Hivi ni sheria kwa mashirika ya ndege kutumia" US dola" kukata tiketi | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Hivi ni sheria kwa mashirika ya ndege kutumia" US dola" kukata tiketi

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by Mshume Kiyate, Jul 15, 2011.

 1. Mshume Kiyate

  Mshume Kiyate JF-Expert Member

  #1
  Jul 15, 2011
  Joined: Feb 27, 2011
  Messages: 6,774
  Likes Received: 22
  Trophy Points: 135
  Wana JF,

  Wenye kujua hivi kwa nini mashirika ya ndege kutoka nje ya nchi na mengine ya ndani ya kwenye huduma zao nyingi pamoja na kuuza tiketi lazima ununue kwa dola za kimarekani, baadhi ya mashirika hayo ni,
  Emirates Airline
  Ethiopian Airline
  Qatar Airways
  Swiss Air
  tena wameweka matangazo pesa inayotumika hapa ni dola za marekani tu, cha kushangaza ukifika sehemu kama China, Hong Kong, Dubai, ukienda kwa ma travel agents kukata tiketi ya kuja Tanzania ukiwapa dola za marekani wanakataa wanakuambia tunapokea pesa za nchi zao tu.
  Nawakilisha
   
 2. Mshume Kiyate

  Mshume Kiyate JF-Expert Member

  #2
  Jul 15, 2011
  Joined: Feb 27, 2011
  Messages: 6,774
  Likes Received: 22
  Trophy Points: 135
  Bei ya tiketi sasa hivi kwenda China, Ethiopian Dola 980, Emirates dola 1400,
  dola inavyozidi kupanda kila siku na watu wanazidi kuumia kwenye kununua tiketi
   
 3. D

  Danniair JF-Expert Member

  #3
  Jul 16, 2011
  Joined: Feb 18, 2011
  Messages: 361
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Asante kwa kuniunga mkono kilio changu cha siku nyingi juu ya jambo hili. Jamani tunao wabunge kama Zitto, naomba wenye simu zake awakilishe hoja hii kama hoja binafsi bungeni. Kwani mimi mwenyewe nimefika hata pale BOT nikawaulizia wachumi juu ya jambo hili. Lakini hawana lolote la kufanya zaidi ya kusema market value! Kwa wanasheria wao pia sheria yetu ya BOT kwao ni pambo tu. Ktk wanasheria wetu ni jaji mmoja tu ndiye aliongelea ktk kesi moja , kwa uzuri sana japo mwenzake alionekana kumpinga!!
   
 4. Anfaal

  Anfaal JF-Expert Member

  #4
  Jul 16, 2011
  Joined: Jan 19, 2010
  Messages: 1,157
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 0
  tatizo lipo wazi saana. Pesa yetu haiko stable kila siku inabadilika. Ndani ya mwaka huu peke yake imefluctuate karibu 15%. Sasa nani anaweza kucheza na currency ya hivyo? Pia pesa yetu haitumiki sehem nyingi, ipo very localised kwahiyo hakuna futures au forward contracts kutokana na mfumo wa soko kuwa duni na hivyo hakuna kampuni inayoweza kuhedge risks in case pesa yetu inaporomoka.
   
 5. Ritz

  Ritz JF-Expert Member

  #5
  Jul 16, 2011
  Joined: Jan 1, 2011
  Messages: 42,252
  Likes Received: 4,672
  Trophy Points: 280
  Mkuu, kwani pesa ya China, Hong Kong, Ethiopia, pesa zao zinatumika wapi zaidi ya nchi zao? Mbona kwenye nchi zao marufuku kutumia dola kununua tiketi za ndege, halafu kama ukezaji mbona hospitali za wawekezaji wanatumia pesa ya kwetu? Kwani sheria za BOT zinasemaje kuhusu kutumia pesa ya kigeni kwenye nchi yako
   
 6. Anfaal

  Anfaal JF-Expert Member

  #6
  Jul 16, 2011
  Joined: Jan 19, 2010
  Messages: 1,157
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 0
  Thanks kwa angalizo. Lakini ngoja nikukumbushe kuwa currency zinaweza kuwa fixed and floating. China wao ni fixed ingawa huwa wanaadjust mara moja moja. Sina hakika na Hong Kong but I think ni floating lakini ni mji ambao ni hub kwa international business na wana financial market za kueleweka na pesa yao inatumika saana. Sasa km currency inakuwa fixed inamaana hakuna fluctuation na hivyo hata bei hazibadiliki. Kwenye mahospital utakubaliana nami kwamba kule ni service based kuliko kwenye aircraft ambapo ni tofauti. Nadhani nimekujibu.
   
