Hivi ni vigezogani vinatakiwa ili mtu aweze kuwa dereva wa gari la wagonjwa?

jogoo wa maajabu

Senior Member
Joined
Mar 4, 2018
Messages
108
Points
250

jogoo wa maajabu

Senior Member
Joined Mar 4, 2018
108 250
Piga chuo cha kawida cha veta ,kata leseni tafuta chombo kaa barabarani uiveee kisawa sawa, kisha nenda NIT (national insitute of transport) piga kozi pale kachukuee udereva mahili daraja la pili utachagua kati ya VIP au HGV ama PSV chaguaa mojaa tembeea nayo ,ukimaliza daraja la pili kama mfukoni upo vizuri unganisha upige na daraja la kwanza hapo ndo utakuwa unaanza kutambulikaa kidogo kidogo kama dereva, kwa madereva wenye mpango wa kufanya kazi ktk sector furani nzury huu ndo mwongozo mzuri sana then kama wewe ni form 4 na kuendelea maliza kabisa na kozi ya mwisho 'senior driver' hapa ndo utaingia ktk kinyanganyilo kizuri endapo zikitokea fursa za ajira haswa za udereva ktk makampuni ,mashirika makubwa ama serekarini.

Kabla ya kuyajua haya nilienda chuo cha nit kuulizia kati ya hizi corse ipi nzury niipige chapu, nlikutana na dogo mmoja kafuta corse zote hafu dogo ukimcheki miaka 21 tu....ahsanteni.
 

Mr.Thinker

Senior Member
Joined
Dec 13, 2013
Messages
109
Points
250

Mr.Thinker

Senior Member
Joined Dec 13, 2013
109 250
Kwa uelewa wangu
Dereva wa gari la kubeba wagonjwa muhimu awe na leseni ambayo daraja lake linaruhusu aendeshe gari za abiria kama vile hiace na coaster(wenye fani wanajua madaraja yao)
Pili, awe na cheti kinachoonesha amehitimu kozi ya huduma ya kwanza.kozi hii ni ya muda mfupi tu(haipungui miezi mitatu na haizidi mwaka mmoja), hutolewa na vyuo vya afya mbalimbali hapa Tanzania(Na gharama yake ni nafuu).

Mwisho kabisa, vigezo na sifa zilizobaki ni principal/basic kwa kazi yoyote ile wanaJF
Kama vile, umri kuanzia miaka 18 na kuendelea, awe raia wa Tanzania, asiwe na rekodi za jinai/kufungwa jela, asiwe mlevi, muaminifu n.k

Lkn pia baadhi ya taasisi au hospitali, huchukua ama huajiri mtu mwenye kigezo cha leseni ya udereva tajwa hapo juu, kisha humpatia elimu ya huduma ya kwanza(Basic first aid training) kwa muda wa wiki 4 au 6. Kisha anakabidhiwa chombo(Gari).

Karibu kwa maswali yoyote yanayohusu sekta ya afya tu.
Vigezo gani au sifa zipi anatakiwa awenazo mtu anyetaka kuwa dereva wa gari la wagojwa

Nawakilisha.....
 

Auz

JF-Expert Member
Joined
Apr 6, 2016
Messages
6,152
Points
2,000

Auz

JF-Expert Member
Joined Apr 6, 2016
6,152 2,000
Uzoefu wa nchi ya Marekani, leseni ni ya kawaida tu bali awe amepata mafunzo ya kuhudumia mtu aliye na dharura kiafya, na si kwa juujuu tu ni kwa undani kama kumzindua, kumuwekea damu/maji mwilini, kumtoboa na kuingiza mipira ya hewa n.k.
Anapomfikisha hospitali anatoa taarifa ya kitaalamu ya jinsi alivyomkuta mgonjwa na kampatia huduma gani.
 

Forum statistics

Threads 1,391,865
Members 528,491
Posts 34,092,270
Top