Hivi ni vifaa vya kutunzia maji kipi umekitumia tangu utotoni?

yajutu

JF-Expert Member
Sep 5, 2016
951
1,206
6570204b0f422ae821fb4652f0a9204c.jpg
 
Ukhuty marhaba unajua tuliokuwa zamani kulikuwa na raha zake bi mkubwa alikuwa mkoloni ni marufuku kunywa maji umesimama inatakiwa unywe umekaa na ilikuwa ni utii mtindo mmoja leo hii watoto wabishi
 
Eti sikuhizi tunaambiwa infection control unahitaji water filter wakati tunakuwa maji yanaingizwa mtungini, ukitoka kuchecha rede unachota maji unakunywa, mwingine anachota anakunya, yakibaki anampa mwenzake. Kikombe hicho kimoja.
 
Mimi sio wa kishua,ila maishani mwangu sijawahi tumia maji ya mtungini home.

Nakumbuka niliwahi kuyatumia barabarani gari lilipata hitilafu maporini kiu imenibana,nikaona kijumba kwa mbaaaali nikaenda kuomba maji,daaaaaah!
Kuna watu wanaishi kwa taabu sana,niliyoyaona nilisikitika sana.
 
Back
Top Bottom