 7. Ritz

  Ritz JF-Expert Member

  #7
  Jul 16, 2011
  Joined: Jan 1, 2011
  Messages: 42,252
  Likes Received: 4,672
  Trophy Points: 280
  Nakubaliana na wewe baadhi ya maelezo yako, haya makampuni ya aircrat yanapanga bei kutoka na Currency cha kushangaza zaidi dola inaposhuka wao bado wana stick pale pale kwenye bei zao hawaitaji tena kuwa fixed mfano, Emirates airline mwezi juni walipandisha tiketi mpaka dola 1420 kwenda China sababu ya Currency leo Jul dola imeshuka bei bado zile zile fixed, na Ethiopia na hivyo hivyo kutoka dola 910, mpaka dola 980. vipi hapo haya makampuni ya airline yanafanya haki?
   
 8. Anfaal

  Anfaal JF-Expert Member

  #8
  Jul 16, 2011
  Joined: Jan 19, 2010
  Messages: 1,157
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 0
  well inayosukuma kupanda bei si dola peke yake. Kuna mafuta nk. Ni kweli mafuta sasa hv yamepungua lakini sasa hivi ndio majira ya utalii. Kuna nchi nilikuwepo kwakweli kusafiri miezi ya June-August basi iwe lazima kweli. Kwahiyo huu msimu sio wenyewe demand ni kubwa saana kwa airticket na ndio maana price zinakwenda juu.
   
 9. X-PASTER

  X-PASTER Moderator

  #9
  Jul 16, 2011
  Joined: Feb 12, 2007
  Messages: 11,651
  Likes Received: 105
  Trophy Points: 160
  Kwanza ungepaswa kusisitiza pale Airport/Border wageni wanao ingia wangetakiwa kulipa kwa pesa ya Tanzania na si Dollar, nimeshuhudia mwenye Kila mgeni mwenye Passport alikuwa anatozwa $100, na wale wenzangu na mie wenye Travel Document walikuwa wakitozwa $50.

  Ukiwa na Euro (€), UK Pound (£) au Yen (¥) au pesa ya nchi yoyote ile hawapokei.
   
 10. D

  Danniair JF-Expert Member

  #10
  Jul 16, 2011
  Joined: Feb 18, 2011
  Messages: 361
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  jamani haya mnayoyasema juu ya floating ina maana ni nchi yetu TU? Tuchangamke tusikalie viti na kusubiri mishahara tu.
   
 11. Ritz

  Ritz JF-Expert Member

  #11
  Jul 16, 2011
  Joined: Jan 1, 2011
  Messages: 42,252
  Likes Received: 4,672
  Trophy Points: 280
  Mkuu, lakini Serikali yetu inatakiwa kusimamia ili swala kuwalinda Wananchi wake unajua haya makampuni ata siku moja hawaweza kusema kama wanapenda faida, nakumbuka DSTV walivyotunyonya na matumizi ya dola kwenye huduma zao
   
 12. Mshume Kiyate

  Mshume Kiyate JF-Expert Member

  #12
  Jul 16, 2011
  Joined: Feb 27, 2011
  Messages: 6,774
  Likes Received: 22
  Trophy Points: 135
  Anfaal,Ebu toa mawazo yako kwenye ili suala kwa kuishauri serikali ya Tanzania, nahisi wewe kama ni Travel Airgents kwa jinsi unavyochangia unakula vichwa vya Guangzhou na Dubai, upo upande wa makampuni ya aircraft unatetea sana matumizi ya dola kwenye tiketi
   
 13. Anfaal

  Anfaal JF-Expert Member

  #13
  Jul 16, 2011
  Joined: Jan 19, 2010
  Messages: 1,157
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 0
  oh bahati mbaya sipo kwa hao agents. Mie napenda saana international business kuanzia currency, bonds na stock markets na performance ya countries pamoja individual companies. Kubwa hasa huwa sisahau theories na kuangalia kwenye uhalisia. Mie ni Mtanzania hasa na niliyependa nisafiri lkn sasa hv nauli inakimbiza saana mpaka demand itakapopungua. Lakini pia kwa wale wanaosafiri mara kwa mara kuna haja ya kustick kwenye airline moja na kuaccumulate miles ambapo baadae unaweza kupata offer ya kusafiri bure au hata kuwa upgraded.
   
