Hivi ni sawa kwa mayahudi kukaa ktk ardhi wa palestina?

Status
Not open for further replies.
Pamoja na kwamba katika historia huwa kuna upotoshaji kwa namna moja au nyingine lakini mjadala wetu utaenda vizuri tutakapotumia rejea mbalimbali za vitabu vituku vya Mungu yaani Taurat, Injili,Zaburi na Quran.
Mimi nitaandika hisoria fupi ya wana wa israel,mayahudi na wazayuni kwa mujibu wa Quran ilivyoelezea.

Makao ya awali yalianzishwa Palestina katika miaka ya 14000 hadi 8000 KI (Kabla ya kuzaliwa kwa ‘Nabii ‘Iysa) kwa utawala wa Tatwafi. Na katika mwaka 8000 KI, mji wa Ariha (Jericho) ulianzishwa huko Palestina. Mji huo ulijengwa na wenyeji ukajengeka kwa njia ya mipango kama ilivyo miji ya kisasa.



Makabila ya mwanzo kuja kuweka makazi yao katika nchi ya Palestina ni yale makabila ya Wayebusi, Waamori, Wahiti, Wakanaani, Waamalika na Wafiniki. Makabila haya yalikaa katika maeneo tofauti ya nchi hiyo: Wakanaani waliweka makazi yao katika eneo la Gaza ilhali Wayebusi walibuni mji wa Yebus, ambao kwa sasa unajulikana kama mji wa al-Quds. Makabila haya yalihamia huko kutoka kusini mwa Bara Arabu takriban mwaka 3000 KI.



Katika mwaka wa 1900 KI, Nabii Ibraahim (‘Alayhis Salaam) alihamia kutoka Iraq na kuja kuweka makazi yake katika mji wa Khalil. Hapo ndipo alipomzaa Nabii Ismaa‘iyl na Ishaaq (‘Alayhimas Salaam) na baadaye kuzaliwa Nabii Ya‘quub (‘Alayhis Salaam).



Katika kipindi 1800 – 1600 KI, Palestina ilitawaliwa na Waheksosi. Ni katika kipindi hiki katika mwaka wa 1750 KI ndio Nabii Ya‘quub (‘Alayhis Salaam) alizaliwa.



Katika karne ya 16 KI (yaani mwaka wa 1580 KI), Bani Israili waliokuwa Misri walitiwa utumwani na Firauni wa wakati huo kuvamia na kuitawala Palestina kwa muda kabla ya sehemu hiyo kuingia katika utawala wa Kiislamu.



Mwaka 1250 KI, Nabii Musa (‘Alayhis Salaam) aliagiziwa na Allaah Aliyetukuka atoke Misri ambako wana wa Israili walikuwa ni watumwa waende wakaishi katika ardhi tukufu. Kwa ajili ya ukaidi wao (Qur-aan 5: 21 – 26), walipigwa marufuku kuingia katika ardhi hiyo. Mbali na hilo walipigwa adhabu kali ya kutangatanga katika jangwa kwa muda wa miaka arobaini (40). Katika kipindi hicho, wale wote waliokuwa wamebaleghe walikufa katika jangwa kikabakia kizazi ambacho kililelekea katika maadili ya Kiislamu, Imani na uchaji Mungu kuingia katika ardhi hiyo tukufu. Kizazi hicho kilipata darsa ya ukakamavu, utii, kujitolea mhanga na malezi bora, hivyo kwa tawfiki ya Allaah Aliyetukuka kuweza kuingia ardhi hiyo mwaka 1190 KI wakiongozwa na Yusha bin Nuun (‘Alayhis Salaam). Wakati huo tayari Nabii Muusa (‘Alayhis Salaam) alikuwa ameaga dunia hivyo kutoweza kuingia katika ardhi hiyo.



Yusha bin Nuun (‘Alayhis Salaam) ndiye mwana Israili wa kwanza aliyeanzisha dola katika maeneo ya Palestina. Hata hivyo, wana wa Israili chini ya uongozi wa Yusha bin Nuun (‘Alayhis Salaam) hawakuweza kuliteka eneo lote la Palestina katika mipaka yake ya sasa na hata mji wa al-Quds haukuingia mikononi mwake. Ifahamike kuwa dola hiyo haikuwa katika misingi ya Kiyahudi kwani dini ya Kiyahudi ilikuwa haijabuniwa kamwe wakati huo bali ilikuwa ikipekeshwa katika misingi ya Kiislamu.



