Hivi ni sahihi kwa wanajeshi kuwaadhibu raia?

Khalu

JF-Expert Member
Oct 3, 2017
525
565
Habarini wanajamvi.

Nadhani sote tunafahamu habari za hawa jamaa, na huwenda kuna watu walishapata kukumbana na kasheshe la hawa jamaa.

Japo watu huwa wanahadithiana stori za hawa jamaa kama mambo ya kawaida lakini kiuhalisia hawa jamaa huwa wanaadhibu raia.

Mifano ni mingi, hata mimi mwenyewe nilishawahi kudhibiwa mara moja, na mara moja niliwahi kukoswakoswa, yaani siku ile wangeamua kuniadhibu sijui ingekuwaje???? maana niliingia ndani ya utepe mwekundu waliouweka.

Sasa swali langu ni je hili suala ni sahihi kwa wanajeshi kuwaadhibu raia, yaani hawa jamaa wamepewa green light kuwa wanaweza kumuadhibu raia?

Na je, hili suala tunalitazama vipi kama raia?

Hivi hata wanajeshi wa huko nchi za wenzetu nao wanafanya hivihivi?

Nb: ukitoa sababu zinazohusiana na usalama wa nchi.
 
Ngoja waje wajuvi wa mambo, Nafikiri hawa wa Jeda wao wanatoaga onyo tu kwa raia kukuadhibu hawa Jamaa na hisi mpaka uhatarishe usalama wa Nchi tofauti na hapo sidhani ila sina uhakika ngoja tuwasubiri tu wa wajuvi wa mambo haya maana
 
Habarini wanajamvi.

Nadhani sote tunafahamu habari za hawa jamaa, na huwenda kuna watu walishapata kukumbana na kasheshe la hawa jamaa.

Japo watu huwa wanahadithiana stori za hawa jamaa kama mambo ya kawaida lakini kiuhalisia hawa jamaa huwa wanaadhibu raia.

Mifano ni mingi, hata mimi mwenyewe nilishawahi kudhibiwa mara moja, na mara moja niliwahi kukoswakoswa, yaani siku ile wangeamua kuniadhibu sijui ingekuwaje???? maana niliingia ndani ya utepe mwekundu waliouweka.

Sasa swali langu ni je hili suala ni sahihi kwa wanajeshi kuwaadhibu raia, yaani hawa jamaa wamepewa green light kuwa wanaweza kumuadhibu raia?

Na je, hili suala tunalitazama vipi kama raia?

Hivi hata wanajeshi wa huko nchi za wenzetu nao wanafanya hivihivi?

Nb: ukitoa sababu zinazohusiana na usalama wa nchi.
Mwanajeshi haruhusiwi kumuadhibu raia kwa jambo lolote,labda wasingizie ulitaka kumdhuru ama kupora silaha.

Kinyume na hapo ni uoga wa watz kudhani kwamba jamaa wanaruhusiwa kupigapiga tu
 
Huku AFRIKA mtu akishakabidhiwa magwanda basi anawaona raia kama vikatuni na anaweza kumfanya lolote na asifanywe lolote......watu pekee wanaowaogopa ni wanasiasa tu.......
 
Swala la kujichukulia sheria mkononi hakikubaliki popote na haliko pia kwenye katiba yetu.. Huo ni uhalifu na uvunjifu wa haki za binadamu
Basi hili watu inabidi waelimishwe maana huwa wanachukulia mwanajeshi ni kama mtu fulani mwenye uhalali kufanya hivyo kwa raia.
 
Mwanajeshi haruhusiwi kumuadhibu raia kwa jambo lolote,labda wasingizie ulitaka kumdhuru ama kupora silaha.

Kinyume na hapo ni uoga wa watz kudhani kwamba jamaa wanaruhusiwa kupigapiga tu
Na hapa kwenye kuogopwa wamefanikiwa sana maana wanaogopwa kweli.

Nakumbuka kuna konda mmoja alimuomba jamaa abiria msamaha baada ya kuwa walipisha kauli, ila alifanya hivyo baada ya kuhisi huwenda jamaa ni mjeshi.

Ila asingekuwa mjeshi Wala asingefanya hivyo, yaani hadi watu walikuwa wanacheka kwa jinsia yule konda alivyokiwa akiomba msamaha,
maana ilikuwa dakika mbili amempandishia dakika mbili akaomba msamaha
 
Hawana haki ya kumuadhibu raia kwa lolote
Huwa wanavunja sheria kwa kuwa wananchi ndio wamewatengenezea mfumo huo wa kuwaogopa
Eti unite karibu na eneo lao unapigwa na kurushwa kichura
Huo ni uhuni kama uhuni mwingine

Hakuna sheria inasema mjeda anaweza kumpiga au kumpa adhabu raia
Huo ni uonezi na ninashangaa kwanini waandishi wa habari hawa makanjanja wanashindwa kumuuliza mkuu wao hili swali?

Kwani wakimuuliza nao watatushwa kichura?

Acheni kuwa dhalili nyie
Hatukuwa kufundishwa kupiga na kuonea raia
Ni woga wenu tu na umewafanya wao wawe bullies
 
Sasa hivi hata SUMA JKT wanaiga hii tabia ya kutandika raia huko kwenye mageti ya ofisi wanazolinda.

Ni kosa kisheria.
 
Hawana haki ya kumuadhibu raia kwa lolote
Huwa wanavunja sheria kwa kuwa wananchi ndio wamewatengenezea mfumo huo wa kuwaogopa
Eti unite karibu na eneo lao unapigwa na kurushwa kichura
Huo ni uhuni kama uhuni mwingine

Hakuna sheria inasema mjeda anaweza kumpiga au kumpa adhabu raia
Huo ni uonezi na ninashangaa kwanini waandishi wa habari hawa makanjanja wanashindwa kumuuliza mkuu wao hili swali?

Kwani wakimuuliza nao watatushwa kichura?

Acheni kuwa dhalili nyie
Hatukuwa kufundishwa kupiga na kuonea raia
Ni woga wenu tu na umewafanya wao wawe bullies
Kwakweli wenye mamlaka inabidi watoe elimu kwa jamii juu ya hili suala na kulikemea.

Maana mentality ya kuwaogopa wajeshi imeenea kwa wengi katika raia hivyo kuona ni sahihi kwa wao kufanya hivyo.

Sio siri watu wengi hawafahamu juu ya hili suala.
 
Ni ujinga tu
Na wameamini kuwa mwanajeshi mmoja anaweza kupiga raia kumi

Ila watu wameanza kuamka na wengine wakifumaniwa wanapigwa haswa
 
Ni uvunjaji wa sheria, ukifanyiwa vile ripoti kwenye kikosi chake, hatarudia tena. Mmoja alimuadhibu jamaa kisa kasikia tu anatembea na mke wake na hana ushahidi, jamaa alipokea kipigo cha mbwa.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom