Hivi ni ujinga, wivu au ni roho mbaya wanandoa waliotengana kuwazuia waliokua wenza wao kuwa na wenza wengine?

mama D

JF-Expert Member
Nov 22, 2010
19,760
35,205
Nilisikitishwa sana na hili tukio lililomkuta kaka Sindato kwa kweli!

Na hii sio kwa Sindato tuu. Inatokea kwa watu wengi wanaume kwa wanawake. Unakuta watu wameshashindwana na kuamua kuachana lakini mmoja wao anapoamua kuingia kwenye mahusiano mengine inakua vita.

Tena wengine wanafikia hatua ya kuuana ili mradi mtu asiwe na mwenza mwingine.

Binafsi naamini ndoa ni maisha mazuri yenye kumpendeza Mungu na watu wanaotuzunguka; na zaidi naamini ndoa ni upendo Kati wa mwanaume na mwanamke. Naamini kabisa kama hakuna upendo basi hakuna ndoa, zaidi kutakua na uadui Kati marafiki waliogeuka kuwa maadui. Na hii ndio inapelekea kwenye Ile hatari ya watu kuuana na kuumizana.

Ifike mahala waoaji na waolewaji watambue kwamba kuoana na mtu haimaanishi kwamba hata upendo unapokua umeisha wewe utaendelea kummiliki, kumnyima haki yake ya kuishi na kumiliki vitu vingine na maisha mengine.

Yaani hawa watu wametengana nikiwa mdogo sana, hapo wanasema 18 years lakini kiuhalisia ni zaidi ya hiyo miaka. Sema hiyo 18 ndio yenye ushahidi wa utengano wao.

Wote ni waelewa, sheria ya ndoa ya dini yao wanaijua, sheria ya ndoa ya nchi wanaijua, wanajua kabisa hadi hiyo miaka ndoa ilishakua batili. Sasa sijui nia yao sasa ni kukomoana au kutaabishana tu.

Ndoa ya kikristo wanawake wanaitumia kama silaha ya kukomoa wanaume. Hasa kama mume ana pesa. Mwanamke hataki pesa ya mirathi imponyoke.

Kesi hizo zipo nyingi sana. Mwanamke anakubali mtengane hata miaka 100. Ila ukimwambia swala la divorce hataki hata kulisikia. Na anakimbilia kanisanii kabisaaa kutaka wachungaji wasilikubali.
 
Lakini mali si ni YENU--mke na mume? Ndoa hainaga EXPIRY DATE.
Wanang'ang'aniaga penye fursa tu. Angekuwa kapuku hata asingehangaika.
Msisahau mahakama ilichofanya kuhusu suala la Jackyne (?) wa late Dr. Mengi.
 
Lakini mali si ni YENU--mke na mume? Ndoa hainaga EXPIRY DATE.

Msisahau mahakama ilichofanya kuhusu suala la Jackyne (?) wa late Dr. Mengi.

Kuna mali za pamoja mke na mume kisheria zinaitwa matrimonial property. Na pia kuna mali binafsi za wanandoa. Ambazo mmoja wa wanandoa kazitafuta mwenyewe kabla hamjafunga ndoa. Ama amerithi kwenye ukoo wao

Kesi ya jack bado haijatolewa maamuzi ya mgao wa mali. Jack lazima apate tu sababu ni mke halali wa marehemu
 
Lakini mahakama imeona kuna sababu zenye mashiko. Ushauri kwa wanaume wasizikimbie ndoa zao. Wakumbuke NDOA ni NDOANO.

Hivi talaka zinaruhusiwa siku hizi? mama D

Makanisa mengi hayatoi talaka sababu kazi yao ni kupatanisha sio kuachanisha
Ila serikali ndio mmiliki wa watu na mali zao wakiwamo wanandoa. Na hawawezi kulazimisha maadui waendelee kuishi chini ya paa moja, maana huko ni kuhatarisha maisha ya wote wawili
 
Lakini mali si ni YENU--mke na mume? Ndoa hainaga EXPIRY DATE.

NDOA INAEXPIRE
Na viongozi wa dini wakifuatilia sheria na maandiko ndoa nyingi sana ni batili maana zimejaa zinaa.
Ukizini talaka ruksaaa

Mathayo 5:32​

Lakini mimi nawaambieni, anayempa mkewe talaka, isipokuwa kwa sababu ya uzinzi, anamfanya azini; na mwanamume akimwoa mwanamke aliyepewa talaka, anazini.
 
Zungumzia kwenye mali hapo pia mama D , because naona kama kuna mchezo unachezwa sana na hawa jinsia M :)
 
mama D, biblia inaruhusu talaka lakini hairuhusu uoe/uolewe na mtu mwingine tena. Yaani kama mmeachana basi kila mmoja abaki hivyo hivyo unless mmeweka mambo sawa inaruhusu kuoana tena (remarrying)

1 Corinthians 7:10-11
10 Lakini wale waliokwisha kuoana nawaagiza; wala hapo si mimi, ila Bwana; mke asiachane na mumewe;
11 lakini, ikiwa ameachana naye, na akae asiolewe, au apatane na mumewe; tena mume asimwache mkewe.
 