Dola hii haikukaa kwa muda kwani vurugu liliingia kati baada ya kuaga dunia Yusha bin Nuun (‘Alayhis Salaam), hivyo kushikiliwa na Ma-Qaadhi kabla ya kusambaratika kabisa kabisa. Kufikiwa na hayo, Bani Israili waliingia katika utawala wa Wapalestina ambayo asili yao ni Wakanaani. Kudhalilishwa kwao huko kuliwafanya watake msaada kutoka kwa Allaah Aliyetukuka ili warudi katika enzi zao (Qur-aan, 2: 246). Allaah Aliyetukuka Aliwateulia Twaaluut kuwa mfalme wao wa kuwaongoza wao kwenda kupambana na Wapalestina wakiongozwa na Jaaluut (Qur-aan, 2: 247). Bani Israili waligomba sana kuhusu uchaguzi huo, hata hivyo wapo waliokuwa na Imani ambao walisalimu amri na kujizatiti kwenda kupambana na Wapalestina. Wakati huo, Nabii Daawuud (‘Alayhis Salaam) alikuwa kijana mdogo aliyejiunga na jeshi hilo ambalo kwa tawfiki ya Allaah Aliyetukuka liliweza kulishinda jeshi la Jaaluut (Qur-aan, 2: 248 – 251). Ushindi huo ulipatikana mwaka wa 1025 KI. Twaaluut aliweza kuanzisha tena dola ya Kiislamu Palestina ikiwa inaongozwa na Bani Israili mpaka kufa kwake mnamo 1004 KI.



Baada ya kuaga dunia tu, hatamu za uongozi zilishikwa na Nabii Daawuud (‘Alayhis Salaam) ambaye aliipanua dola hiyo kwa kasi kubwa sana. Ni wakati wake ndio mji wa al-Quds uliweza kutekwa. Nabii Daawuud (‘Alayhis Salaam) aliaga dunia mwaka wa 960 KI na kumuacha mtoto wake, Nabii Sulaymaan (‘Alayhis Salaam) katika utawala. Kwa upande wake naye, Nabii Sulaymaan (‘Alayhis Salaam) aliipanua dola hiyo lakini haikufika katika mipaka yake ya sasa. Nabii Sulaymaan (‘Alayhis Salaam) aliimarisha sana dola hiyo, akiwa yeye na babake wameitawala kwa misingi ya Kiislamu. Ilibaki hivyo hadi mwaka wa 922 KI pale naye alipoaga dunia.



Kufariki kwake kuliifanya dola hiyo igawanywe sehemu mbili: Dola ya Yuda (kusini) na Israili (kaskazini). Bani Israili waligawanyika katika koo zao kwa kiasi ambacho walianza kupigana wao kwa wao (baina dola mbili hizo) na ufisadi ukakithiri kwa kiasi kikubwa sana. Wakati huo ndio alitokea mtu kwa jina la Yuda aliyekiuka mipaka ya Dini na kuasi. Alipata wafuasi wengi na hapo kukazaliwa Dini ya Uyahudi.



Hali hiyo halisi ya mapambano baina ya Bani Israili iliwapelekea dola zao mbili hizo kudhoofika na mwisho katika mwaka wa 722 KI, dola ya Israili ilianguka na eneo hilo kutawaliwa na Wa-Asiria. Nayo dola ya Yuda ilivamiwa na mfalme Nubukadneza wa Babeli (Iraq) mwaka 586 KI, na dola hiyo kuingia katika utawala wa Kibabeli. Wana wa Israili wote walipelekwa uhamishoni huko Iraq kama watumwa. Hapo wengine wao walipata kukimbia na kuingia Ufursi (Iran) ambapo walijaribu kufanya mahusiano ya karibu na utawala wa huko hadi wakamtoa msichana wao kwa ajili ya kuolewa na mfalme wa Iran. Mafungamano hayo yalimfanya mfalme Cyrus wa Iran aunde jeshi kwa usaidizi wa Mayahudi ili kuivamia Palestina na kuwang’oa Wababeli. Cyrus alifanikiwa kuwashinda Wababeli kutoka Palestina na kuwapatia ruhusa Mayahudi kurudi katika nchi hiyo lakini hata hivyo waliorudi hawakuwa wengi, walikuwa wachache sana. Wengi miongoni mwao walibakia katika nchi ya uhamisho wao. Kushinda kwao kulitokea mwaka wa 538 KI. Hata hivyo, Mayahudi wakati wa utawala wa Kifursi hawakuwa na mamlaka wala madaraka yoyote lakini walipatiwa uhuru wa kufanya Ibadah zao bila kufuatiliwa, kuingiliwa wala kubughudhiwa na Wafursi.



Na katika mwaka 332 KI, Palestina ilivamiwa na kutekwa na Warumi wakiongozwa na Alexander kutoka Macedonia. Hata hivyo, Warumi hawakuweza kukaa huko kwa muda mrefu pale wafalme wa kutoka Syria walipovamia sehemu hiyo na kuitia katika utawala wao mwaka 198 KI.



Wayunani nao waliiteka ardhi hiyo mwaka wa 175 Ki na kuitawala. Mayahudi waliweza kujizatiti na kuiteka sehemu hiyo ya ardhi mwaka wa 166 KI na ikabaki mikononi mwao kwa kipindi cha miaka 4. Wasyria walirudi tena kwa kishindo na kuwashinda Mayahudi mwaka wa 162 KI. Hata hivyo, nao Mayahudi walijizatiti kwa mara nyingine tena wakaja wakawang’oa Wasyria kutoka sehemu hiyo mwaka 143 KI. Hapo waliweza kuibakisha ardhi hiyo katika utawala wao hadi mwaka 70 KI.



