Hivi ni upi U - professor wa Mh Lipumba? Sina shaka na elimu yake lakini.....

Mboko

JF-Expert Member
Oct 8, 2010
1,095
293
Napenda kufahamu nini Uprofessor wa Mh Lipumba Ibrahim maaake sijawahi kusikia anafanya nini na taaluma yake hii Je?ana ushauri gani kwa serikali ya Bongo??
Nataka tu kuelewa simsemi vibaaya ni Proffesor wa ukweli namkubali lakini nataka kufahamu nini anafanya ukiondoa Uenyekiti wa Cafu.

Ahsanteni hope to get good answers from you The great thinkers
 
Umefanya vizuri kulizungumzia hilo. Mimi mwenyewe ni muislam lakini siwezi kuruhusu hawa watu watumie gia ya uislam kupata kura zetu

Prof Lipumba haongei na wananchi mpaka nyakati za uchaguzi tu!
 
angekua chama tawala ungeutambua msaada wake lakini kutokana yupo upinzani mchango wake hautathaminiwa na wala mawazo yake kusikilizwa lakini ni mchumi mzuri sana
 
Umefanya vizuri kulizungumzia hilo. Mimi mwenyewe ni muislam lakini siwezi kuruhusu hawa watu watumie gia ya uislam kupata kura zetu

Prof Lipumba haongei na wananchi mpaka nyakati za uchaguzi tu!

mkuu sijakuelewa ni kama uko nje ya mada hivi.!
 
angekua chama tawala ungeutambua msaada wake lakini kutokana yupo upinzani mchango wake hautathaminiwa na wala mawazo yake kusikilizwa lakini ni mchumi mzuri sana

Lakini anaweza kutumia advantage ya kushare serikali kule Zanzibar, akaingia kwenye system na kuonyesha mchango wake. May be amejisahau sana na kuridhika na misifa ya kushauri Uchumi nje ya Tanzania, SIJAJUA SANA.
 
Ni Professor wa uchumi, hatumiki Tz kwasababu ya kiburi cha viongozi masikini wa fikra nchini humu!

Mkuu Genecius Kaiza,
Jamaa kashindwa kuinua uchumi wa CUF wa Taifa ataweza? Tangu miaka nenda rudi CUF imekua ni chama kinachotegemea ruzuku licha ya kuongozwa na Profesa wa Uchumi! Mbowe juzi juzi kabuni mbinu ya kuchangisha wafuasi kuongeza wingo wa mapato ya chama, nae kakopi na kupesti. Is this how Professors work?

Nakala: Kaka Mkweli
 
Kawaida ya siasa zetu hapa bongo ni kwamba mtanzania mwenzetu hata akiwa na uwezo vipi kitaaluma, kama yupo upinzani hawezi kuthaminiwa. Atapondwa aonekane si lolote wala si chochote. Lakini poa tu, ipo siku utanzania wetu utarejea tuwe kitu kimoja. Hizi siasa za chuki zilizopandikizwa na ccm haziwezi kutufikisha popote.
 
achen majungu hamjui kwamba alikua mshaur wa rais mwinyi ambapo mpaka leo mwinyi ndo rais alieleta maisha bora tz..meng ameyafanya lkn tatzo nch ya tz haipend kutumia wataala si tunapenda wanasiasa.
 
Mkuu Genecius Kaiza,
Jamaa kashindwa kuinua uchumi wa CUF wa Taifa ataweza? Tangu miaka nenda rudi CUF imekua ni chama kinachotegemea ruzuku licha ya kuongozwa na Profesa wa Uchumi! Mbowe juzi juzi kabuni mbinu ya kuchangisha wafuasi kuongeza wingo wa mapato ya chama, nae kakopi na kupesti. Is this how Professors work?

