Hivi ni wapi Rais Magufuli anakosea, mbona kila siku lawama zisizo na msingi?

Mukulu wa Bakulu

JF-Expert Member
Aug 12, 2014
4,052
12,905
Kila kukicha kunakua na lawama lukuki dhidi ya Rais Magufuli.

Nikiangalia sioni wapi amekosea saana(sijasema makosa hayapo), hizi lawama msingi wake ni nini?

Kuna wanaolalamika kuminywa uhuru wao wa kisiasa na maandamano na mikutano ya kisiasa(hawa wana hoja hasa ukizingatia haya mambo yako legalized kwenye katiba). Kikubwa ambacho watu wangekisemea ni hiki cha uhuru wa kisiasa na mikutano ya kisiasa.

Sasa wanaolalamika zaidi ya hao wanasiasa msingi wa malalamiko wao uko wapi, I don't see a pont kwenye malalamiko yao. Huwezi kusema kuminywa kwa uhuru wa kisiasa kumesababisha wewe usile.

Wanaolalamika nje ya wanasiasa wanalalamika nini, nashangaa kuona hadi wafanyakazi wanaolipwa mishahara wanalalamika wakati hawajawahi kukosa kulipwa mishahara, hopeless kabisa.

Mahala pengi rais anafanya vizuri kuliko vibaya, kubana wakwepa kodi, kubana matumizi yasiyo na msingi ya pesa za umma, kurekebisha sheria kulinda rasilimali zetu na mambo kama hayo bado ni faida kwa taifa kuliko kutofanya hivyo.

Naomba kujua, mnaolalamika, wapi rais anakosea ili niweze kuungana na nyie kwenye kulalamika.
 
Ndio anafanya vizur baadhi ya sehemu ila sehemu kubwa analeta mashaka ..kwanza hataki kukosolewa anajiona yeye mungu mtu ...pili watu wanakufa wanapotea hasa upinzan nini maana yake .. Nchi zenye maendeleo kama USA watu wakiona uoneaji wanaandamana huku eti tufanye kazi zipi anazozisemea yeye !!! Maana vijana wapo hoolla ukisema wajiajiri mtaji wanautoa wapi !!! Maisha yamepanda bei mama ntilie wali wa buku sa hivi efu mbili " anaita vyombo vya habari ikulu vipunguze ukali vimsifie " tunajua anafanya mazuri na ana nia nzuri achange from materialism to consider people ... Ni hayo tuu asisahau atafute dawa ya frustration nimemaliza ..
 
Bashite leta vyeti,kala rambirambi,chato kupewa bajeti kubwa,kusimamishwa kwa ajira,uongo ripoti za TRA na makinikia,movie za kitoto kama kuokota vichwa vya treni, ubovu wa projects kama hostel za magu
 
Lawama lazima ziwepo, maana mfumo alioukuta ni watu kufanya haya ...
  • Mavyeti feki
  • Wizi na ufisadi
  • Kufanya kazi kimazoea
  • Kutokuwajibika na kutokuiheshimu kazi
  • Ubabaishaji, madili na utapeli uliokufuru
  • Madili na mikataba mibovu katika kila sekta..
  • Kutokupendakufanya kazi au kupata kipato halali..
  • Kutokupenda kufuata sheria bial shuruti..
Sasa watu ni kama mambo yamebadilika kabisa, walizoea maovu hayo juu, kubadilika hawataki, wanafikiri Magu akiondoka hayo maovu yatarudi ili warudie tena, wanajidanganya, haya ndio yatakuwa maisha yetu, mpaka mwisho wetu, ni kufuata dola inasemaje badala kupoteza nguvu kutaka huo uchafu kurudi tena..
 
Kumbe unakubiali wanafunzi wanakosa mikopo wewe ukiwa mmoja wapo sio, Sasa kwann hutaki watu walalamike
Sijakataa watu kulalamika lakini hiyo sio agenda kwani ni ngumu kwa serikali za nchi zilizopo dunia ya tatu kusomesha wanafunzi wote
 
Back
Top Bottom