Hivi ni sahihi media kutangaza mambo ya ushirikina? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Hivi ni sahihi media kutangaza mambo ya ushirikina?

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by crome20, Nov 5, 2011.

 1. crome20

  crome20 JF-Expert Member

  #1
  Nov 5, 2011
  Joined: Feb 5, 2010
  Messages: 833
  Likes Received: 105
  Trophy Points: 60
  Wana JF, Juzi nilistuka sana kusikia Redioni tangazo la Mganga wa kienyeji llililokuwa linatoa taarifa kuwa tiba zifuatazo zinapatikana1. Kupanda cheo kazini 2. Kuvuta wateja( mvuto wa biashara) 3. Pete za bahati 4. Mapenzi n.k. .Nikajiuliza, hivi kama mojawapo ya kazi ya chombo cha habari ni kuelimisha , kwa kutoa matangazo hayo tena kwa mbwembwe ni sahihi katika zama hizi za science na technologia? Hivi mtu mwingine akiona tangazo gazetini au kusikia redioni si atasema taarifa hii imeaminiwa na ndio maana inatangazwa redioni! Kuna njia yoyote ya kupanda cheo bila kuchapakazi na kujiendeleza kielimu kweli, mimi nadhani kuna haja ya taaluma ya habari kuheshimika na sio kutumika kupotosha jamii au mnasemaje wana jamii?
   
Loading...