hivi ni sheria baadhi ya maofisa wa tanroad kutumia ofisi za serikali kuhujumu wananchi?

mumak

JF-Expert Member
Oct 24, 2013
1,069
661
ndugu wana jf siku chache zilizopita katika kata ya kawe mtaa wa mzimuni na ukwamani walipita baazi ya watu waliodai wanatoka tanroads hawa jamaa waliweka x nyumba zote zinazotezamana na barabara bila kutoa taarifa,wala kujari kama hii nyumba ipo nje ya hifadhi ya bara bara,siku ya pili wakaleta barua kudai ni notes sasa cha kushangaza hii barua ilitakiwa ipitie kwa viongozi kama vile mwenyekiti wa mtaa,diwani,na mkurugenzi wa manispaa chakushangaza ngazi zote hizo hawakupita,baada ya wananchi kufuatilia katika serikali zao za mitaa hadi kwa diwani,ndipo diwani alipo fuatilia kwa meneja mkuu wa tanroad wa mkoa,cha kushangaza zaidi hata huyo meneja wa mkoa hakujua swala hilo,pia hakuna agizo lolote lililotolewa la kuweka x nyumba za watu katika mitaa ya ukwamani na mzimuni,walipoulizwa baadhi ya maofisa mmoja akabainika kuwa niyeye alitoa agizo la kufanya hivyo kwa kuombwa na mmiliki mmoja wa nyumba ili amuondoe mtu alijenga mbele yake na kuomba msamaha,sasa tunajiuliza hivi ni sawa kwa mtu kama huyu aliye sababisha kuwatia hofu wananchi wa kawe na kuwafanya waichukie serikali yao kuomba msamaha tu ikatosha?pia kuna wananchi wangapi wanafanyiwa dhuruma kama hii kuwasababishia maradhi ya moyo na pia kuaribu biasharaza watu?source diwani kata ya kawe,
 
Back
Top Bottom