Nakala: Kaka Mkweli

Mi mwenyewe nimekuwa nikiumiza sana kichwa ninaposikia kuwa huwa prof eti mkuu wamaprof wa uchumi, nikajiuliza hivi huyu haoni kuwa nchi yake nimasikini halafu huku akiendelea kujiita prof wa uchumi wa dunia, nikajifariji na kajibu kangu mwenyewe kasikoridhisha eti labda mpaka aupate huo urais ndo atajidhihirisha kuwa yeye ni prof wa uchumi kweli, swali lingine likaibuka, kama kweli yeye ni mchumi kwa nini chama chake hakiongozi kwa vitega uchumi kwa sababu wanamwanauchumi wa dunia labda hii ingesaidia chama kujiendesha chenyewe bila kutegemea rudhuku au napo anasubiri mpaka awe rais, nikagundua kuwa ni kweli prof Lipumba ni mwanauchumi, lakini ni uchumi upi tunaouzungumzia? ni uchumi wa vitabu au uchumi wa kwenye makaratasi yaani non tangible economy
 
Napenda kufahamu nini Uprofessor wa Mh Lipumba Ibrahim maaake sijawahi kusikia anafanya nini na taaluma yake hii Je?ana ushauri gani kwa serikali ya Bongo??
Nataka tu kuelewa simsemi vibaaya ni Proffesor wa ukweli namkubali lakini nataka kufahamu nini anafanya ukiondoa Uenyekiti wa Cafu.

Ahsanteni hope to get good answers from you The great thinkers
Mwenye CV atuchomekee humu ndani, tuone machapisho na awards alizonazo katika medani za wasomi. Ukishaona msomi kaenda kwa siasa mara nyingi huko alikotoka amechemsha!
 
Huyu jamaa ni mweupe kinyama yaani. Hata sijui kwanini watu wanammegea maujiko yasiyo na kichwa wala mguu. Huyu jamaa kuna siku nilikutana naye kwenye harusi ya dadangu Arusha. Basi nikamuuliza je ukipata urais utafanya nini cha kwanza. Hayo majibu aliyinipa nikabaki naduwaa tu kama kweli huyu ni Profesa au Konjesta. Jamaa kichwa cheupe tu huyo mbona
 
Mkuu Genecius Kaiza,
Jamaa kashindwa kuinua uchumi wa CUF wa Taifa ataweza? Tangu miaka nenda rudi CUF imekua ni chama kinachotegemea ruzuku licha ya kuongozwa na Profesa wa Uchumi! Mbowe juzi juzi kabuni mbinu ya kuchangisha wafuasi kuongeza wingo wa mapato ya chama, nae kakopi na kupesti. Is this how Professors work?

Nakala: Kaka Mkweli
NI mtazamo tu!!!!
 
Anaganga njaa tu ila hana mchango wowote ktk hili taifa kama ilivyo kwa maprofesa wengine wa hapa tz. Pia ana sign za udini kwa mfana alikuwa ni mmoja aliyemchangia ponda ili aendeshe kampen kwa waislam kususia sensa
 
Naomba uweke dondoo ya majibu aliyo kupa.

maana mimi nimesha msikiliza lipumba mara nyingisa ni mtu mwenye mawazo mazuri sana kwa swala la uchumi, sema serikali yetu haitaki kumtumia vizuri.

Sio kweli kwamba ni mweupe.
Huyu jamaa ni mweupe kinyama yaani. Hata sijui kwanini watu wanammegea maujiko yasiyo na kichwa wala mguu. Huyu jamaa kuna siku nilikutana naye kwenye harusi ya dadangu Arusha. Basi nikamuuliza je ukipata urais utafanya nini cha kwanza. Hayo majibu aliyinipa nikabaki naduwaa tu kama kweli huyu ni Profesa au Konjesta. Jamaa kichwa cheupe tu huyo mbona
 
Profesa Lipumba alinifundisha Chuo Kikuu napenda kusema ni mmoja kati ya ma Lecture wachache sana ambao walikuwa wanafundisha na kueleweka kwani alikuwa anatoa mifano ambayo inaendana na uchumi wa nchi hii, tofauti na ma Lecture kama Dr. Mpango wa tume ya mipango ambaye ndio anatakiwa atengeneze dira ya uchumi wa nchi hii.

Mipango yeye aliongoza kwa kutisha wanachuo wa somo lake na alikuwa haeleweki darasani, naamini Pro. anauwezo mkubwa sana wa kushauri mambo ya uchumi kwani ametumika katika nchi hata jirani ya Uganda na ikawa na uchumi mzuri kwani kabla ya hapo ilikuwa hoi sana.

Tatizo la Lipumba ni kuingia kwenye siasa mchwara za Tanzania aliamini angekuwa kwenye siasa angeweza kuwa raisi wa nchi hii na kuleta mabadiliko ya kiuchumi.
 
Back
Top Bottom