Kwa miaka saba baada ya huo mwaka wa 70 kukawepo vurugu kubwa hadi mwishowe Warumi wakaweza kuwashinda Mayahudi mnamo 63 KI. Kuanzia mwaka huo hadi mwaka wa 616 BI (Baada ya kuzaliwa kwa Nabii ‘Iysa) Palestina ilibaki katika utawala wa Warumi isipokuwa kile kipindi cha mapinduzi ya Mayahudi cha mwaka 66 BI na 132 – 135 BI. Hata hivyo, katika kipindi cha mapinduzi hayo ya Mayahudi serikali ya Roma ilituma wanajeshi wake wengi ili kuyasagasaga hayo mapinduzi. Ni wakati huo ndio serikali ya Kirumi ilipitisha sheria kuwa mji wa al-Quds haufai kukaliwa na Mayahudi.



Utawala wa Kirumi ulisitishwa kidogo na ule wa Wafursi mwaka wa 616 BI. Lakini utawala wa Wafursi haukukaa kwa muda mrefu kwani katika mwaka wa 624 BI walishindwa na Warumi katika vita ambavyo Allaah Amevizungumzia katika Suratur Ruum (30): Aayah 1 – 5. Warumi waliweza kusonga mbele hadi kuuteka mji wa al-Quds katika kipindi cha muda miaka 3 hadi 4.



Kipindi baada ya Sulhu ya Hudaybiyah ndicho kile ambacho Mtume Muhammad (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) alianza kupeleka barua kwa mataifa mbali na ndio barua hiyo ikamfikia mfalme wa Warumi, Hiraql (Heraclius) akiwa al-Quds mwaka wa 628 BI. Hapo ndio yalianza mapambano baina ya Waislamu wakiongozwa na Mtume (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) na Warumi. Mji wa al-Quds uliingia mikononi mwa Waislamu wakati wa ukhalifa wa 'Umar bin al-Khatwtwaab (Radhiya Allaahu ‘anhu) ambaye alifunga safari kwenda kuchukua funguo za mji kutoka kwa kasisi Sophronius mwaka wa 638 BI na hapo miji mingi ya Palestina ikaingia katika Dola ya Kiislamu. Nchi hiyo pamoja na nchi za Shaam zote zilibakia katika utawala wa Kiislamu hadi mwaka wa 1099 BI wakati ambapo Wakristo walikuja kuzivamia ardhi hizo katika vita vya Msalaba.



Watu wa Msalaba kutoka bara Ulaya waliweza kuwaua Waislamu 70,000 ndani ya eneo la Msikiti wa Aqswa. Wakristo waliweza kuitawala ardhi hiyo kwa muda wa miaka 88 ambapo harakati za kuikomboa zilipamba moto. Harakati hizo zilianzishwa na Nuurud-Diyn Zinkiy, mwanae Nuurud-Diyn Mahmuud na baadaye Swalaahud-Diyn Hasan al-Ayyuubiy ambaye aliweza kwa tawfiki ya Allaah kuirudisha Palestina kuwa katika Dola ya Kiislamu mwaka 1187 BI.



Kuanzia mwaka huo wa 1187 BI, Palestina ilibakia kuwa katika Dola ya Kiislamu hadi baada ya Vita vya Kwanza vya Dunia (1917) ndio Palestina iliingia katika utawala wa Uingereza. Wenyeji wa al-Quds hawakusadiki masikio yao pale walipokusanyika kumsikiliza jemadari Allenby katika uwanja wa al-Quds. Allenby alisema kwa uwazi kabisa: “Leo ndio vita vya Msalaba vimekwisha”. Kabla hata ya kuiteka na kuitawala ardhi hiyo, serikali ya Uingereza tayari ilikuwa imewaahidi Wazeyuni kuwa wakiondoka watawazawadia wao kipande hicho cha ardhi. Hayo yanapatikana katika ahadi au tangazo la Waziri wa Nje, Arthur James Balfour ya tarehe 2 Novemba 1917.



Na kweli kwa ahadi yao, Uingereza ilipoondoka Mei 1948 waliwaachia ardhi hiyo Wazeyuni wasiokuwa na mafungamano na ardhi hiyo. Hakika ni kuwa Mayahudi wakati huo na kabla ya hapo hawakuwa na kitambulisho cha aina yoyote ile. Hii ni kwa mujibu wa barua aliyoiandika Dkt Chaim Weizman ya 18 Aprili 1918 kwa mkewe: “Ni masikitiko makubwa kuona kuwa hapa hatuna chochote. Hapa hakuna hata taasisi moja ya Kiyahudi, lakini kumejaa minara (kumaanisha wingi wa Misikiti)”.



Ndugu zetu walianzisha harakati ya kutaka kujikomboa na minyororo ya ukoloni. Harakati ya kwanza ni ile iliyoongozwa na Sh. Abdul-Qaadir al-Qassaam, kutoka Syria mwaka 1925. Mwaka wa 1929 kulikuwa na Intifadha ya al-Buraaq, naye Sh. Al-Qassaam akauliwa mwaka wa 1935 alipokuwa anapambana na jeshi la Muingereza katika maeneo hayo matakatifu.



