Hivi ni sahihi mitandao ya simu kuingiza tena sokoni namba ya simu ambayo haijatumika kwa muda fulani?

mimi najipigiaga nikijiskia.
airtel wanaongoza kwa huu ujinga line isipokua hewani hata week3 ujue umeumia.
utaanza kupigia mtu yuko mahenge akutumie code za whatsapp
Mimi ni mhanga wa hili, Airtel waliuza line yangu niliyotumia kwa zaidi ya miaka 10 ( Toka ikiwa Celtel, baada Zain na hatimae Airtel ) kwa kutoitumia kwa miezi miwili tu!
 
Teh teh teh
Baada ya kuona uzi huu, nikaona niicheck laini yangu ya voda niliyokuwa nimeiweka dirishani kwa takriban mwaka na nusu.

Kuiweka tu hewani inaniomba PUK, nikaitafuta nikaweka. Ile inawaka tu inaniandikia " sim card can't be registered" Oooh yamenikuta
Nikazima sim nikaiwasha imo, yaani ikakubali .
Nikaanza kutest mitambo. Nikadial *102# ngoma sifuri, *149*60# dakka 60 vd to vd 20 allnet mb890 zinaisha 2019-12-14
what a magic!!!!
 
Laini yangu sikuitumia mwezi mmoja siku najaribu kuipiga anapokea mwanamke yuko mahenge.
Nimesajiri laini ya airtel mpya ila kila mara nimekuwa nikipigiwa simu na wakurya wa mara wanamuulizia Chacha karibu kila siku imekuwa kero sasa.
warudishie chacha wao
 
Teh teh teh
Baada ya kuona uzi huu, nikaona niicheck laini yangu ya voda niliyokuwa nimeiweka dirishani kwa takriban mwaka na nusu.

Kuiweka tu hewani inaniomba PUK, nikaitafuta nikaweka. Ile inawaka tu inaniandikia " sim card can't be registered" Oooh yamenikuta
Nikazima sim nikaiwasha imo, yaani ikakubali .
Nikaanza kutest mitambo. Nikadial *102# ngoma sifuri, *149*60# dakka 60 vd to vd 20 allnet mb890 zinaisha 2019-12-14
what a magic!!!!
labda bando limesaidia
 
Mimi na kesi na hawa tigo wana mambo ya ajabu sana.
Nilikua na line ya tigo ambayo nimeitumia takribani 4yrs hivi. sasa nikaitoa hewani kwa muda kama wa mwaka moja hivi
Sasa .kuna kipindi nikawa nimefulia mbaya ikabidi ni mcheki mwanangu moja hivi ili anitumie pesa .
mshikaji akasema poa kwa kawaida mshikaji akikwambia anakutumia hela mkikata simu tu .baada kama ya dk 10 hivi utapokea ujumbe muhalama umethibitishwa .
sasa siku iyo nikaona kimya nikajua mwana nae haka kaupepo ka hawamu ya tano katakua kamempitia lakini jamaa sio mtu wa chenga chenga imean yuko straight kama hana ana kwambia hana.
nikajiuliza huyu mwana kwanini anipe matumaini hewa nikaamua kumcheki nimuulize kulikoni mbona kimya .
Akaniambia mbona hela nimetuma toka jana akani fwadia ile sms ya muhamala .kucheki kanitumia kwenye namba yangu ya tigo ambayo nina kama mwaka hivi sijaitumia
nikasema isiwe issue coz line ninayo gheto ngoja nikaiweke kwenye cm duh naweka kwenye simu network inasoma fresh lakini nikipiga menyu yao ya tigo pesa hainipi feedback.
nikasema isiwe kesi ngoja niwaibukie tigo kwenye shop zao nilipofika shop wakaniambia line yangu wameifunga nikawaambia kama wameifunga mbona mihamala inakubali na nikipiga namba haipatikani wakasema ndo inakua ivyo nikasema isiwe kesi basi tufanye kama tuna swap ili nipate ile ile namba.
wananiambia haiwezekani iyo mambo nikawaambia mbona nikajaribu kuitumia iyo line pesa bado inasoma jina langu wakakosa majibu ya kunipa waniambia ni mwambie jamaa apige simu warudishe muhamala. Hawa tigo nimeshindwa kuwa elewa mpaka leo namba ni metumia for 4 good yrs alafu wanaipiga bunn kirahisi rahisi tu.
 
Hili swala lije lifwatiliwe maana linaleta usumbufu kwa watu.Watu tukipotea hewani kidogo unashangaa baada ya muda hiyo line imeshauzwa au ukinunua line mpya kila mara unapigiwa simu na watu wanamuulizia mmiliki wa awali wengine unakuta ni wanaume waliotelekeza familia zao alafu wake zao kila siku nikupiga simu zakulalamika nakutuma mesej zamatusi.Mwaka jana nilisajili line mpya ya airtel baada ya yamwanzo kupotea na nikashindwa kukidhi masharti yakuirenew sasa baada ya siku nikapigiwa simu na namba kama yangu ila ya voda mtu akajitambulisha kua hiyo namba ilikua yake akapoteza simu kwaiyo alitaka kuirenew ila anashangaa iko hewani nikamwambia aje tuonane tulivyokutana nikaona ni mdada mrembo ikabidi nitumie fursa kua naye kwaiyo sasa hivi niwapenzi tulionganishwa na namba.Ila kiujumla hii kitu sio nzuri na nategemea usajili huu wa alama za vidole umalize hii changamoto.
 
Pole mkuu.
Airtel wamenipigia ikifika 31 Dec 2019 sijasajili alama za vidole line itafungwa.
Sijui wanataka kunifanyia mnachosema?
Mimi niko kitandani nimepooza miguu japo naongea na kuandika watakuwa hawajanitendea haki waje hapa kitandani wachukue alama zao.Mimi ni mteja wao toka wanaitwa Celtel-Zain-Airtel au lugha nyepesi toka waje nchi hii nimewachangia mno.
 
hii kitu inakera sana, binafsi nikitaka kumtumia mtu hela namuuliza kwanza je hiyo namba yako ni active kuepusha usumbufu. nina line yangu ya airtel ipo kwenye kitochi siihudumii kwa chochote isipokuwa tu nahakikisha ipo hewani muda wote kitochi hakizimwi, sijui napo watanifungia au.
moja ya ndugu zangu kila wakati anatumiwa sms za alerts za credit,debit na statement kutoka bank asiyotumia. hili swala mitandao ya simu iliangalie upya haswa airtel na voda.
 
Dah Leo ndo nimejua
Unakuta unayempigia yupo MWANZA anayepokea Yuko Tandahimba kwa harmonize, unaanza kuambiwa kimakonde kiroho safi unakata bila hata kuuliza jina.
mimi najipigiaga nikijiskia.
airtel wanaongoza kwa huu ujinga line isipokua hewani hata week3 ujue umeumia.
utaanza kupigia mtu yuko mahenge akutumie code za whatsapp
 
Mie kila mara napigiwa na watu wakimuulizia Mr Chambi, wengine wananigombeza kabisa wakitaka nimpe mwenye simu waongee nae
... dalili tosha unatumia iliyokuwa laini ya marehemu Mkuu pengine baadhi ya marafiki na jamaa zake hawajui jamaa yao kashatangulia. Hapo ndipo makampuni ya simu yanapokosea, kabla ya kuuza laini zisizotumika fasta fasta wangeweka on hold kwa muda wa kutosha - 3 yrs say kabla ya kurudisha hizo namba kwenye matumizi.

At least 3 yrs habari za mmiliki wa zamani kutokutumia tena namba yake hiyo au kutangulia mbele ya haki zinakuwa zimeenea kwa jamaa zake wote hivyo kupokea calls za ajabu ajabu kutoka kwa watu "wasiofahamika" zingepungua. But sijui 3 weeks, 6 months too short duration.
 
Dah Leo ndo nimejua
Unakuta unayempigia yupo MWANZA anayepokea Yuko Tandahimba kwa harmonize, unaanza kuambiwa kimakonde kiroho safi unakata bila hata kuuliza jina.
ukiona una namba ya mtu wa airtel umepiga haipatikani mwezi mmoja
mwezi unaokuja ikipatikana anapokea mazola yuko Morogoro
 
... dalili tosha unatumia iliyokuwa laini ya marehemu Mkuu pengine baadhi ya marafiki na jamaa zake hawajui jamaa yao kashatangulia. Hapo ndipo makampuni ya simu yanapokosea, kabla ya kuuza laini zisizotumika fasta fasta wangeweka on hold kwa muda wa kutosha - 3 yrs say kabla ya kurudisha hizo namba kwenye matumizi.

At least 3 yrs habari za mmiliki wa zamani kutokutumia tena namba yake hiyo au kutangulia mbele ya haki zinakuwa zimeenea kwa jamaa zake wote hivyo kupokea calls za ajabu ajabu kutoka kwa watu "wasiofahamika" zingepungua. But sijui 3 weeks, 6 months too short duration.
Hapana sio marehemu, bali hiyo namba haitumii tena. Kuna mmoja aliwahi kunipigia nilipokwambia hii namba naitumia mimi kwa sasa, akasema ngoja amtafute kwa namba nyingine. Baadae akanipigia na kuniambia ameshampata.
 
Ngoja niwe mbishi pia haiuzwi tena.
Ila ikikaa bila kutumika kwa muda unaweza piga ikapokelewa na MTU mwengine.
Nadhani huyu wanakuwa wemempatia bureee.
Kwamba wanaenda mtaani kugawa line bure au kupewa bure namna gani
 
Back
Top Bottom