 14. Mshume Kiyate

  Mshume Kiyate JF-Expert Member

  #14
  Jul 16, 2011
  Joined: Feb 27, 2011
  Messages: 6,774
  Likes Received: 22
  Trophy Points: 135
  Kweli, unachosema lakini kwa sasa hivi wafanya biashara wetu wengi wao wemekimbilia Ethopian airline kutokana bei chini, kupata offer ya tiketi lazima uwe na miles laki moja unaitaji usafiri zaidi ya mara sita kutoka Tanzania to China, kutoka Dar to Dubai miles 2800, Dubai to China miles nadhani miles 4800, na lazima kwanza card yako iwe Gold, inaitaji usafiri sana
   
 15. Saint Ivuga

  Saint Ivuga JF-Expert Member

  #15
  Jul 16, 2011
  Joined: Aug 21, 2008
  Messages: 39,349
  Likes Received: 19,530
  Trophy Points: 280
  viongozi wetu ni was***e
   
 16. Mshume Kiyate

  Mshume Kiyate JF-Expert Member

  #16
  Jul 16, 2011
  Joined: Feb 27, 2011
  Messages: 6,774
  Likes Received: 22
  Trophy Points: 135
  Mkuu, punguza jazba!
   
 17. Kibukuasili

  Kibukuasili JF-Expert Member

  #17
  Jul 16, 2011
  Joined: May 15, 2010
  Messages: 858
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 35
  hamna tofauti, hata wakitoza tzs bei itabadika kila siku tena kwa exchange rate wanayotaka wao. Nenda dstv uone. Usifananishe na nchi zenye viongozi
   
 18. Ritz

  Ritz JF-Expert Member

  #18
  Jul 16, 2011
  Joined: Jan 1, 2011
  Messages: 42,252
  Likes Received: 4,672
  Trophy Points: 280
  Mkuu, labda ujafanya utafiti uwezi kusema hata wakitoza Tsh bei aitobadikika sio kweli, usifanye mfano na DSTV bei yao inaweza kukaa miezi sita bila kupanda, dola kwa siku inaweza kupanda hata mara 4 kwa siku, unaweza kukuta asubuhi bei tofauti, mchana tofauti, jioni tofauti, watoze kwa Tsh tuone kama itapanda hivyo kama unavyosema tiketi ipande bei mara 4 kwa siku
   
 19. POSHO MAVYEO

  POSHO MAVYEO JF-Expert Member

  #19
  Jul 16, 2011
  Joined: Jun 28, 2011
  Messages: 377
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 0
  hata kama zitabadilika tatizo liko wapi lakini hii itasaidi sana kuondoa upuuzi kwenye pesa yetu wao wanaku dola na kuzibeba kwenye masanduku na kuondoka lakini kama watapewa shilingi itawalazimu kupitia BANK kutumia dola ni njia zao za wezi kuamisha pesa kirahisi
  ni hakika naninocho sema nimeona.
  wanakwwepa kodi pia kwa njia hii
   
 20. Anfaal

  Anfaal JF-Expert Member

  #20
  Jul 16, 2011
  Joined: Jan 19, 2010
  Messages: 1,157
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 0
  Nadhani kuna concept nyingine hapa haieleweki. Hapo hawakwepi fluctuation ya currency tu bali pia wanaangalia kwamba wakiwaambiwa mtoe kwa Tshs inamaana wakiwa wanafanya reptriation ya pesa zao itabidi kwanza wabadili kwenye USD then wakifika huko kwenye Rand. Hapo ni hasara kubwa kutokana na bid-ask spread kwahiyo hali hiyo wamewaachia nyie muhangaike nayo. Wakiamua kufanya hivyo inawezekana ila bei mtakayolipa inamaana mtacompensate administrative charges na costs nyingine za exchange rates.
   
Loading...