Kuanzia mwaka wa 1948, kumekuwa na vita baina ya Waarabu na Wazeyuni, lakini Waarabu wakashindwa sana kwa kutokuwa na kiongozi mmoja, kutokuwa na mipango mizuri na wakati mwingine kushirikiana na dola haramu ya Israili. Hata hivyo, sababu kubwa ya kushindwa ni kule Waarabu kuichukulia kuwa hiyo ni kadhiya ya Waarabu tu na kutowajumuisha Waislamu wengineo.


Mkuu kwa wale Watu Wa zamani walikua na Imani gani?
Maana tunaona uislam unakuja baada ya mtume kuja?
 
Kwa maana hiyo wayahudi wanagombea ardhi ya parestina pasipo muongozo wa Mungu

sio kwamba wayahudi wanagombea ni kwamba mgogoro mzima unaenda kwa kufuata willing za watu kila wanavyotaka kwa matakwa yao si kwamba wahudi wanagombea bila muongozo wa Mungu. Ikumbukwe kwamba mgogoro wa nchi hii ndo uta- trigger vita ya mwisho wa dunia
 
PAMOJA SANA!MWENDA KWAO SI MTUMWA!WAYAHUDI SI WAARABU SO ILE ARDHI NI YA WAYAHUDI SO WALE WAPALESTINA WALEJEE KWENYA NCHI ZA MAARABU HARAKA.NADHANI SIKU IPO GAZA NA UKINGO WA MAGHARIB pia JERUSALEM ITAKUJA KUWA MJI MKUU WA ISRAEL.MUNGU IBARIKI ISRAEL TAIFA TEULE.
 
Mkuu Adisamigo Taratibu Mkuu!
Punguza kutoa maneno makali! Hii mada ni nzuri kujadili Lakini kwa mfumo huu Wa kutoa maneno itapelekea hii Mada kufungwa!
Tujadili Taratibu na kufahamishana kwa Taratibu Lakini kuanza kutoa maneno tu kwa wenzio haikai vizuri!
Ntuzu hakuna mtu anabisha topic hi nzuri, tatizo lina kuja mtu anapo kosea nakuanza kuleta udini ,na wakati hajui dini. Hapo lazima tumfunze dini tena kwa adabu hatuongei isipokuwa ukweli mtupu.

Niliye mjibu ndio alileta udini na alianza kusema Hagar na mwanae Ishamel walifukuzwa, ndio nikajibu. Lazima ajuwe wazi hakuna aliye mfukuza Hagar, si Sara wala si Ishaq, Hagar aliondoka pale kwa amri ya Mungu, kila kitu kilochotekea ni mipango ya Mungu.
 
Mkuu kwa wale Watu Wa zamani walikua na Imani gani?
Maana tunaona uislam unakuja baada ya mtume kuja?

Watu wa zamani wa sehemu gani? Kama ni ulimwenguni kwote watu walikuwa na dini zao tofauti tofauti na uislamu ukiwemo na si kweli kwamba uislamu umekuja baada ya Mtume Muhammad SAW kuja hebu rejea hapa katika maneno ya Ibrahim baba wa Mitume,
(( رَبَّنَا وَاجْعَلْنَا مُسْلِمَيْنِ لَكَ وَمِن ذُرِّيَّتِنَا أُمَّةً مُّسْلِمَةً لَّكَ وَأَرِنَا مَنَاسِكَنَا وَتُبْ عَلَيْنَآ إِنَّكَ أَنتَ التَّوَّابُ الرَّحِيمُ))

((Ewe Mola Mlezi wetu! Tujaalie tuwe ni wenye kusilimu Kwako, na pia miongoni mwa vizazi vyetu wawe umma uliosilimu Kwako. Na Utuonyeshe njia za ibada yetu na Utusamehe. Bila shaka Wewe Ndiye Mwenye kusamehe Mwenye kurehemu)) [Al-Baqarah: 128]
“Na kwa hakika kwa kila ummah Tuliutumia Mtume kwamba: Muabuduni Allah, na muepukeni Shetani (na miungu wasio wa kweli)” (16: 36).

Naomba hii isiwe maada.
 
PAMOJA SANA!MWENDA KWAO SI MTUMWA!WAYAHUDI SI WAARABU SO ILE ARDHI NI YA WAYAHUDI SO WALE WAPALESTINA WALEJEE KWENYA NCHI ZA MAARABU HARAKA.NADHANI SIKU IPO GAZA NA UKINGO WA MAGHARIB pia JERUSALEM ITAKUJA KUWA MJI MKUU WA ISRAEL.MUNGU IBARIKI ISRAEL TAIFA TEULE.

Unadhani hili ulizungumzalo litatokea kweli au ni ndoto? Hebu soma historia ndani ya vitabu vya Mungu halafu uone suruhu ya ishu ya Palestina na Israel itakuwaje?
 
Mkuu kwa wale Watu Wa zamani walikua na Imani gani?
Maana tunaona uislam unakuja baada ya mtume kuja?
There were many prophets before Muhammad (pbuh) including: Adam, Noah, Abraham (Ibrahim), Ishmael, Isaac, Jacob, Joseph, Job, Moses (Musa), Aaron, David, Solomon, Elias. The heart of faith for all Muslims is obedience to Allah's will.


Ukristo umeletwa na Paulo jamani mbona hamtaki kusikia, nileteni wapi Yesu alisema dini yake Ukristo, mkileta mimi takuwa wakwanza kuwa mkristo kuanzia sasa hivi. Yesu mwenyewe anasema wanao abudu kwenye kanisa ni mashetani na nyie bado mnabisha tu.
 
Wakristo acheni kutunga uongo nani aliye mfukuza Hajar? Hajar kwa Mungu anaheshimiwa kuliko Sara sababu ni mwanamke peke yake aliye ongea na malaika wa Mungu kabla ya hata mama yake Yesu kuongea na malaika wa Mungu.

Na nani anaye wadanganya alifukuzwa wakati Ishaq kazaliwa, Hajar na Prophet Ismael waliondoka pale wakati bado sana Prophet Ishaq kuzaliwa, Bibilia zenu zimebaki kutunga uwongo tu.

Hajar alipoenda Saud Arabia ni amri ya Mungu, sababu Mungu alikuwa ana sababu zake kuonyesha uislam ndio dini ya kweli.

Hajar alipo ondoka alikuwa na mwanae Prophet Ismael, na wakati Ismael akilia malaika wa Mungu walikuwa wanakuja kumbembeleza kama hamjui.

Mtoto wa huyo mnasema mjakazi ndio alipewa jina na Mungu, kabla ya mwingine ambaye anaitwa Yakoub (Jacoub) au kama alivyo itwa na Mungu Isra'il.

Kwa hio mnapo ongelea Prophet Ismael lazima muweke heshima sana, ni Prophet peke aliye letwa duniani kapewa jina na Mungu na mama yake kaongea na malaika wa Mungu direct.

Kama yuko Prophet wa namna hio basi atakuwa ana kimoja tu sio vyote viwili, ambao ni mama wa Yesu ndio aliongea na malaika wa Mungu, na Prophet Yakoub ambaye anajulikana kama Isra'il, ndio aliye kuwa Prophet wa pili kuitwa jina na Mungu bada ya Prophet Ismael.

Kumbukeni siku zote Mungu angekuwa ana akili kama zenu wakristo, basi asinge msogelea Prophet Ismael kwa njia mbili, ya kumpa jina na kumtukuza mama yake kwa kuongea na malaika wake.

Mtabaki tu na ujinga wenu wakristo mpaka siku za kiyama, ndio matajua uwongo mlio mtungia Prophet Ismael, kama kazaliwa nje ya ndoa au alizaliwa kwenye ndioa ya halali. Si mnaona hata Bibilia zenu zinavyo kanyagana, mara zina sema Hajar ni mke halali wa Prophet Ibrahim ,mara zinasema Prophet Ibrahim ali sex nje ya ndoa hahaha.

Kweli wakristo hamnazo, mpaa kipenzi cha Mungu Prophet Ibrahim mkasema alizini nje ya ndoa, hapo kweli manenda peponi wote na waislam tunaenda motoni hahaha.


(Gen 21:6 [NET])
Sarah said, “God has made me laugh. Everyone who hears about this will laugh with me.”

(Gen 21:7 [NET])
She went on to say, “Who would have said to Abraham that Sarah would nurse children? Yet I have given birth to a son for him in his old age!”

(Gen 21:8 [NET])
The child grew and was weaned. Abraham prepared a great feast on the day that Isaac was weaned.

(Gen 21:9 [NET])
But Sarah noticed the son of Hagar the Egyptian – the son whom Hagar had borne to Abraham – mocking.

(Gen 21:10 [NET])
So she said to Abraham, “Banish that slave woman and her son, for the son of that slave woman will not be an heir along with my son Isaac!”

(Gen 21:11 [NET])
Sarah’s demand displeased Abraham greatly because Ishmael was his son.

(Gen 21:12 [NET])
But God said to Abraham, “Do not be upset about the boy or your slave wife. Do all that Sarah is telling you because through Isaac your descendants will be counted.

(Gen 21:13 [NET])
But I will also make the son of the slave wife into a great nation, for he is your descendant too.”

(Gen 21:14 [NET])
Early in the morning Abraham took some food and a skin of water and gave them to Hagar. He put them on her shoulders, gave her the child, and sent her away. So she went wandering aimlessly through the wilderness of Beer Sheba.

(Gen 21:15 [NET])
When the water in the skin was gone, she shoved the child under one of the shrubs.

(Gen 21:16 [NET])
Then she went and sat down by herself across from him at quite a distance, about a bowshot away; for she thought, “I refuse to watch the child die.” So she sat across from him and wept uncontrollably.

(Gen 21:17 [NET])
But God heard the boy’s voice. The angel of God called to Hagar from heaven and asked her, “What is the matter, Hagar? Don’t be afraid, for God has heard the boy’s voice right where he is crying.