Tatizo linaanziaga kwa waoaji yaani watoa mahari yaani wanaume. Ukishakosea kujua kwamba mke bora ni moyo wake na ukajua rangi wala makalio makubwa ni sifa za nyongeza hutokaa ujute!!!! Tatizo tamaa inakua mbele😃😃😃

Mit 18:22​

Apataye mke apata kitu chema; Naye ajipatia kibali kwa BWANA.

MITHALI 31: 1-20​

Maneno ya mfalme Lemueli; mausia aliyofundishwa na mama yake
Ni nini, mwanangu? Tena ni nini, mwana wa tumbo langu? Tena, ni nini mwana wa nadhiri zangu? Usiwape wanawake nguvu zako; Wala moyo wako usiwape wale wawaharibuo wafalme.
Ee Lemueli, kunywa mvinyo hakuwafai wafalme, hakuwafai wafalme; Wala haifai wakuu waseme, Ki wapi kileo? Wasije wakanywa na kuisahau sheria, Na kuipotosha hukumu ya mtu aliye taabuni.

Mke mwema, ni nani awezaye kumwona? Maana kima chake chapita kima cha marijani.
Moyo wa mumewe humwamini, Wala hatakosa kupata mapato. Humtendea mema wala si mabaya, Siku zote za maisha yake.
Hutafuta sufu na kitani; Hufanya kazi yake ya mikono kwa moyo. Afanana na merikebu za biashara; Huleta chakula chake kutoka mbali.
Tena huamka, kabla haujaisha usiku; Huwapa watu wa nyumbani mwake chakula; Na wajakazi wake sehemu zao.
Huangalia shamba, akalinunua; Kwa mapato ya mikono yake hupanda mizabibu.
Hujifunga nguvu viunoni kama mshipi; Hutia mikono yake nguvu.
Huona kama bidhaa yake ina faida; Taa yake haizimiki usiku.
Hutia mikono yake katika kusokota; Na mikono yake huishika pia.
Huwakunjulia maskini mikono yake; Naam, huwanyoshea wahitaji mikono yake.

MWANZO 24​

Basi Ibrahimu alikuwa mzee mwenye miaka mingi, na Bwana alikuwa amembariki Ibrahimu katika vitu vyote. Ibrahimu akamwambia mtumishi wake, enenda hata nchi yangu, na kwa jamaa zangu, ukamtwalie mwanangu Isaka mke. Yule mtumishi akamwambia, Labda yule mwanamke hatakubali kufuatana nami mpaka nchi hii, je! Nimrudishe mwanao mpaka nchi ulikotoka? na yule mwanamke asipokubali kufuatana nawe, basi, utafunguliwa kiapo changu hiki; lakini usimrudishe mwanangu huko. Kisha huyo mtumishi akatwaa ngamia kumi katika ngamia za bwana wake akaenda zake, maana mali zote za bwana wake zilikuwa mkononi mwake, akaondoka, akaja mpaka Mesopotamia, mpaka mji wa Nahori.
Tazama! Nimesimama karibu na kisima cha maji, na binti za watu wa mjini wanatoka kuteka maji, basi na iwe hivi; yule msichana nitakayemwambia, Tua mtungi wako, nakuomba, ninywe; naye akasema, Unywe, nami nitawanywesha na ngamia zako pia; basi huyu na awe ndiye uliyemchagulia mtumishi wako Isaka; na kwa hayo nitajua ya kuwa umemfadhili bwana wangu.
Ikawa, kabla hajaisha kunena, tazama, Rebeka anatokea, binti wa Bethueli mwana wa Milka, mkewe Nahori, ndugu wa Ibrahimu, naye ana mtungi begani pake.
Naye yule msichana alikuwa mzuri sana uso wake, bikira, wala mwanamume hajamjua bado; akashuka kisimani, akajaza mtungi wake, akapanda.
Ndipo yule mtumishi akapiga mbio kwenda kumlaki, akasema, Tafadhali unipe maji kidogo katika mtungi wako ninywe.
Naye akasema, Unywe, bwana wangu, akafanya haraka, akatua mtungi wake mkononi mwake, akamnywesha.

Basi yule mtu akamkazia macho, akanyamaza, ili ajue kwamba Bwana ameifanikisha safari yake ama sivyo.
Ikawa, ngamia walipokwisha kunywa, yule mtu akatwaa pete ya dhahabu, uzani wake ulikuwa nusu shekeli, na vikuku viwili kwa mikono yake, uzani wake ulikuwa shekeli kumi za dhahabu, akasema, U binti wa nani wewe? Tafadhali uniambie. Je! Iko nafasi katika nyumba ya baba
 
Biblia inakataza kuachana isipokua kwa sababu ya zinaa.
Maachano yote yanakatazwa wala huruhusiwi kuoa au kuolewa tena.
Achano la kusababishwa na zinaa halijasema wewe uliyemwacha mzinzi ubaki hivyohivyo bila kuoa ila limesema atakayemuoa yule mzinzi uliyemwacha kwa talaka anazini. Kwahiyo adhabu ya mzinzi ni kutalikiwa na kubaki bila mwenza

Mali ni muhimu sana mama D
 
Back
Top Bottom