Hivi ni Service gani muhimu kwenye pikipiki?

Afisa Mteule Drj 2

JF-Expert Member
Mar 21, 2017
3,586
3,932
Wataalamu wa pikipiki ninaomba kujuzwa je ni service gani ambazo natakiwa kuzifanya mara kwa mara kwenye pikipiki ili kuhakikisha chombo kinakuwa salama muda wote.

Moja ya mambo unayohitaji kujua ni kwa mfano oil inatakiwa ibadilishwe baada ya muda gani.Naomba kuelimishwa vitu vyote vya muhimu kwenye service ya pikipiki.
 
Badili oil kila baada ya km 1000! Kabla ya kuendelea kukushauri, ni pikipiki gani unatumia? Maana ziko aina tofauti tofauti, kuna zingine zina oil filter n.k
 
Natumia pikpik aina ya TV'S nabadili oil ya total 20W50 kila baada ya kilometa 2000 sijutii kununua hii pikpik sijafungua enjini tangu ninunue mwaka unaelekea wa pili now
 
Ni boxer bm 150 mkuu,go on please

Kwa boxer basi hakikisha unatumia oil aina moja, yaani usiwe unabadilisha badilisha brand ya oil. Pia hakikisha kila unadilishapo oil basi badiki na oil filter, Yote hayo fanya kila baada ya km 1000 ili kukipa chombo uhai mrefu.

Kingine kama pikipiki yako ni kwa commercial use especialy bodaboda basi kumbuka kui grease pikipiki kila baada ya miezi 3 pamoja na kusafisha air cleaner.

ZINGATIA : kwenye uendeshaji usipendelee sana kutumia gia ndogo kwa mwendo mrefu hadi engine inalalamika, hakikisha uki flow gear kwa kuzingatia mlio wa engine na kuweka gia stahiki inayoendana na mwendo.

Ukizingatia hayo chuma itakaa hata miaka 10.

Mie boxee yangu inamiaka 4 sasa, ni ile ya gia 4 lakini ukichukua mo boxer leo pale kariakoo au tvs ukasema tuwekeane ligi basi hutaisogelea wala hutaiona.
 
Haha naona unaifagilia TVS yako mkuu,Hii yangu ni ya matembezi yangu mwenyewe sio bodaboda,Oil gani ni nzuri mkuu
 
Back
Top Bottom