(Gen 21:18 [NET])
Get up! Help the boy up and hold him by the hand, for I will make him into a great nation.”

(Gen 21:19 [NET])
Then God enabled Hagar to see a well of water. She went over and filled the skin with water, and then gave the boy a drink.

(Gen 21:20 [NET])
God was with the boy as he grew. He lived in the wilderness and became an archer.

(Gen 21:21 [NET])
He lived in the wilderness of Paran. His mother found a wife for him from the land of Egypt
.
 
Mayahudi wamevamia ardhi ya wapalestina na mpaka leo wanawanyanyasa waarabu na kuwatesa. Kihistoria mayahudi ndio wakazi wa asili wa ardhi hii ya Palestina. Kifupi naweza kusema mayahudi wamerudi nyumbani kwao baada ya kukaa ugenini kwa miaka mingi. Yaani namaanisha leo hii Wangoni waamue kurudi South Africa ambako ndio asili yao,Wazigua warudi Somalia ambako kihistoria ndio asili yao, washihiri warudi kwao Yemen, makuburu nao warudi kwao, n.k

Je, watu kama hao niliowataja wakitaka kurudi nyumbani kwao watapokelewa na je wanahaki ya kuwapokonyonya ardhi wale watakao wakuta kwa hoja kwamba sisi ndio mababu zetu waliishi hapa?
Simply mwenzangu na mimi nikukute hapo unapoishi na familia yako imeshakaa miaka zaidi ya mia tatu, je hapo utaondoka na hata nikiwa sina document zozote zinazoonyesha kuwa mimi ndio ninaemiliki?

AKHSANTENI.

we waache tu hao watu bana, they are elected nation, piga ua garagaza, unpingikable, hawa jamaa hawalaaniki, hata wakisomewa itikaf mara milioni haiwapati. cha msingi ni kuwabariki tu. fulu stopu..waisrael hawajavamia wamerudisha chao na bado wata extend mpaka iran.
 
Israel itabaki kuwa taifa teule tu hata wenye wanaofuga midevu baada ya akili wanajua kuwa;israel maana yake nn walejee kitabu chao cha shetan so wao wamepewa mafuta israel akili.tusibishane na majuha coz wanataka watuaminishe ujinga wao.
 

(Gen 21:6 [NET])
Sarah said, "God has made me laugh. Everyone who hears about this will laugh with me."

(Gen 21:7 [NET])
She went on to say, "Who would have said to Abraham that Sarah would nurse children? Yet I have given birth to a son for him in his old age!"

(Gen 21:8 [NET])
The child grew and was weaned. Abraham prepared a great feast on the day that Isaac was weaned.

(Gen 21:9 [NET])
But Sarah noticed the son of Hagar the Egyptian – the son whom Hagar had borne to Abraham – mocking.

(Gen 21:10 [NET])
So she said to Abraham, "Banish that slave woman and her son, for the son of that slave woman will not be an heir along with my son Isaac!"

(Gen 21:11 [NET])
Sarah's demand displeased Abraham greatly because Ishmael was his son.

(Gen 21:12 [NET])
But God said to Abraham, "Do not be upset about the boy or your slave wife. Do all that Sarah is telling you because through Isaac your descendants will be counted.

(Gen 21:13 [NET])
But I will also make the son of the slave wife into a great nation, for he is your descendant too."

(Gen 21:14 [NET])
Early in the morning Abraham took some food and a skin of water and gave them to Hagar. He put them on her shoulders, gave her the child, and sent her away. So she went wandering aimlessly through the wilderness of Beer Sheba.

(Gen 21:15 [NET])
When the water in the skin was gone, she shoved the child under one of the shrubs.

(Gen 21:16 [NET])
Then she went and sat down by herself across from him at quite a distance, about a bowshot away; for she thought, "I refuse to watch the child die." So she sat across from him and wept uncontrollably.

(Gen 21:17 [NET])
But God heard the boy's voice. The angel of God called to Hagar from heaven and asked her, "What is the matter, Hagar? Don't be afraid, for God has heard the boy's voice right where he is crying.

(Gen 21:18 [NET])
Get up! Help the boy up and hold him by the hand, for I will make him into a great nation."

(Gen 21:19 [NET])
Then God enabled Hagar to see a well of water. She went over and filled the skin with water, and then gave the boy a drink.

(Gen 21:20 [NET])
God was with the boy as he grew. He lived in the wilderness and became an archer.

(Gen 21:21 [NET])
He lived in the wilderness of Paran. His mother found a wife for him from the land of Egypt
.
We fatilia tu hizo Quote ulizo weka uona Bibilia inavyosema uwongo, Ismail kaondoka pale kabla ya Ishaq kuzaliwa sababu alikuwa bado ananyonya, sa hio sijui Mocking his brother alikuwa ana umri gani Ismail?

