol!!
 
Una tatizo tena kuubwa sana

Kivipi....Kwa sababu wakati mwingine nahisi labda kama ningekuwa namfanyia uchunguzi kabla sijaona red light pengine ingekuwa tatizo. Lakini hii ya niki-doubt nafanikisha ni tatizo pia?
 
Kivipi....Kwa sababu wakati mwingine nahisi labda kama ningekuwa namfanyia uchunguzi kabla sijaona red light pengine ingekuwa tatizo. Lakini hii ya niki-doubt nafanikisha ni tatizo pia?

Ukimchunguza kuku hutamla....
una doubt sababu unajua toka mwanzo.....

Ni sawa na mtu aamue kuishi na Simba halafu aseme nikihisi damu
nitachunguza nitajua...

while simba kula nyama ni jadi yake...
 
Ukimchunguza kuku hutamla....
una doubt sababu unajua toka mwanzo.....

Ni sawa na mtu aamue kuishi na Simba halafu aseme nikihisi damu
nitachunguza nitajua...

while simba kula nyama ni jadi yake...

Girl nayeamua kuwa naye kabisa huwa tayari nimeamini ametulia na wala sitilii mashaka.
Labda nikupe kisa kidogo Siku tatu zilizopita X wangu alinipigia simu kunijulia hali na baada ya blah blah za hapa na pale nikamuuliza bado upo (wilaya jirani na nilipo), akanijibu ndiyo bado yupo huko, yakaishia hapo.

Jioni yake nikampigia kumuulizia rafiki yake mmoja juu ya hali yake (alikuwa mgonjwa na hayupo hewani) na kwamba nipate uhakika kama yupo kwake nikamtembelee........kumbe naye (X) alikuwepo hapo na si kweli kwamba hajarudi. Baada ya hapo alijifanya network inasumbua na akachanganyikiwa akihaha kidogo aanguke apitie wapi nisije kumkuta nikamuona muongo!!
Ndio maana bado najiuliza na nauliza hii hali ni nini?
 
mtani pole weeh!wakati mwingne ni raha kutokujua vitu vingine!
mwanadamu mpana sana rafiki yangu!
 
mtani pole weeh!wakati mwingne ni raha kutokujua vitu vingine!
mwanadamu mpana sana rafiki yangu!

Niilkuwa natamani usione haya maandishi yangu lol!
Ni kweli mwanadam mpana sana,sasa hii sauti ya ndani inayopiga alarm niifanyaje?
 
Girl nayeamua kuwa naye kabisa huwa tayari nimeamini ametulia na wala sitilii mashaka.
Labda nikupe kisa kidogo Siku tatu zilizopita X wangu alinipigia simu kunijulia hali na baada ya blah blah za hapa na pale nikamuuliza bado upo (wilaya jirani na nilipo), akanijibu ndiyo bado yupo huko, yakaishia hapo.

Jioni yake nikampigia kumuulizia rafiki yake mmoja juu ya hali yake (alikuwa mgonjwa na hayupo hewani) na kwamba nipate uhakika kama yupo kwake nikamtembelee........kumbe naye (X) alikuwepo hapo na si kweli kwamba hajarudi. Baada ya hapo alijifanya network inasumbua na akachanganyikiwa akihaha kidogo aanguke apitie wapi nisije kumkuta nikamuona muongo!!
Ndio maana bado najiuliza na nauliza hii hali ni nini?

Hiyo hutokea watu weengi
lakini kwa nini aogope wewe kumkuta hapo na umeshaa achana nae?
lazima utakuwa na 'nongwa' hivi..
huna 'dogo'....na wenzio wanakujua so wanakuficha ficha na kukukwepa
hilo ndo tatizo lako...
 
Mh! nongwa, afadhali umeiweka kwenye "quote"..........Ukweli ni kuwa hata simu X simpigii labda iwe kesi kama hiyo ya mgonjwa, hata habari ya maisha yake siitafuti na wala marafiki zangu hawajui nimeachana naye kwa lipi zaidi ya kuwaambia 'it was over' ili 'kumsitiri' (i guess).

Lakini kama sauti kutoka ndani inaniambia hapa unadanganywa au something wrong somewhere nitulie au unafanya maamuzi gani kwa hilo?
 
Unapo deal na women...
treat them like children....
dharau vitu vidogo...
 
Now that bossman is on the control room, mie napita pia. Ngoja upewe sure. Manake kama kila ukimhisi mpenzi unamchunguza hadi kupata ushahidi sijui kama kuna relationship ingedumu. Kama ni flirt zinafanyika, na kuitwa sweetheart maa mrembo ni kawaida sanaaa! Ndo maana hata Bible imeandika, Bwana kama wewe ungehesabu maovu ni nani angesimama?
 
mie nadhani twaweza kuwa tuko sawa

naweza uliza, ama nikatumia sense ya sita, na nikitumia sense ya 6 ni hatari tupu
 
Back
Top Bottom