HIVI NI SIFA ZIPI UNATAKIWA UWE NAZO UITWE MTANZANIA ORIGINAL AU HALISI?

Bata batani

JF-Expert Member
Nov 11, 2011
3,215
3,682
hivi jamani naombeni kuuliza hivi ili uitwe mtanzania halisi au original unatakiwa uwe na sifa zipi ?

ninazungumza haya nikiwa nina kuna alikuwa akiniambia kama BABU YAKO ALITOKEA NCHI KAMA RWANDA,BURUNDI, CONGO UGANDA akaja kuishi tanzania akaziliwa Baba yako halafu ukazaliwa wewe hapo unatambukika wewe sio mtanzania halisi ?

kuna mwingine aliwahi niambia inatakiwa babu wa babu yake awe mzaliwa wa tanzania.

kuna mwingine aliwahi niambia kama umezaliwa tanzania bila kujali chimbuko lako ni wapi au unatokea wapi wewe tayali ni mtanzania na una sifa na haki zote .

kwa wale wanaojua mambo ya uraia hebu tupeni somo la uraia
 
Kwa mujibu wa katiba...na sheria za uraia wa tanzania kuna utanzania wa aina tatu
1.kuzaliwa
2.asili
3.kuasiliwa,kundikwa.

Ufafanuzi..

1.kama mmoja wa wazazi wako ni raia wa tanzania ama kwa kuzaliwa au kuasiliwa asili akakuza wewe akiwa tanzania basi wewe ni mtanzania kwa kuzaliwa.

2.Endapo mzazi wako ni raia wa tanzania ila anaishi nje ya nchi ya tanzania na akakuzaa wewe akiwa nje ya nchi basi wewe ni mtanzania kwa asili ila siyo kwa kuzaliwa.

3.endapo wazazi wako walihamia tanzania wakiwa si raia wa tanzania na kipindi wanakuzaa wewe walikua bado hawajapewa uraia wa tanzania inamaana na wewe huna sifa ya kuitwa mtanzania japo umezaliwa tanzania (hapa kuna hitaji marekebisho)sababu eti wazazi wako si raia wa tanzania ila wanaishi tanzania kwa maana hiyo nasi inabidi wazazi wako waombe uraia au wapewe uraia na wewe mwenyewe upewe uraia ndo upate kuitwa mtanzania..
Mfano wakimbizi wa burundi katika mikoa ya kigoma,tabora,ngara,kagerana katavi walipewa uraia mwaka 2015..wakati wamekaa nchini toka mwaka 1972 kwa maana hiyo watoto wao waliozaliwa mwaka 1972-2015 walikua hawatambuliki kama watanzania harali japo wamejaa kwenye kila sekta ya serkali kuanzia usalama wa taifa mpaka mjumbe wa nyumba kumi.

Mfano mwingine ni husseini Bashe mbunge wa nzega mjini yule bwana kazaliwa tanzania ila baba yake kazaliwa somalia kwahiyo kisiasa na kikatiba si mtanzania ila kiuhalisia ni mtanzania...japo ili apate ridhaa ya kugombea ubunge ilibidi aende wizara ya mambo ya ndani kuomba uraia..

Ila kama babu yako au baba yako alihamia tanzania na hakuna aliyegundua kua kahamia tanzania ataendelea kutambulika kama mtanzania na watoto wake kwa asili yao,kwa maana hiyo watanzania wa asili ni wale ambao mpaka tunapata uhuru na katiba ya tanzania walikua ndani ya mipaka ya tanzania na wakakubali kuitwa watanzania...na wale walioingia tanzania baada ya uhuru basi hawa ni wahamiaji na ili wawe watanzania inabidi wapewe uraia,baada ya kupewa uraia watoto watakaozaliwa baada ya hapo watakua raia kwa kuzaliwa.

Nimeeleza kidogo,ila sheria ya uraia tanzania ni ya kizamani sana...haivutii wageni kuja kuishi hapa kwetu ili watupe changamoto ya maendeleo.

Angalau wafanye kama marekani kwamba wewe ukizaliwa tu ndani ya marekani wewe ni mmarekani hata kama wazazi wako walikua wako njiani kwenda canada
 
Back
Top Bottom