Tazama Quran Chatper 37 Surah Saafaat verses 100-112:100 ...(And Ibraheem (a.s.) prayed;;) "O my Lord! grant me a righteous (son)!"101 So We gave him the good news of a boy (Ismail (a.s.), ready to suffer and forbear. 102 Then when (Ismail (a.s.)) reached (the age of serious) work with him he (Ibraheem (a.s.)) said: "O my son! I see in vision that I offer thee in sacrifice: now see what is thy view!" (Ismail (a.s.)) said: "O my father! Do as thou art commanded: thou will find me if Allah so wills one practicing patience and constancy!"103 So when they had both (Ibraheem (a.s.) and Ismail (a.s.)) submitted their wills (to Allah), and he (Ibraheem (a.s.)) had laid him (Ismail (a.s.)) prostrate on his forehead (for sacrifice),104 We called out to him "O Ibraheem! 105 Thou hast already fulfilled the vision!"; thus indeed do We reward those who do right.106 For this was obviously a trial107 And We ransomed him (Ismail (a.s.)) with a momentous sacrifice: 108 And We left (this blessing) for him among generations (to come) in later times: 109 "Peace and salutation to Ibraheem!"110 Thus indeed do We reward those who do right.111 For he was one of Our believing servants.112 And We gave him the good news of Ishaaq, a Prophet, one of the Righteous.
 
ISRAEL WANASAMBARATIKA KWA MARA YA KWANZA

Israel walikuwa makabila 12 na walipofika pale wakaanza kuiga desturi za watu walio wazaunguka mabao walikuwa na wafalme. basi nao wakataka kutawaliwa kwa mfumo huo. BWANA akawaruhusu ingawa kwa kuwakasirikia. wakatawaliwa na Saul ambaye alikuwa mbenjamini. alipotawala alikuwa hana hofu ya Mungu yaani alikuwa anawaogopa wanadamu kuliko Mungu BWANA akamkataa na ndo ukawa mwanzo wa Daudi kutoka kabila la Yudah. kumbuka ufalme ulikua unaenda kwa kufata Order (uzao- baba, mwana, mjukuuu....)
Daudi alipofariki yale mwataifa 11 yakatunga hila kwamba hili kabila ambalo mfalme ndo anatokea anawakandamiza kwa hiyo wakaamu kutokutawaliwa na mfalme wa Yuda. walipojitenga ndo ikatokea Israel ya Uyahudi ambayo makao yake makuu ilikua Jerusalem (Mji wa Daudi) ambao Daudi aliutwaa katika vita na kunnuua kiwanja cha Haruna Myebusi na kujenga madhabahu hapo (Ndipo lilipojengwa Hekalu)
yale mataifa 11 ya ambayo makao yake yalikuwa samaria walimwasi BWANA sana kwa kufuata desturi za mataifa yaliyowazunguka kwa hiyo wakawa victim wa kufukuzwa katika nchi kwa kutwaliwa utumwani.
Taifa lilikuwa limebaki ni Yuda ambao nao walianza kunyanyasana wao kwa wao, BWANA kwa kupitia kwa mtumishi wake Yeremia Nabii aliwaambia atawafukuza pia waende utumwani wasipobadilika (this time Babylon). kumbuka hili taifa la Yuda peke yake ndo BWANA alikuwawa amebaki nalo kwa maana ya kulinda ahadi yake na Ibrahim.

(Jer 26:2 [NET])
The LORD said, “Go stand in the courtyard of the LORD’s temple. Speak out to all the people who are coming from the towns of Judah to worship in the LORD’s temple. Tell them everything I command you to tell them. Do not leave out a single word!

(Jer 26:3 [NET])
Maybe they will pay attention and each of them will stop living the evil way they do. If they do that, then I will forgo destroying them as I had intended to do because of the wicked things they have been doing.

(Jer 26:4 [NET])
Tell them that the LORD says, ‘You must obey me! You must live according to the way I have instructed you in my laws.

(Jer 26:5 [NET])
You must pay attention to the exhortations of my servants the prophets. I have sent them to you over and over again. But you have not paid any attention to them.

(Jer 26:6 [NET])
If you do not obey me, then I will do to this temple what I did to Shiloh. And I will make this city an example to be used in curses by people from all the nations on the earth.’”


Nani mwenye haki ya kuishi ndani ya ardhi ya Palestina kati ya muarabu na myahudi?.
 
we waache tu hao watu bana, they are elected nation, piga ua garagaza, unpingikable, hawa jamaa hawalaaniki, hata wakisomewa itikaf mara milioni haiwapati. cha msingi ni kuwabariki tu. fulu stopu..waisrael hawajavamia wamerudisha chao na bado wata extend mpaka iran.

Hapa umezungumza kiushabiki zaidi bila kuangalia upana wa hili sakata.
 
Nani mwenye haki ya kuishi ndani ya ardhi ya Palestina kati ya muarabu na myahudi?.

huu mgogoro uko spiritual ndo maana on one of my accounts kwenye kile kitabu cha Daniel 12, Daniel aliambiWa 'close the book till the time of the end'. ila kimsingi ni nchi ya wayahudi na ni haki yao kabisa ila dhambi zao ziliwaondoa na mpango wa kuwarudisha pale ni wa Mungu kwani tunaambiwa watarudi na kuimiliki nchi yao na watajenga hekalu palepale pa mwanzo ambapo ndo kwenye huyo msikiti Aqsa
 
Israel itabaki kuwa taifa teule tu hata wenye wanaofuga midevu baada ya akili wanajua kuwa;israel maana yake nn walejee kitabu chao cha shetan so wao wamepewa mafuta israel akili.tusibishane na majuha coz wanataka watuaminishe ujinga wao.
Anaye sema Israel taifa teule lazima atakuwa kondoo walio potea.
 
We fatilia tu hizo Quote ulizo weka uona Bibilia inavyosema uwongo, Ismail kaondoka pale kabla ya Ishaq kuzaliwa sababu alikuwa bado ananyonya, sa hio sijui Mocking his brother alikuwa ana umri gani Ismail?

Tazama Quran Chatper 37 Surah Saafaat verses 100-112:100 ...(And Ibraheem (a.s.) prayed;;) "O my Lord! grant me a righteous (son)!"101So We gave him the good news of a boy (Ismail (a.s.), ready to suffer and forbear. 102Then when (Ismail (a.s.)) reached (the age of serious) work with him he (Ibraheem (a.s.)) said: "O my son! I see in vision that I offer thee in sacrifice: now see what is thy view!" (Ismail (a.s.)) said: "O my father! Do as thou art commanded: thou will find me if Allah so wills one practicing patience and constancy!"103So when they had both (Ibraheem (a.s.) and Ismail (a.s.)) submitted their wills (to Allah), and he (Ibraheem (a.s.)) had laid him (Ismail (a.s.)) prostrate on his forehead (for sacrifice),104We called out to him "O Ibraheem! 105Thou hast already fulfilled the vision!"; thus indeed do We reward those who do right.106For this was obviously a trial107And We ransomed him (Ismail (a.s.)) with a momentous sacrifice: 108And We left (this blessing) for him among generations (to come) in later times: 109"Peace and salutation to Ibraheem!"110Thus indeed do We reward those who do right.111For he was one of Our believing servants.112And We gave him the good news of Ishaaq, a Prophet, one of the Righteous.

mara ya kwanza aliondoka akiwa mjamzito halafu akakutana na malaika akambwambia arudi na ajinyenyekeshe kwa bosi wake (Sarah) na inaonekana alirudi, aliporudi ndo Isaka akazaliwa na furaha yoote ikawahamia kwa isaka ndo akaona uchungu na mwanae ndo akawa anamfanyia mocking Isaka ndo ***** kuona vile kamwambia Ibrahimu awaodnoe kwani hawatarith pamoja na mwanae
 
kwani waliondoka wote? na unaposema wamevamia una maana gani?

Katika kusoma historia sijawahi kukuta taifa linaitwa Palestina, wala lugha ya Wapalestina wala sijaona utamaduni wa kipalestina. Na kwa taarifa fupi tu Wayahudi ndio waliitwa Wapalestina na Gazeti lao maarufu liliitwa Palestinian Post (kama sijakosea spelling).

Ninachokikuta katika historia ni kuwa Warumi baada ya kuwa wamesumbuliwa na wayahudi kwa muda mrefu kwa uasi wao usiokoma tangu enzi za Yuda Makabayo vs Antichus Epiphanes wakaamua kuwasambaratisha kama taifa. Wakaua wengi sana kulingana na Josephus, et al na wakaibadili jina Yudea na Samaria na kuiita Palestina. Hawakuwafukuza wote wapo waliobakia ingawa wengi walipelekwa uhamishoni.

Hii si mara ya kwanza katika historia wao kufanyiwa hivi.......

Kabla hujasema wamevamia ungetuambia historia ya wapalestina ili tupime. Objectively bila religious emotions. Maana haya mambo ni historia ambayo yeyote anaweza kuchimbua na kuona!
wayahudi waliobaki walichanganyika na jamii mbalimbali hapo palestine,ujua palestine siyo race bali ni jina la eneo hilo lilianza kutumika enzi za utawala wa warumi.sasa yataka ujue kuwa hawa waliorudi palestine toka nchi za ulaya ni uzao wa wayahudi waliokimbilia huko miaka ya nyuma,wakaenda kuingiliana na wazungu huko ndo baadae wakarudi kulazimisha kuanzisha taifa la israel mwaka 1948.ukimwangalia mfano netanyahau ni myahudi mwenye asili ya russia.na kiukweli ni mzungu copyright,sasa ndo ujiulize ni halali kwa mgoni kurudi africa kusini na kuclaim ardhi.
 
hebu tuanche ubishi twende kwenye simple logics and imagination. Unadhani solution ya mgogoro huu itakuwa ipi na itakuwa implemented kivipi. Au hata tukilalamika unadhani ili wayahudi waondoke hapo au waarabu waondoke hapo nini kinatakiwa kifanyike na je itaakua realistic
Kwa mimi ninachokiona Wayahudi wako tayari kusemwa kivyovyote vlie na hawako tayari kubadilika, jeje nini kifanyike na je kitawezekana?
 
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom